Ukavu wa Macho, Dalili, Vipimo na Tiba

ukavu wa macho
macho

Ukavu wa macho ukoje?

Hata ukiwa na furaha, fahamu tu kwamba macho yako yamejaa machozi. Macho haya yanalainisha macho na kukufanya uone vizuri. Macho yameundwa kwa maji, mafuta, uteute pamoja na kinga ya kupambana na vimelea. Ukavu wa macho utafanya macho yako yawe kwenye hatari ya kushambuliwa na vimelea na pia macho kuvimba. Japo ukavu wa macho utakufanya usione vizuri nyakati fulani, haliwezi kupelekea upofu .

Dalili za ukavu wa macho

  • macho kuuma
  • kuwasha na
  • kuwa na wekundu
  • macho kuchoka haraka kuliko kawaida
  • ugumu wa kusoma hasa maandishi ya computer na simu
  • kuhisi kama kuna mchanga kwenye macho na
  • kuhizi macho mazito kuliko kawaida

Nini kinasababisha ukavu kwenye macho

Machozi kama tulivoona hapo mwanzo yameundwa kwa mafuta, majimaji na uteute. Kama tezi zinazozalisha machozi zikivimba ama zikashindwa kuzalisha kitu kimojawapo kati ya majimaji, uteute na mafuta itapelekea ukavu wa macho.

Pale mafuta yanapokosekana kwenye macho yako,inapelekea machozi kuyeyuka haraka na hivo macho kukosa unyevunyevu unaotakiwa. Baadhi ya sababu zinazopelekea machozi kutozalishwa vizuri ni pamoja na

  • mgonjwa kuwa kwenye tiba ya homoni
  • mazingira ya upepo na joto kali
  • aleji
  • upasuaji kwenye macho
  • baadhi ya dawa mfano dawa za aleji, uzazi wa mpango na dawa za kupunguza msongo wa mawazo.
  • kuvaa miwani ya lens kwa muda mrefu
  • matumizi makubwa ya computer
  • kutofumba macho kila mara vya kutosha

Mazingira hatarishi yanayopelekea ukavu wa macho

Tatizo la ukavu wa macho linawatokea zaidi watu wa umri zaidi ya miaka 50. Wengi wao wakiwa ni wanawake, japo tatizo linawapata pia na wanaume.

Wanawake wajawazito , wanaotumia dawa za kurekebsha homoni ama wanaokaribia kukoma hedhi wapo kwenye hatari zaidi. Hapa chini ni sababu mbalimbai zinazoongeza hatari ya kuugua ukavu macho

  • aleji ya muda mrefu
  • matatizo ya homoni ya thyroid
  • magonjwa ya autoimmune kama rheumatid arthritis
  • watu wanaolala bila kufumba macho vizuri na
  • upungufu wa vitamin A

Tiba ya hospitali kwa ukavu wa macho

Kuna namna nyingi daktari anaweza kupendekeza utibwe. Tiba hizi zinajumuisha

Matone kulainisha macho: Hii ni tiba kubwa sana inayotumika zaidi. Dawa nyingi za matone zinapatikana kwenye famasi ya karibu yako, japo siyo kila aina ya dawa inafanya kazi kwa kila mtu. Kama una tatizo sugu la kukauka kwa macho, utahitaji kutumia matone ya kulainisha macho hata kama unajisia vizuri. Kama macho yako yanakauka hata ukiwa umelala unahitaji kutumia dawa yenye matone mazito mfano wa jelly.

Upasuaji mdogo kuruhusu uzalishaji wa kutosha wa machozi

Cream ya kuongeza homoni ya testosterone: Ukavu wa macho waweza kuashiria upungufu wa testosterone kwenye tezi za kuzalisha mafuta za macho.

Lini unatakiwa kumwona daktari?

Kama unahisi macho yako ni makavu na unashindwa kutazama vizuri, unahitaji kumwona daktari bingwa wa macho. Tatizo la ukavu wa macho linaweza kutibika vizuri endapo utaliwahi. Lisipotibiwa mapema inakuwa ngumu kuisha kabisa.

One reply on “Ukavu wa Macho, Dalili, Vipimo na Tiba”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *