Mkojo Mchafu

mkojo mchafu
mkojo mchafu

Tunaposema mkojo mchafu ni pale unapooona mkojo wako una rangi isiyo ya kawaida na vile ulivozoea. Mkojo ukiwa na rangi ya mawingu badala ya rangi ya njano mpauko, hapo kuna tatizo.

Kama mkojo wako ni mchafu maaana yake kuna kitu hakipo sawa kwenye mfumo wako wa mkojo. Na tuposema mfumo wa mkojo nia kuanzia hapo kwenye kikojoleo kwenda kwenye kibofu cha mkojo kwenda mpaka kwenye figo. Japo siyo kila mara ukiwa na mkojo mchafu ni ugonjwa la hasha.

Mkojo Mchafu ni Kiashiria Cha Ugonjwa

Mkojo mchafu unaweza kuashiria uwepo wa tatizo kubwa kiafya linalohitaji tiba ya haraka. Vile unavojifunza kwa haraka na kujua chanzo cha tatizo, ndivyo itakapokupa uharaka wa kufanya maamuzi ya kuanza tiba mapema.

Chanzo cha mkojo mchafu

1.Kuishiwa maji mwilini

Mkojo mchafu husababishwa kwa kiasi kikubwa na kupungukiwa maji. Inatokea sana kwa watoto na watu wazima, pamoja na watu wenye magoonjwa sugu. Watu wazima wengi hupungukiwa maji nyakati za asubhi wanapoamka na wanapotoka mazoezi.

Pale mwili unapopungukiwa maji unafanya kujizuia kupoteza maji zaidi. Kwahivo mkojo wako unakuwa mzito na njano zaidi kuliko kawaida. Dalili zingine kwamba umepungukiwa maji ni pamoja na

  • kutoa mkojo wa mawingu
  • kiu kupita kiasi
  • kukojoa mara chache
  • kwa watoto, pampas kuwa kavu mda mwingi
  • mdomo mkavu
  • kuumwa kichwa na
  • kuhisi kizunguzungu

Kama ni asbhi na unahisi umepungukiwa maji, maana yake tiba yako rahisi na ya haraka ni kunywa maji. Kama mtoto wako anatapika na kuharisha, mpeleke hospital mweleze daktari mtoto atibiwe.

Na kama ikitokea unakunywa maji na tatizo haliishi, maana yake kuna tatizo nyuma ya pazia linalotakiwa kutibiwa hospital haraka.

2.UTI

Mambukizi kwenye njia ya mkojo yani UTI ni chanzo kikubwa pia cha kupata mkojo mchafu. Wanawake wanaugua zaidi UTI ukilinganisha na wanaume, kwasababu ya anjia fupi ya mkojo. Njia inapokuwa fupi ni rahisi kwa vimelea kuthiri.

Unapoumwa UTI mwili unatuma kinga kupambana na bakteria wabaya, matokeo ya huo mpambano zi seli zilizokufa zikichanganyika na mkojo na kupelekea mkojo mchafu.

Dalili zingine za UTI ukiacha hii ya mkojo mchafu ni pamoja na

  • kuhisi moto wakati wa kukojoa
  • kupata haja ndogo mara kwa mara
  • kuongezeka kwa hamu ya kwenda kukojoa
  • kushindwa kutoa mkojo mwingi kwa pamoja
  • damu kwenye mkojo
  • kuhisi mgandamizo uzito eneo la nyonga
  • kutoa mkojo wenye harufu kali
  • kuumia eneo la mkundu wa wanaume
  • maumivu kwenye nyonga kwa wote wanaume na wanawake
  • maumivu kwenye tumbo la chini

Anza Tiba ya UTI Mapema

Kumbuka maambukizi mengi ya bakteria yanatibika tu kwa antibiotic. Ni mara chache sana UTI ikashambulia eneo la juu la figo. Hii ikitokea utahitaji kupigwa sindano za antibiotics.

Usipuuze dalili mbaya hata sku moja. Nenda hospital endapo utaanza kupata dalili hizi

  • homa kali
  • mwili kutetemeka
  • kichefuchefu na kutapika
  • maumivu makali chini ya kitovu na pande za kulia na kushoto

3.Vaginitis

Hili ni tatizo linalowapata wanawake na linapelekea mkojo mchafu. Vaginitis ni maambukizi kwenye njia ya uke, maambukizi haya yanaweza kuwa ya

  • bakteria
  • fungus au
  • trichomoniasis

Kumbuka ili uke uwe na afya njema, lazima kuwe na uwiano mzuri wa viumbe wadogo ukeni. Pale tu inapotokea viumbe baadhi aidha fungus au bakteria wakakua kupita kiasi, mazingira ya uke yanavurugika na unaanza kutokwa na uchafu usio wa kawaida.

Dalili za uke kushambuliwa ni pamoja na

  • muwasho, maumivu na hali ya kuungua ukeni
  • kutokwa uchafu mwingi usio wa kawaida
  • harufu mbaya ya shombo la samaki
  • maumivu wakati wa kukojoa
  • kutokwa uchafu wa njano, kijana au mweupe mzito kama mtindi

Matibabu ya maambukizi kwenye uke itategemea na chanzo cha tatizo. Kazi ya daktari ni kushirrikiana na wewe kugundua chanzo cha tatizo lako na kukupa tiba sahihi. Hakikisha unajieleza dalili zote unazopata ukienda kwa daktari.

4.Mawe kwenye figo

Mawe kwenye figo ni mkusanyiko wa madini na chunvi kwenye njia ya mkojo. Siyo lazima mawe haya yakae kwenye figo, yanaweza kushuka mpaka kwenye kibofu. Mawe ya figo yanaweza kukukua na kuleta maumivu makali sana.

Pia mawe ya figo yanaweza kuziba njia ya mkojo na kusababisha maambukizi. Kwahivo kupata mkojo mchafu sometime yaweza kuashiria tatizo la mawe ya figo

Dalili zingine kwamba una mawe kwenye figo ni pamoja na

  • kupata haja ndogo mara kwa mara
  • maumivu makali chini ya mbavu
  • maumivu makali unapokojoa
  • kuumia eneo la tumbo kushoto au kulia na kwenye kibofu
  • kukojoa damu
  • kutapika na kichefuchefu
  • homa kali na
  • kupata mkojo wenye harufu kali

Ushauri muhimu kwa mgonjwa wa mawe ya figo

Kwa wagonjwa wengi shida ya mawe kwenye figo huisha yenyewe bila hata dawa. Wagonjwa wachache hitaji dawa za kupunguza maumivu na kuyeyusha mawe ili yatolewe kwa njia ya mkojo. Unashauriwa kunyw amaji ya kutosha kila siku ili kuchochea utoaji wa mawe haya.

5.Magonjwa ya zinaa

Ukiambiwa magonjwa ya zinaa maana yake ni yale yanayoambukiwa kwa njia ya tendo. Magonjwa mengi ya zinaa ambayo yanawapata sana watu kama kaswende na kisonono yana dalili chache. Kama ilivo kwa UTI, unapougua magonjwa ya zinaa mwili unatuma askari kupambana. Matokeo ya mpambano ni uchafu utakaoambatana na mkojo.

Dalili zingine za magonjwa ya zinaa ni pamoja na

Kama unahisi ulikutana kimapenzi na mtu usiyemwelewa , na umeanza kupata mkojo mchafu, nenda hospitali upime magonjwa ya zinaa. Magonjwa mengi yanatibika vizuri hospital.

6.Kisukari kinaweza kupelekea mkojo mchafu

Watu wanaougua kisukari wana kiwango kikubwa na sukari kwenye damu. Figo zao inabidi zifanye kazi kubwa sana ya kuchuja sukari, na sukari hii mara nyingi inatolewa kwenye mkojo.

Kisukari chaweza kudhoofisha figo na kupelekea magonjwa ya figo, endapo utasumbuliwa kwa mda mrefu. Wagonjwa wa kisukari wanapata mkojo mchafu mara kwa mara.

Sasa ili kujua kama umeanza kuugua kisukari, tazama dalili hizi pia

  • kiu kikali
  • kukojoa mara kwa mara
  • kupata maambukizi mara kwa mara
  • kuchelewa kupona kidonda
  • kupungua uzito kwa kasi na
  • mwili kuchoka sana

Fahamu kwamba kuna aina mbili za kisukari. Kisukari cha ukubwani Type 2 na kisukari cha utotoni ama cha kurithi-type 1. Kisukari cha ukubwa chaweza kutibika kama mgonjwa akifatilia ushauri wa lishe vizuri na kutumia dawa. Kisukari cha kurithi hakitibiki, kinahitaji mgonjwa apate sindano za insulini kila siku.

7.Tezi dume

Maambukizi ya bakteria kwenye tezi dume yanaweza kupekelea tezi kuvimba kupita kiasi(prostatitis). Tezi ikiathiriwa na vimelea , kama kawaida mwili unatuma seli nyeupe kwenda kupambana. Sasa matokeo ya mpambano huu ni uchafu utakaochanganyika na mkojo na hivo kufanya mkojo mchafu.

Dalili zingine za shida kwenye tezi dume ni pamoja na

  • kushindwa kukojoa vizuri
  • maumivu wakati wa kukojoa
  • maumivu ya tumbo la chini, mkundu na chini ya mgongo
  • homa
  • mkojo wenye harufu kali
  • maumivu wakati wa kukojoa
  • uume kutosimama na kushindwa kabisa kufanya tendo na
  • kukosa hamu ya tendo

Kumbuka kufanya vipimo mara moja kwa mwaka endapo ni mwanaume zaidi ya miaka 40. Tezi dume inapona mapema endapo itawahi kugundulika.

8.Mimba na mkojo mchafu

Kipindi cha mimba, mjamzito anaweza kupata mkojo mchafu kutokana na UTI, magonjwa ya zinaa na hata fungus. Dalili ni zilezile za wasio wajawazito. Endapo hutatibiwa mapema magonjwa yanaweza kuhatarisha mimba yako.

Endapo mkojo wako una protini, na wewe ni mjamzito, hichi kinaweza kuwa kiashiria cha presha ya kupanda kwa mjamzito. Presha hii isipodhibitiwa yaweza kupelekea kifafa cha mimba.

Nenda hospitali mapema endapo una mimba na unahisi dalili za mkjo mchafu zisozo za kawaida, ama unahisi kuna maambukizi ukeni.

Bofya kusoma makala inayofuata kuhusu: kumkojoza mwanamke