Chanzo cha uke mkavu na kukosa ute wa mimba
Ute wa mimba ama ute unaovutika ni muhimu sana kwenye ishu ya mimba kutunga. Ute unaovutika mithili ya yai unasaidia mbegu kuogelea na kupenya kwenye mlango wa kiazi mpaka kwenda kulirutubisha yai kwenye mirija. Baadhi ya njia za kupanga uzazi zinapelekea kukosa ute wa mimba ili usishike mimba isiyotarajiwa.
Malelezo ya utangulizi kuhusu kukosa ute wa mimba
Changamoto ya kukosa ute wa mimba inachangia pia uchelewe kushika mimba. Baadhi ya wanawake watahitaji kutumia kwanza dawa za kuongeza ute ili kushika mimba mapema.
Umri mkubwa, maambukizi , magonjwa na kuvurugika kwa homoni ni baadhi ya vitu vinavyochangia kukosa ute wa mimba. Dawa pia za uzazi zinaweza kusababisha ukose ute wa mimba.
Jinsi Mimba inavyofanyika
Yai linapokomaa hutolewa kwenye mfuko wa mayai ili kurutubishwa, kitendo hiki huitwa ovulation. Kikawaida kila mwezi yai moja hukomaa na kutolewa kwenda wenye mirija ya uzazi lipate kurutubishwa.
Yai linakuwa salama masaa 12 mpaka 36 kusubiri mbegu ije irutubishe. Kama mbegu zinaweza kuishi mpaka siku 5 kwenye kizazi maana yake unaweza ukashika mimba ukifanya tendo la ndoa kwenye siku za mwisho za hedhi. Siku ambazo zinakaribiana na siku za yai kupevuka.
Kazi ya ute wa mimba
Ute ute laini unaovutika ni muhimu ili kuweka mazingira mazuri ya kushika mimba. Siku chache kabla ya ovulation ute ute laini wa kuvutika huanza kuzalishwa kwa wingi kwenye mlango wa kizazi.
Katika ulaini wake ute huu unaleta mazingira mazuri kwa mbegu za mwanaume kuogelea kupenya mlango wa kizazi. Changamoto yoyote kwenye ute maana yake mbegu haitapenya na mimba haitatungwa.
Chanzo cha kukosa ute wa mimba
Kukosa ute unaovutika inaweza kuchangiwa na vitu hivi
1.Kusafisha uke kupita kiasi (Douching)
Kuosha uke mara kwa mara hupelekea kuondoa bakteria wazuri na hivo kuongezeka hatari ya kuapata maambukizi na pia kupungua kwa uteute ukeni. Ni muhimu kuacha kuosha uke mpaka ndani zaidi, badala yake osha mwanzoni tu mwa uke. Pia uepuke kutumia sabuni na manukato ukeni.
2.Maambukizi hupelekea kukosa ute wa mimba
Maambukizi ya bakteria au fangasi kwenye uke hupelekea ukavu na kukosa ute wa mimba. Fangasi ukeni husababisha dalili za muwasho, kutokwa na uchafu mwingine mweupe na maumivu kwenye tendo.
Harufu mbaya ukeni ni dalili ya maambukizi ya bakteria. Ni muhimu kumweleza daktari anayekutibu kuhusu dalili zote unazopata. Magonjwa ya zinaa pia yanaweza kupelekea ukose ute wa mimba pamoja na kuziba kwa mirija ya uzazi kama hutatibiwa mapema.
3.Matumizi ya Dawa za kupevusha mayai za Clomid
Siyo kila mwanamke anayemeza dawa hizi anakosa ute. Kwa wanawake wanaotumia dawa hizi kwa muda mrefu, wanapata changamoto ya kukosa ute ute wa mimba. Endapo utagundua uke wako ni mkavu ama unakosa ute wa mimba baada ya kumeza clomid, mjulishe daktari mapema. Daktari ataweza kukupa dawa zingine kuondoa madhara haya.
4.Umri
Kadiri umri unavyokwenda ndivyo siku za kupata ute unaovutika zinavyopungua. Kwenye umri wa miaka 20′ unaweza kupata uteute mpaka siku tano katika mzunguko wako wa hedhi.
Kwenye miaka ya 30’s na 40’s siku za kupata ute hupungua mpaka mbili ama moja.Nyakati zingine ute unaweza kubaki tu kama majimaji na usivutike kama yai.
5.Uzito mdogo kupita kiasi
Homoni ya etsrogen ndio kichocheo kinachopelekea mwili kuzalisha uteute wa mimba. Watu wenye uzito mdogo sana, na wanaofanya mazoezi makali, wana kiwango kidogo cha estrogen. Kupata lishe nzuri, kupunguza mazoezi na kuongeza uzito yaweza kusaidia kama hichi ndio chanzo cha tatizo lako.
6.Kuvurugika kwa homoni
Kwa wanawake wengi hiki ndio chanzo kikubwa cha kukosa ute ute wa mimba. Kama mayai hayapevuki, huwezi kupata ute ute wa mimba. Pia inawezekana ukapata uteute lakini mayai hayapevuki, yategema tu na chanzo cha tatizo.
Baadhi ya changamoto zinazopelekea mayai yasipevuke ni pamoja na matatizo ya tezi ya thyroid, kuongezeka kwa homoni ya maziwa, vimbe kwenye mayai, na kukoma hedhi mapema.
Tumia vidonge asili vya Evecare kurejesha uteute wako
Evecare ni dawa asili na imetengenezwa nchini India kupitia mimea ua Ashoka, Asaparagus na lodh tree. Kwa miaka zaidi ya mitano ambayo tumekuwa tukihudumia wagonjwa wetu wa matatizo ya homoni, tumepokea shuhuda lukuki.
Dawa itakusaidia kurekebisha homoni ili uanze kupata ute ute mwingi. Evecare inakuwa na vidonge 30, unameza vidonge viwili kila siku kwa muda wa wiki mbili.
Baada ya kutumia Evecare tegemea kupata matokeo haya
- Uteute kuwa mwingi na uke wako kuwa na afya njema
- Maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi kuisha kabisa
- Homoni kubalansi
- Mzunguko wa hedhi kurekebika na kuanza kupata kila mwezi
- Kizazi kuimarika sana hata kuongeza chansi ya kushika mimba kama wewe ni muhanga wa kukosa mimba kwa muda mrefu.
Bei ya Evecare ni Tsh 75,000/=
Ushuhuda
Hapa chini kwenye picha inaonesha mafanikio aliyopata mgonjwa wetu Munira kutokana na kutumia dawa zetu.
Tahadhari
Kuna wimbi kubwa la wajasiliamali mitandaoni wanauza vidonge fake vya evecare, tena wanauza kwa bei rahisi sana. Watu hao siyo madaktari wala siyo wataalamu wa afya na wanauza bidhaa feki ambazo ni hatari wa afya yako. Wengi wao hawana hata ofisi, ukipata madhara unakosa pa kuuliza. Kuwa makini na watu hao, wamejaa sana insta na fb