Chanzo Cha Ukavu Ukeni

ukavu ukeni
mfano wa uke

Nini kinasababisha ukavu ukeni?

Uke umeumbwa kwa mashavu yenye kuta zenye tishu laini sana. Na kufunikwa na majimaji yenye utelezi ili kusaidia mbegu za kiume kuogelea vizuri na kurutubisha yai wakati wa tendo la ndoa.

Uteute huu pia ni kilainishi cha uke kupunguza msuguano wakati wa tendo la ndoa.

Uzee na mashavu ya uke kusinyaa

Kadiri mwanamke anavozeeka mabadiliko ya uzalishaji wa vichocheo ama homoni vinapelekea kuta za uke kusinyaa na kuwa dhaifu. Kuta zikisinyaa maana yake seli zinazozalisha uteute zinapungua na hivo kupelekea ukavu ukeni.

Mabadiliko ya homoni ndio sababu kubwa inayokufanya uwe na uke mkavu.

Nini Madhara ya Ukavu Ukeni?

Kukauka kwa uke wako kunaweza kusababisha madhara kama

Nini Kinapelekea Ukavu ukeni?

Kupungua kwa homoni ya estrogen ndipo chanzo kikubwa cha ukavu ukeni. Wanawake wote hupungua uzalishaji wa estrogen kadiri wanavozeeka na kukaribia kukoma hedhi yaani menopause.

Menopause siyo chanzo pekee kwani kuna vitu vingine vinavyopelekea uwe na uke mkavu. Mambo mengine yanayopunguza uzalishaji wa estrogen ni pamoja na

  • kunyonyesha
  • kuvuta sigara
  • kuzaa
  • upasuaji kuondoa mifuko ya mayai(ovary)
  • stress kupita kiasi
  • maozezi makali sana
  • sonona
  • magonjwa ya kinga na
  • baadhi ya tiba kama chemotherapy na radiotherapy

Lini Unatakiwa Kumwona Daktari?

Ni mara chache sana ukavu wa uke iwe ni kiashiria cha tatizo kubwa la kiafya. Muhimu ni kutafuta ufumbuzi wa daktari endapo tatizo lako limechukua muda mrefu . Endapo usipotibia mapema ukavu wa uke unaweza kusababisha kumeguka kwa kuta za uke.

Matibabu ya Tatizo la Ukavu Ukeni

Kuna aina nyingi za tiba ambazo waweza kuzipata famasi ya karibu yako ili kulainisha uke. Tiba hizi zinakuwa kwenye mfumo wa jelly mfano KY jelly ni maarufu sana.

Hakikisha unatumia vilainishi vya maji siyo vya mafuta. Vilainihsi hivi visiwe na manukato wala kemikali hatarishi.

Kamwe usitumie mate kama kilainishi wakati wa tendo la ndoa kwani unaweza kupata maambukizi ya bakteria. Usitumie mafuta ya kujipaka kama kilainishi kwani utaharibu kuta za uke.

Nawezaje Kuzuia tatizo hili kujitokeza mara kwa mara

  • kunywa maji ya kutosha kila siku
  • usitumie sabuni wa marashi ukeni
  • ongea na mwenzi wako kuhusu tatizo ili akuvumilie wakati unatafuta tiba.

Je kuna madhara yoyote kutumia jelly na vilainishi vya pharmacy?

Jibu ni ndio, vilainishi hivi vya kununua pharmacy siyo vya kuzoea kutumia. Vitumike mara moja moja sana. Madhara yake ni makubwa endapo zinatumika mda mrefu. Athari hiyo ni kuvurugika mazingira ya uke na kuugua fungus na bakteria mara kwa mara.

Pia uke kuanza kunuka vibaya na kutokwa na uchafu usio kawaida. Ndiomana tunashauri kulenga kutibu chanzo cha tatizo ambalo ni kurekebisha homoni.

Tumia Vidonge Asili vya Evecare kurejesha uteute mzuri.

Evacare ni tiba asili iliyo kwenye mfumo wa vidonge. Ni dawa zinazozalishwa nchini India kutibu changamoto za wanawake kama ukevu ukeni, upungufu wa ute, hedhi kuvurugika na maumivu makali kwenye hedhi.

Dozi moja ina vidonge 30, unatumua kwa week mbili. Kulingana na ukubwa wa tatizo lako tunaweza kushauri utumie zaidi ya dozi moja. Evecare inafaa kwa wanawake chini ya miaka 35. Na soy power inawafaa zaidi wenye umri kuanzia 36 mpaka 50.

Vidonge vimetengenezwa kitaalamu kupitia muunganiko wa mimea na kuhifadhiwa vizuri ili kutunza uasili wa dawa pasipo kuwekwa kemikali. Tutakushauri vizuri kulingana na tatizo lako, endapo yafaa utumie evecare ay soypower.

angalizo

Kuna wimbi kubwa la wajasiliamali mitandaoni wanauza vidonge fake vya evecare, tena wanauza kwa bei rahisi sana. Watu hao siyo madaktari wala siyo wataalamu wa afya na wanauza bidhaa feki ambazo ni hatari wa afya yako. Wengi wao hawana hata ofisi, ukipata madhara unakosa pa kuuliza. Kuwa makini na watu hao, wamejaa sana insta na fb

Gharama ni Tsh 75,000/= kwa Evecare na
Tsh 90,000/= kwa soy power.
Tuandikie whatsapp no: 0678626254 kuanza Tiba.

Bofya kusoma kuhusu: mashavu ya uke kusinyaa

12 replies on “Chanzo Cha Ukavu Ukeni”

Samahani, kama tatizo la ukavu ukeni limetokea, je kuna uwezekano wa kushika mimba?

Me na hilo taizo na nikiwa nasex natumia mafuta au mate japo nasex kila baad ya miez kazaa kutokana mume wangu yupo mbali je naweza pata madhara

Duuu…? So bacteria wanao zalishwa kwenye mate pindi mwanamke anapo kuwa amekosa ute wanaitwaje,
Kuna wanawake wengine wanakuwa na hofu ya kufanya mapenzi ndio sababu hufanya baadhi za watu kutumia mate ili kulainisha uke na kutimiza haja yake ya ndoa

Mke wangu anatatizo la ukavu na muda mwingine hutoa uchafu mweupe wakati wa tendo la ndoa na huo uchafu hua unaharufu kali jee ni nini tatizo je linatibika?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *