Wanaume wengi kwa sasa wanapata shida ya kuvuja shahawa pasipo kufanya tendo. Na hii ndiomaana tumeandika makala hii kukwelekeza chanzo cha tatizo na tiba.
Kwanza yatakiwa kujua nini maana ya shahawa. Shahawa ni ule ute mweupe ambapo hutoka kwenye uume wakati wa tendo la ndoa. Ute huu unazalishwa na tezi dume ili kubeba mbegu, na kusaidia mbegu kuogelea. Kwenye shahawa kunakuwa na kiwango kidogo tu cha mbegu.
Shahawa kwa kiasi kikubwa zinaweza kutoka kipindi ukiwa na hisa za mapenzi kwenye tendo au ukipiga punyeto. Lakini sometime shahawa zaweza kutoka bila hata msisimko wa kimapenzi.
Kuvuja shahawa ni kawaida wakati unajiandaa kufanya tendo ama kwenye tendo lenyewe. Pia kuna changamoto zinaweza kupelekea shahawa kuvuja, baadhi ya changamoto zinahitaji kutibiwa na zingine wala hazihitaji tiba.
Vipi kama natafuta mtoto bila mafanikio?
Ikiwa unavuja shahawa na unatafuta mtoto mda mrefu bila mafanikio, na una changamoto ya nguvu za kiume, itahitaji kuonana na daktari specialist wa magonjwa ya njia ya mkojo yani urologist.
Nini kinapelekea kuvuja shahawa au mbegu
Ukiacha swala la tendo la ndoa, mambo mengine yanayofanya kuvuja kwa mbegu ni pamoja na
1.Ndoto Nyevu(nocturnal emissions)
Ndoto nyevu zinatokea sana kipindi cha kubalehe. Wanaume wengi wanapitia hii hali kutokana na ukuaji.
Hiki ni kitendo cha kuvuja mbegu bila hiyari wakati umelala. Inaweza kutokea wakati unaota ndoto ya mapenzi au via vya uzazi vimesuguana na mashuka ya kulalia.
Tiba ya ndoto nyevu
Kwa wanawaume wengi hii ni hali ya kawaida na haihitaji dawa zozote. Ni hali ya mabadiliko ya mwili unapoingua utu uzima. Ndoto nyevu zinaongezeka zaidi pale ukikosa mwanamke wa kufanya nae tendo na kama kupiga punyeto.
2.Athari ya madawa
Baadhi ya madawa kama ya kupunguza msongo wa mawazo yanaweza kupelekea kuvuja shahawa. Dawa hizi pia zaweza kukuletea changamoto zingine kama
- kukosa hamu ya tendo
- kuchelewa kumwaga mbegu
- kushindwa kusimamisha uume vizuri
3.Kuugua Tezi Dume
Tezi dume ni tezi inayozaliusha majimaji yanayobeba mbegu za kuzisafirisha mpaka nje ya uume. Kiungo hiki kinaweza kupata hitilafu nyingi sana ikiwemo saratani na kushambuliwa na vimelea. Tezi inaweza kushambuliwa na bakteria, fungus na hata virusi.
Dalili za tatizo kwenye tezi dume ni pamoja na
- kushindwa kukojoa vizuri
- maumivu ya tumbo la chini, mkundu na chini ya mgongo
- homa
- mkojo wenye harufu kali
- maumivu wakati wa kukojoa
- uume kutosimama na kushindwa kabisa kufanya tendo na
- kukosa hamu ya tendo
Matibabu ya tezi dume
Endapo unapata hizi dalili mbaya, uende hospitali mapema kupata vipimo. Kama daktari atagundua kuna maambukizi ya bakteria atakwanzishia antibiotic.
Saratani ya tezi dume kidogo ni tatizo kubwa linalohitaji uangalizi wa karibu. Vipimo vya mara kwa mara vitahitajika ili kufatilia kama saratani inasambaa au la.
Upasuaji waweza kuhitajika ili kuondoa kabisa tezi dume. Kumbuka aina na ukubwa wa tiba utategemea na hatua ya saratani yako.
4.Athari kwenye mishipa ya fahamu.
Mishipa ya fahamu inapoathirika, yaweza kupelekea tatizo kwenye utoaji wa mbegu na kusababisha kuvuja mbegu. Umri mkubwa, maradhi, ajali na hata upasuaji kwenye uti wa mgongo au kwenye mapumbu yaweza kuathiri mishipa ya fahamu.
5.Kuvuja shahawa wakati wa kukojoa
Hili ni tatizo kubwa kwa wanaume. japo siyo mara zote ni tatizo, lakini yatakiwa ufatilie kwa umakini shida ilipoanzia. Unaweza kuwa unaugua magonjwa ya zinaa, na kupelekea utoe shahawa kwenye mkojo. Pia waweza kuwa na magonjwa ya figo na tezi dume.
6.Mbegu kurudi ndani (retrograde ejaculation)
Wanaume wenye tatizo hili hawatoi mbegu baada ya kufika kileleni yani dry orgasms. Ukiwa na tatizo hili mbegu badala ya kutoka nje , zinarudi ndani kwenda kwenye kibofu cha mkojo. Tatizo linatokana na msuli wa kwenye mrija wa mkojo kutofunga vizuri wakati wa tendo. Hali hii yaweza kupelekea baadae ukojoe vitu vyeupe ambavyo ni mbegu.
Japo wanawaume wengi hupata hii hali, na yaweza isiwe tatizo kubwa ila itakukwamisha kumpa mwanamke mimba.
Tiba ya tatizo la kuvuja shahawa bila ridhaa
Ikiwa tatizo linajirudia unatakiwa kupata usaidizi wa daktari. Usipuuze kabisa endapo dalili zinaendelea kwa mda mrefu. Tiba itategemea na chanzo cha tatizo, kazi ya daktari itakuwa ni kukusaidia kujua shida imeanzia wapi na kukupa tiba ya chanzo.
Lini unatakiwa kumwona daktari?
Kuvuja shahawa mara mojamoja wala siyo ishu kubwa. Lakini kama kuvuja huku kunatokea mara kwa mara hii inaweza kuwa shida. Mwone daktari endapo kuvuja kwako kwa mbegu kunaambatana na
- damu kwenye shahawa au mkojo
- shahawa kunuka
- mabadiliko kwenye utoaji wa mbegu
- maumivu makali unapotoa mbegu au kukojoa
- kutokwa na uchafu usio wa kawaida kwenye uume
Dalili hizi zaweza kuashiria tatizo kubwala kiafya, linalohitaji kutibiwa mapema
Soma makala zinazofuata kuhusu