Kujifukiza Ukeni(Vaginal steaming)

namna ya kujifukiza ukeni
kujifukiza ukeni

Uke unapitia vipindi vigumu sana, kuanzia kwenye tendo la ndoa, hedhi mpaka kwenye kuzaa, kweli uke unavumilia mambo mengi. Pamoja na haya kuna mengine kama mabadiliko ya homoni na changamoto za misuli ya nyonga inayozunguka uke. Tutajifunza kwa kina namna ya kujifukiza ukeni kwenye makala hii.

Kujifukiza ukeni ni njia ya asili inayotumiwa na wanawake tangu enzi hizo za kale. Matumizi yake ni kama tiba asili kuleta nafuu kwa changamoto mbalimbali za uzazi kama kurekebisha hedhi, kusafisha uke na kupunguza maumivu ya tumbo na kiuno kipindi cha hedhi.

Swali ni je njia hii ni salama na imethibitishwa kisayansi? Tusome zaidi namna inavyofanya kazi hapa chini.

Jinsi ya Kujifukiza ukeni

Kujifukiza ukeni ni kitendo cha kuchemsha kwa pamoja mkusanyiko wa mimea tiba kwenye sufuria au chungu chako, kisha unaruhusu ule mvuke wa dawa kupenya kwenye uke. Unafanya huku ukiwa umetanua miguu karibu na sufuria lako au kuchuchumaa chini ya sufuria au beseni yenye mvuke wa dawa.

Mimea inayotumika zaidi kwenye mchanganyiko huu wa kujifukiza ni pamoja na

  • Mugwort
  • wormwood
  • chamomole
  • calendula
  • basil na
  • oregano

Kabla hujaanza kujifukiza dawa hii ukeni, muhimu kufahamu tahadhari na hatua unazotakiwa kuzingatia ili fanikishe zoezi hili pasipo kuumia au kupata madhara.

Fuata hatua hizi kujifukiza ukeni

  1. Chemsha maji kisha yaweze kwenye beseni la kuogea.
  2. Chemsha dawa yako pembeni kisha changanya kikombe kikubwa kimoja cha dawa kwenye beseni na usubiri kwa dakika moja.
  3. Vua nguo zako zote kuanzia kiunoni.
  4. Simama ukiwa umepanua miguu na beseni liwe katikati, au chuchumaa kama unajisaidia kwenye beseni la mvuke.
  5. Kama una choo cha kukaa weka kopo la dawa ndani ya choo kisha ukae kwa dakika 20 mpaka 30. Hakikisha unaziba maeneo mengine ya  pembeni ili mvuke usipotee.

Zipi ni Faida za kujifukiza Ukeni?

Kujifukiza ukeni ni tiba ya asili ya kusafisha uke, kizazi na via vya uzazi kwa ujumla. inasadikika kwamba tiba hii inasaidia pia kwa changamoto za

  • msongo wa mawazo
  • bawasili
  • sonona
  • maambukizi
  • ugumba
  • kuvurugika kwa homoni
  • changamoto za hedhi
  • maumivu ya kichwa
  • changamoto za tumbo la chakula
  • maumivu ya viungo na
  • uchovu

Je ni kuna utafiti wa kisayansi kwamba kufukiza uke inafanya kazi?

Hakuna utafiti wa kisayansi kuhusu tiba hii ya kujifukiza ukeni. Hakuna utafiti kuonesha ni kwa namna gani mvuke huu unaweza kupenya mpaka ndani ya kizazi na kuleta tiba. Tiba hii kwa kiasi kikubwa ni kutokana na mila na desturi za jamii husika na siyo swala la kisayansi.

Je ni Salama kujifukiza uke?

Hakuna utafiti wa kisayansi kuonesha kwamba kufukiza ukeni ni salama. Uke wako unaweza kujisafisha wenyewe, na umeumbwa kwa tishu laini kiasi ya kutohitsji mvuke wa mtoto kusafishwa.

Mvuke unaweza kuongeza joto la ukeni na kufanya bakteria wabaya na fangasi kushambulia uke.

Ngozi ya uke ni laini na nyepesi sana. Kupitisha mvuke au kitu cha moto sana kunaweza kuleta majeraha na makovu kwenye uke.

Hakuna utaratibu wowote rasmi ulioidhinishwa kisayansi wa kuelekeza namna ya kujifukiza ukeni. Kwa maana hiyo unatakiwa kumwona mtaalamu wa tiba asili, ama wewe mwenyewe kwa kutumia ujuzi wako kufanya kitendo hiki.

Ni kweli kwamba kuna tiba asili nyingi sana zinafanya kazi na kuleta matokeo mazuri, ila wa tiba hii ya kujifukiza uke, hakuna uhakika kama inaleta matokeo. Hakuna uhakika kama kujisafisha ukeni hakuleti madhara kwa mjamzito maana baadhi ya tiba asili husababisha mimba kuharibika.

Hitimisho

Uke wako ni kiwanda kinachoweza kusjisafisha chenyewe bila msaada kwa kujisafisha. Yawezekana kujisafisha kukasaidia kupunguza maumivu lakini hakuna utafti wa kisayansi kusapoti hilo.

Kujifukiza kunaweza kusababisha uke kushambuliwa na bakteria na fangasi kisahisi. Na siyo kwmaba hakuna tiba asili zinazofanya kazi hapa, ila tu haku autafiti kwenye uwezo wa tiba hii ya kujifukiza.

Kuna njia zingine salama zaidi za kutumia joto kupunguza maumivu ya tumbo la hedhi. Jaribu kunywa kikombe cha green tea au jikande kwa taulo eneo la tumbo.

Kabla hujafikiria kuanza kujifukiza ukeni, zungumza na daktari wako, atakusaidia kukupa njia zingine salama na zilizohakikiwa kisayansi katika kutibu changamoto yako.

Bofya kusoma makala inayofuata kuhusu: Chanzo cha uchafu mweupe ukeni