Mafuta ya mdalasini hupatikana kutoka kwenye magome ya mti wa mdalasini. Mimea hii ikipatikana zaidi India, Srilanka na Tanzania pia.
Matumizi ya Mafuta ya Mdalasini
Mafuta ya mdalasini yana harufu nzuri huku yakiwa na utamu wa asali, yanatumika zaidi viwandani kuongeza ladha kwenye dawa za meno. Kwa matumizi ya nyumbani tafiti zinasema kwamba mafuta haya yanasaidia
- Kupunguza mafuta mabaya kwenye mwili (bad cholesterol)
- Kutibu vidonda na majeraha
- Kurekebisha sukari kwenye damu
- Kuleta nafuu kwa mafua makali
- Kutokana la ladha yake tamu na harufu nzuri, mafuta ya mdalasini yanatumika kwenye nyama na vyakua vingine kuongeza ladha.
Faida za Kutumia Mafuta ya Mdalasini
Mafuta ya mdalasini yamekuwa yakitumika kwenye tiba kwa muda mrefu na tafiti zinasema kwamba mafuta yana saidia
- Kupambana na virusi wa herpes wanaosababisha vigwaru na masundosundo na pia virusi vya HIV
- Kupambana na saratani ya damu na
- Kutibu fangasi ikiwemo fangasi ukeni
Namna ya Kutumia mafuta ya Mdalasini
Kwa ajili ya kuleta nafuu kwa mvurugiko wa tumbo, weka kijiko kimoja cha mafuta ya mdalasini kwenye kikombe cha maji ya moto au chai , koroga kunywa mara mbili kwa siku.
Kwa changamoto zingine za kiafya tumia mafuta haya kwa uangalifu kama ulivyoelelekewa na mtaalamu wa tiba asili anayekuhudumia.
Je ni Salama kutumia mafuta ya Mdalasini kwa kila mtu?
Kama ilivyo kwa mafuta tiba mengine, mafuta ya mdalasini yanatakiwa kutumika kwa uangalifu sana. Yakitumika kwa wingi kupita kiasi yanageuka kuwa sumu. Baadhi ya madhara ambayo waweza kupata ni pamoja na mwili kusisimka kupita kiasi, mapigo ya moyo kubadilika na maumivu ya kichwa.
Wajawazito na wanaonyonyesha wanatakiwa kuepuka kutumia mafuta ya mdalasini na mafuta tiba mengine yeyote ili kuepuka matokeo mabaya.