Vidonda ukeni na kwenye mashavu ya uke

Mashavu ya uke au vulvar ni eneo la nje la sehemu ya uke. Vidonda ukeni ni malengelenge yanayojitokeza eneo la nje la uke, vidonda hivi vinaweza kuambatana na maumivu makali sana.

Kwa kiasi kikubwa vidonda hivi husababishwa na magonjwa ya zinaa. Tiba yake inapatikana vizuri hospitali. Endelea kusoma zaidi makala yetu kujua vyanzo vingine vinavyopelekea vidonda kwenye mashabu ya uke, dalili pamoja na tiba.

Dalili za vidonda kwenye mashavu ya uke

Vidonda kwenye uke huanza kama kipele au chunusi na kukua taratibu mpaka kupasuka. Dalili za vidonda kwenye mashavu ya uke zinajumuisha

  • maumivu
  • muwasho kwenye ngozi
  • kutokwa na majimaji au damu
  • maumivu wakati wa kukojoa
  • kuvimba mtoki na
  • kupatwa na homa

Aina za vidonda ukeni

Kiujumla vidonda kwenye mashavu ya uke hugawanywa kwa namna mbili. Vidonda kutokana na zinaa au ngono na vidonda visivytokana na ngono. Vidonda vinavyotokea baada ya tendo la ngono inawapata watu wengi zaidi.

Chanzo cha vidonda ukeni

Kuna vitu vingi ikiwemo magonjwa kadhaa yanayoweza kupelekea vidonda ukeni kama

1.Magonjwa ya zinaa

Chanzo kikubwa cha vidonda kwenye uke ni magonjwa ya zinaa. Magonjwa haya huambukizwa kwa njia ya kufanya tendo la ngono. Ukimwi, kisonono, kaswende na chylamydia ni magonjwa baadhi yana zinaa yanayoongoza kwa kuathiri watu wengi zaidi.

2.Maambukizi ya fangasi ukeni

Fangasi kwenye mashavu ya uke na ndani ya uke ni chanzo cha vidonda ukeni. Fangasi aina ya candida wanachangia kwa kiasi kikubwa kumomonyoa mashavu ya uke. Dalili zingine za fangasi ukeni ni pamoja na

  • muwasho
  • hali ya kuunguza ukeni hasa wakati wa kukojoa na sex na
  • kutokwa na uchafu mwingi mweupe mzito uekni

3.Maambukizi ya bakteria

Baadhi ya mambukizi ya bakteria kama streptococcus wanaweza kusababisha vidonda kwenye mashavu ya uke. Maambukizi haya hutibiwa na antibiotics na kupona kabisa.

4.Kutumka kwa ngozi ya uke

Kujikuna sana kwenye ngozi ya mashavu ya uke, kunaweza kupelekea kututumka kwa ngozi na hatimaye kuvimba mpaka kuleta vidonda.

5.Matokeo ya dawa

Baadhi ya dawa mfano baadhi ya antibiotics zinaweza kuleta vidonda ukeni.

6.Saratani

Japo ina tokea kwa wanawake wachache sana, saratani ya mashavu ya uke inaweza kusababisha vidonda kwenye mashavu ya uke. Saratani hii inawapata zaidi wanawake wazee.

7.ALeji ni chanzo cha vidonda vya uke

Aleji ya ngozi kutokana na vitu mbalimbali mfano mafuta au vifaa vya usafi kama pedi inaweza kuleta muwasho na hatimaye vidonda ukeni.

Vipimo kugundua vidonda ukeni

Daktari atafanya uchunguzi wa macho ili kujiridisha kama kuna mabadiliko kwenye uke wako. Daktari atakuuliza kuhusu mara ya mwisho kufanya tendo la ndoa, idadi ya wapenzi ulionao, na dawa unazotumia kwa hivi karibuni.

Pia daktari anaweza kupendekeza vipimo hivi maabara

  • kipimo cha damu
  • vaginal swab test na
  • kipimo cha mkojo

Endapo daktari atahisi uwepo wa saratani, atachukua sampuli kidogo ya nyama kwenye uke na kuipeleka maabara ili kujiridhisha.

Tiba ya vidonda vya uke

Tiba yako kwa kiasi kikubwa itategemea na chanzo cha tatizo lako. Baadhi ya vidonda kwenye mashavu ya uke vinaweza kuisha vyenywe bila tiba. Lakini vingine vitahitaji tiba sahihi hospitali.

Magonjwa ya zinaa mara nyingi hutibiwa kwa antibiotics na antiviral, kwa kupewa vidonge ama sindano.

Mtoa huduma atakwelekeza vizuri namna ya kusafisha kidonda chako mpaka pale utakapopona kabisa.

Wakati mwingine tiba ya nyumbani inaweza kusaidia kupunguza maumivu kwenye mashavu ya uke. Tiba hizi ni pamoja na

  • kipande cha barafu kwenye kitambaa na kuweka kwenye uke
  • kukaa kwenye beseni la maji lililochanganywa na chunvi kiasi.

Endapo tatizo lisipotibiwa mapema linaweza kuleta athari zaidi. Mgonjwa ana weza kupata mawazo, kushindwa kufurahia tendo la ndoa, maambukizi na makovu kwenye uke. Pia kama mgonjwa ana magonjwa ya zinaa anaweza kumwambukiza mtu mwingine kirahisi.

Tiba kupitia vidonge asili vya UCP-Uterus cleansing pills

Kwa mwanamke mwenye changamoto ya vidonda ukeni kutokana na maambukizi ya bakteria au fangasi, tunashauri atumie uterus cleansing pill kusafisha uke. Uterus cleansing pill (UCP) ni vidonge 2 vilivyotengenezwa kitaalamu kwa kuzingatia uasili wa dawa.

Dawa inatibu changamoto za wanawake kama vidonda, kurejesha mazingira mazuri ya uke na kulinda uke usipate michubuko mara kwa mara, kutibu muwasho, fangasi ukeni, kutokwa uchafu na harufu mbaya ukeni.

Dozi moja yenye vidonge viwili vinatumika kwa wiki moja, na yatakiwa utumie dozi mbili. Kidonge kimoja kinawekwa ukeni na kutolewa baada ya siku 3, kisha unapumzika masaa 24 unaweka tena kidonge kingine.

Gharama ni Tsh 50,000/= .

Angalizo pale unapotumia Uterus Cleansing Pill

Kuna wimbi kubwa la wajasiliamali mitandaoni wanauza vidonge vyenye mfanano na hivi vya UCP, tena wanauza kwa bei rahisi sana. Watu hao siyo madaktari wala siyo wataalamu wa afya na wanauza bidhaa feki ambazo ni hatari wa afya yako. Wengi wao hawana hata ofisi, ukipata madhara unakosa pa kuuliza. Kuwa makini na watu hao, wamejaa sana insta na fb

Dawa haitumiki kwa wanawake bikira na wajawazito. Usifanye tendo la ndoa wakati huo upo kwenye dozi, ukianza hedhi pumzika kutumia vidonge hivi mpaka pale utakapomaliza hedhi.

Tunapatikana Magomeni Dar, Tuandikie kwa whatsapp no-0678626254 kuanza tiba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *