
Kwanini unapata maumivu kwenye tendo baada ya kujifungua? Ukiwa na maswali mengi kuhusu tendo la ndoa baada ya kuzaa, hapa ndio mahali pako kupata maelezo ya kina.
Lini uanze kufanya tendo baada ya kujiungua?
Mwili wa mwanamke unapitia mabadiliko mengi sana baaada ya kushika mimba na kujifungua. Wawanake wengi wanakuwa na shauku sana ya kuanza tendo na kujua utofauti wake pale wakishazaa. Kwa kiasi kikubwa nesi kliniki atakushauri usifanye tendo kwa week 6 za kwanza.
Kila mwili unapona kwa spidi yake, kuna wengine watapona mapema na hisia kurudi haraka, kuna wenine watachukua miezi mingi. Muhimu ni kufatilia tu afya yako na usihaakishe kuanza tebdo la ndoa.
Sababu 5 kwanini unapata maumivu kwenye Tendo baada ya kuzaa
1.Mipasuko na michubuko
Wanaojifungua kawaida wanaweza kupata michubuko na mipasuko na wengine huhitaji kuongezewa njia ili mtoto atoke, hasa kama mtoto ni mkubwa. Endapo utaongezewa njia, yaweza kuchukua mda mrefu zaidi kupona ,hata miezi miwili.
Endapo utahisi maumivu kwenye tendo na ulionezewa njia, basi jua kwamba bado hujapona vizuri mshono wako na unatakiwa kujipa muda zaidi.
2.Ukavu ukeni unapelekea maumivu kwenye tendo
Baada ya mwanamke kijifungua kiwango cha hormone ya Oytocin huongezeka na kupunguza homoni ya estrogen(homoni ya uteute). Oytocin inasaidia kuongeza ukaribu wa mama na mtoto. Kitendo cha kupungua estrogen kinafanya uke kuwa mkavu na maumivu kwenye tendo.
Kupungua kwa estrogen pia kunaweza kufanya mwanamke kukosa hamu ya tendo. Unaweza kujaribu vilainishi salama ili kupungua maumivu na kufanya tendo muda mfupi.
3.Kutanuka Mlango wa kizazi (cervical dilation)
Kufanya tendo wakati mlango wa kizazi umetanuka yaweza kupelekea maumivu na kuongea hatari ya kupata maambukizi. Kupunguza hatari hii, jipe muda mrefu wa kupumzika baada ya kuzaa ili upone vizuri.
4.Mifupa ya nyonga inapelekea maumivu kwenye tendo baada ya kujifungua
Ujauzito hupelekea mabadiko mengine ya mwanamke ikiwa ni pamoja na nyonya kutanuka. Hali hii yaweza kufanya upate maumivu makali kwenye tendo. Kama maumivu yanaendelea kwa miezi mingi hakikisha unarudi hospitali kufanyiwa vipimo zaidi..
5.Upasuaji unachangia maumivu kwenye tendo baada ya kujifungua
Baada ya kuzaa kwa upasuaji, utabaki na mshono kwenye eneo la tumbo la chini. Mshono huu unaweza kuchukua miezi kadhaa kupona vizuri. Endapo utawahi kuanza tendo, lazima utapata maumivu makali. Hakikisha unapumizka walau miezi mi3 ndipo uanze tendo kama ulizaa kwa upasuaji.
Hatua za kufanya kupunguza maumivu kwenye tendo baada ya kujifungua
- Kuwa mbunifu hasa kwenye staili za mapenzi. Tumia staili zinaokupa raha zaidi bila kutumia nguvu kubwa.
- Fanya mazoezi ya kegel; mazoezi haya yaasaidia kuimarisha nyonga na misuli. Fanya walau kila siku kupata matokeo mazuri
- Tumia vilainishi pale inapobidi. Kwenye vilainishi tumia mafuta ya nazi yasiyo na harufu. Usitumie kabisa mafuta mgando, wala mate na mwisho kabisa
- Kuwa muwazi ongea na mpenzi wako ikiwa unapata maumivu, atakusaidia kutafuta ufumbuzi wa tatizo.