Ni hali ya kawaida kutokuwa sawa nyakati za hedhi, mfano kupata muwasho, maumivu ya tumbo, mashavu ya uke kuuma na kuvuta nk. Mashavu ni eneo la juu kabisa la uke. Limejengwa kwa kuta ambazo kitaalamu tunaziita laboa majora na labia minora.
Kwenye makala hii tutajifunza kwanini mashavu ya uke yanavuta na kuuma wakati wa hedhi, na muda gani umwone daktari kulingana na tatizo lako.
Kwanini mashavu ya uke yanauma kwenye hedhi?
Hapa chini ni changamoto zinazopelekea upate hali ya kuvuta na maumivu kwenye uke wakati wa hedhi.
1.Vulvodynia
Haya ni maumivu sugu ya mashavu ya uke ambayo huchukua mpaka miezi mi3 kuisha. Pamoja na kwamba hakuna chanzo cha moja kwa moja cha tatizo, mambo haya yanaweza kuchangia tatizo
- kama umeugua maambukizi ya ukeni hivi karibuni
- aleji ya ngozi
- majeraha kwenye mishipa ya fahamu kwenye uke
- mabadiliko ya homoni
- kulegea misuli ya uke
2.Fungus Ukeni
Karibu asilimia 75 ya wanawake lazima wanaugua fangas ukeni katika kipindi flani kwenye maisha yao. Hii ni kutokana na kukua kupita kiasi kwa vimelea wa fungus ya yeast. Baadhi ya vyanzo cha tatizo ni
- mabadiliko ya homoni kutokana na uzazi wa mpango
- matumizi makubwa ya antiboitics
- kuosha uke mpaka ndani-douching
- kuvaa nguo za kubana ambazo siyo za pamba
- kuugua kisukari mda mrefu
Dalili za fungus ukeni ni pamoja na maumivu wakati wa kukojoa, kutokwa na uchafu mweupe mzito na mtindi, maumivu kwenye tendo na muwasho.
3.Maambukizi ya Bakteria Ukeni
Maambukizi ya bakteria yani bacterial vaginosis, yanatokea pale tindikali ya kwenye uke inapopungua sana. Hii inatokea ikiwa unafanya ngono na wapenzi tofauti mara kwa mara ama unaosha sana uke mpaka ndani.
Ukiwa na maambukizi haya utapata hali ya kuungua unapokojoa na uchafu mweupe unaonuka.
4.Folliculitis
Folliculitis ni pale kipele chekundu kinapoota eneo la unywele. Hii inaleta maumivu na kuvuta wakati wa hedhi. Kipele hichi chaweza kujitokeza baada ya kunyoa mavuzi, ama kama eneo husika la unywele limeshambuliwa na bakteria.
5.Bartholin Gland Cyst
Hizi ni tezi zilizopo ndani ya uke, kazi yake ni kutoa majimaji yanayolainisha uke wakati wa tendo. Na pia majimaji haya yanaua vijidudu vya magonjwa. Inapotokea tezi zimeshambukiwa ama zimeziba, zinaweza kuvimba na kuleta maumivu makali kwenye uke.
6.Vaginismus
Hii ni hali maumivu ya kuvuta kwenye uke yasiyo ya kawaida. Ni kwamba misuli ya uke inajikaza ili kutoruhusu kitu cha nje kuingia ndani hata uume. Unaweza kuandaliwa vizuri na uke ukalowa lakini uume usipenye kabisa kwenye uke kutokana na uke kugoma kutanuka.
Baadhi ya vitu vinavyochangia tatizo ni msongo wa mawazo na historia ya kufanyiwa ukatili wa kingono mfano kubakwa au kukeketwa.
Nini cha kufanya ukiwa nyumbani kwa hili tatizo la Uke kuuma na kuvuta?
Ikiwa unapata maumivu ya mashavu ya uke kwenye hedhi, karibu kubadili pedi au tampon kisha uone kama utapata nafuu. Pia badili aina ya pedi ucheki kama utapata nafuu. Mambo mengine ya kufanya ni pamoja na
- kuhakikisha chupi yako haikubani na ni ya pamba
- tumia kitu cha baridi sana au cha moto kwenye eneo la uke kupunguza maumivu na muwasho
- epuka kazi zinazobana uke wako kama za kuendesha baiskeli hasa ukiwa period
- usioshe uke mpaka ndani wala kitumia deodorantas kwenye uke
- usitumie shampoo na sabuni ukeni
- osha uke wako na maji pekee
Lini unatakiwa kumwona daktari?
Ni muhimu sana kumuona aktari ikiwa maumivu ya mashavu ya uke ni makali sana, hasa kama inaambatana na dalili zingine. Daktari atakusikiliza historia yako na dalili unazopata, kisha atakupa tiba sahihi kulingana na chanzo cha tatizo.
Soma makala zinazofuata kuhusu