Je ni salama kula udongo?
Kitaalamu changamoto ya kula udongo huitwa geophagia. Ni utaratibu wa miaka mingi sana kwa watu wa rika zote kupenda kula udongo.
Baadhi ya watu wenye upungufu wa damu pia hupenda sana kula udongo na kundi lingine kubwa ikiwa na wanawake wajawazito.
Japo watu wengi husjikia vizuri wanapokula udongo lakini tabia hii ina madhara makubwa mengi sana kiafya. Ulaji wa udongo kwa muda mrefu unakuweka kwenye hatari ya kuugua matatizo kama
- minyoo
- matatizo ya tumbo
- vimelea kama amiba
Hapa chini kuna maelezo ya kina kuhusu tatizo la kula ugongo pamoja na sababu zinazopelekea mtu kuwa mlevi wa udongo na nini ufanye ili kupuka kula udongo.
Sababu za Mtu Kupenda Kula Udongo
Kula udongo kunaweza kusababishwa na vitu mbalimbali ikiwemo
Ugonjwa wa Kula Vitu Visivyo Chakula (PICA)
Kama una ungonjwa wa PICA- changamoto inayokufanya upende kula vitu visivyo vyakula, unaweza kujisikia hamu pia ya kula udongo. Vitu vingine ambavyo mgonjwa huyu hupendelea kula ni pamoja na
- chaki
- nguo
- kalamu
- nywele
- karatasi na
- majivu na
- barafu
Tafiti zinasema tatizo linaweza kuibuka kutokana na mgonjwa kukosa virutubishi fulani muhimu mwilini. Katika mazingira fulani tatizo la kula vitu visivyoliwa linaweza kuisha endapo utakula kwa wingi vyakula vyenye madini chuma na lishe kamili kwa ujumla.
Utamaduni Wa Jamii Yako Kula Udongo
Baadhi ya jamii huamini katika kula udongo. Wewe pia waweza kujitengenezea tabia hii kutokana na jamii yako inavyo amini. Mfano jamii nyingi hula udongo wa kuamini kwamba udongo
- unawasaidia kutibu chngamoto za tumbo
- unafanya ngozi kuwa nyororo
- unakinga wakati wa ujauzito na
- kutibu magonjwa
Madhara Ya Kula Udongo
Kula udomgo kunaweza kusikusababishie madhara kwa haraka, lakini inaweza kuchangia kwa matatizo makubwa ya kiafya kwa siku za baadae. Kadiri unavozidi kula udongo ndivyo unaongeza zaidi hatari ya kupatwa na madhara makubwa ikiwemo
Kupungukiwa damu
Kula sana udongo kunaweza kuashiria una upungufu wa damu, lakini kula udongo hakuongezi damu kabisa. Ni muhimu kuonana na daktari akupime kiwango cha damu na kukwelekeza lishe ya kukufaa kuongeza damu.
Baadhi ya tafiti zinasema kwamba ulaji wa udongo unaongeza zaidi hatari ya kupungukiwa damu kwasababu udongo unapunguza kiwango cha madini chuma kinachofonzwa kwenye mwili.
Kupata bakteria na vimelea wengine hatarishi
Udongo umejaa bakteria na vimelea wengi wabaya. Kula udongo kunakuweka katika hatari zaidi ya kupata vimelea hawa ikimwemo minyoo.
Kukosa choo na kupata choo kigumu
Kukosa choo ni moja ya changamoto kubwa sana inayopwata walaji wa udongo. Kuziba kwa utumbo pia ni changamoto ingine inayoweza kukupata kwa kula udongo.
Matatizo ya ujauzito kutokana na kula udongo
Wajawazito wengi hupendelea kula udongo. Mabadiliko ya kinga ya mwili na mabadiliko ya homoni pia yanaweza kuchangia mjamzito kuwa mlevi wa udongo.
Kula udongo kwa mjamzito kunamuweka mtoto aliye tumboni kwenye hatari zaidi ya kukosa virutubishi sahihi, kutokana na udongo kuzuia ufonzwaji wa viini lishe tumboni.
Hatua Za Kukusaidia Kuacha Kula Udongo
Kama unataka kuacha ulevi wa kula udongo, fuata hatua hizi
- Zungumza na rafiki au mwanafamilia unayemwamini: Endapo utaweka wazi tatizo lako kwa ndugu ama rafiki mliyeshibana, atakupa sapoti wakati unapambana kuacha kula udongo.
- Kula au tafuna vitu vyenye mwonekano kama udongo: Unaweza kutafuna vitu vigumu au kunyonya icecream na kutafuna bublish kama mbadala wa kula udongo.
- Fika hospitali onana na daktari: Kama huna uhakika na sababu ya kukufanya uwe mlevu wa kula udongo, daktari ataweza kukusaidia kuchunguza chanzo cha tatizo na kukupa ushauri wa kina kupambana na tabia hii. Unaweza kuwa unakula udongo kutokana na kupungukiwa kwa viini lishe fulani. Daktari ataweza kukupa virutubisho mbalimbali kuziba upungufu huu.
Lini Watakiwa Kumwona Dakari
Kama umekuwa muhanga wa tatizo kwa muda mrefu, na umehisi kuna madhara ya kiafya umeshaanza kuyapata kwa kula udongo, ni muhimu sasa swala lako kulipeleka hospitali upate tiba na ushauri wa uhakika.
Kama umeanza kuona dalili zisizo za kawaida, na umekuwa ukila udongo kwa muda mrefu, unahitaji kumwona daktari mapema. Dalili hizi ni pamoja na
- maumivu wakati wa haja kubwa
- kukosa choo na kupata choo kigumu
- kuharisha
- kutapika na kichefuchefu
- pumzi kukata mara kwa mara
- kifua kubana
- mwili kukosa nguvu na uchovu na
- kujihisi tu mwili upo ovyo
Kuugua Tetenus kwa Kula Udongo
Inawezekana kabisa kuugua tetenus kwasbabau ya kula udongo. Tetenanus ni ugonjwa mbaya unaweza kutishia uhai wako. Muone daktari mapema endapo unapata dalili hizi
- maumivu kwenye taya
- misuli kukaza haya ya tumbo
- maumivu ya kichwa
- kutokwa jasho jingi na
- homa kali
Unahitaji pia Kumwona Mwanasaikolojia
Mtu kuwa na uraibu wa kula udongo siyo lazima iwe ni tatizo la kisaikolojia, lakini bado kuna umuhimu pia wa kumwona mtaalamu wa saikolojia endapo muda wako utakuruhusu.
Tumia Vidonge Asili vya Spirulina Kutibu Tatizo
Dawa imetengenezwa kupitia mimea ya spirulina na kuwekwa kwenye mfumo wa vidonge. Vina kiwango kikubwa cha madini chuma, protini na vitamini za kutosha kuupa mwili kiwango kikubwa cha virutubisho vinavyohitajika. Spirulina inatumika kwa mwezi mmoja, kila siku unameza vidonge viwili.
Baada ya kutumia spirulina tegemea haya
- Ndani ya wiki mbili utaacha kula udongo
- Mwili utarudia afya yake nzuri na kuimarika
- Hamu ya kula chakula itarejea