Kiungulia Kwa Mjamzito

kiungulia kwa mjamzito
mjamzito

Nini sababu ya kiungulia kwa mjamzito?

Ukiwa mjamzito unategemea kwamba ni kawaida utavimba miguu na vidole na kupata kichefuchefu hasa nyakati za asubuhi. Linapokuja swala la kiungulia waweza kujiuliza nini hasa sababu? Je ni chakula ulichokula au ni kitu gani kingine kimesababisha?

Kiungulia ni nini

Kiungulia ni ile hali ya kupatwa na tindikali inayopanda kutoka tumboni mpaka kooni na kusababisha maumivu makali kifuani. Dalili zingine unazoweza kujisikia ni pamoja na

  • tumbo kujaa gesi
  • kubeua kila mara
  • uchachu mdomoni
  • kupata malengelenge kwenye mdomo na
  • kukohoa mara kwa mara

Mjamzito anaweza kupatwa na kiungulia na changamoto ya choo kigumu katika umri wowote wa mimba yake. Japo hali hii inatokea zaidi kuanzia miezi 6 ya ujauzito.

Sababu Zinazopelekea Kiungulia Wakati wa Ujauzito

1.Mabadiliko ya Homoni

Kiwango cha homoni ya progesterone huongezeka zaidi wakati wa ujauzito ili kujenga zaidi kizazi na mtoto. Kuongezeka kwa homoni hii ndio chanzo kikubwa cha kiungulia chako.

Kazi ingine ya homoni ya progesterone ni kufanya misuli ilegee. Hali hii yaweza kupelekea misuli ya koo la juu kulegea zaidi na hivo kuruhusu tindikali ya tumboni kupanda juu na kizuizi.

Unapokula misuli ya valve za kwenye koo huachia ili chakula kiingine tumboni, kisha hufunga ili chakula kisirudi juu. Wakati wa ujauzito homoni inaongezeka na kufanya misuli kutojifunga vizuri na hivo chakula cha tumboni kurudi juu.

2.Ukuaji Wa Mtoto Tumboni

Kadiri mtoto anakua tumboni anachukua nafasi zaidi na kupunguza nafasi ya viungo vingine vya mwili. Ni kama vile unavyobinya dawa ya meno upige mswaki, mfuko wa mimba unapoendelea kukua unaweka presha tumboni, na kufanya asidi ya tumboni kutoka hasa kama tumbo limejaa.

Kadiri mimba inavozidi kukua ndivyo inabinya zaidi tumbo la chakula na hivo asidi kuendelea kutoka. Hii ni sababu kwanini tatizo huwa kubwa zaidi unapokaribia kujifungua.

Nini cha Kufanya Kupunguza Kiungulia Kwa Mjamzito?

  1. Tazama unachokula: vyakula vyenye tindikali na vile vichachu ni chanzo cha asidi nyingi tumboni. Punguza vyakula na matunda machachu, nyanya, vitunguu maji, kahawa na chai nyeusi, chokleti, soda ,tangawizi na vyakula vilivyokaangwa kama chips.
  2. Kula Mara nyingi kidogo kidogo badala ya kula milo mikubwa mitatu katika siku
  3. Unapokula hakikisha unakaa ukiwa umenyooka, usijipinde, itasaidia chakula kuteremka vizuri tumboni.
  4. Masaa matatu kuelekea kulala usile chakula. Unapolala yatakiwa kuwe hakuna chakula tumboni itakusaidia kukontroo kiungulia .
  5. Usivute Sigara: Kemikali zilizopo kwenye sigara zinafanya kulegea kwa valve zinazouzia chakula kutoka.
  6. Unapolala hakikisha unaweka mto: Hakikisha unapoenda kulala eneo la juu la kichwa linakuwa juu kidogo.
  7. Vaa nguo pana zisizobana
  8. Kunywa maji baada ya kumaliza kula na siyo katikati ya mlo
  9. Usitumie pombe: Pombe ni mbaya hata kwa ukuaji wa mtoto maana hupelekea mtoto kuwa na ulemavu wa ubongo na viungo. Pombe pia hufanya valve za kwenye koo la chakula kulegea na hivo kuruusu chakula kurudi juu.

Muone Daktari

Hali ikiwa mbaya hakikisha unaenda hospitali, kwa kulingana na hali yako ya ujauzito, daktari atapendekeza dawa za kukupatia. Usimeze dawa bila kupata ushauri wa daktari maana zinaweza kukudhuru.

Bofya kusoma kuhusu: Bawasili kwa mjamzito+Ushauri

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *