Kufanya tendo kinyume na maumbile kwa njia ya haja kubwa/kuliwa tigo ilikuwa ni utamaduni wa wazungu kwa miaka ya nyuma. Lakini kutokana na utandawazi kuongezeka na picha za ngono kuwepo mitandani kiasi kwamba mtu yeyote anaweza kuziona, waafrica pia wameanza kuiga kufanya ngono kinyume na maumbile.
Wadada wengi wa mjini hivi sasa kati ya 10 unakuta watano wanafanya michezo hii maarufu kama kuliwa tigo au kuliwa ndogo. Nimekuwa nikipata kesi nyingi za watu walioathirika na kufanya mchezo huu. Kuna madhara mengi sana ya kuliwa tigo ukiacha raha ya muda mfupi ambayo wanaipata wahusika.
Madhara ya kufanya tendo kinyume na maumbile(kuliwa tigo)
Kuongezeka hatari ya maambukizi ya bakteria
Kuta za mkundu hazina majimaji kwa ajili ya kulainisha kama ilivo kwa uke. Pia kuta zake ni nyemamba kiasi kwamba haziwezi kuhimili msuguano wakati wa tendo. Kukosekana huku kwa uteute kunaweza kusababisha michubuko na hivo kuruhusu vimelea wabaya kutoka kwenye kinyesi kupenya kwenye mishipa ya damu na kukufanya uugue.
Kupata magonjwa ya zinaa
Kama ilivo kwa maambukizi ya bakteria, ni rahisi sana kuambukizwa magonjwa ya zinaa kwa kuliwa tigo. Vimelea wanaweza kupenya kwenye ngozi ya mkundu pale inapotokea michubuko na ikiwa kinga haikutumika..
Magonjwa haya ya zinaa ni pamoja na kisonono, kaswende , trichonomiasis, ukimwi na homa ya ini. Tafiti zinasema kwamba asilimia kubwa ya watu wanaojihusisha na ngono kinyume na maumbile hupata amagonjwa ya zinaa.
Tendo kinyume na maumbile huleta bawasili
Kwa mtu ambaye tayari una bawasili, kufanya ngono kupitia mkundu inaongeza zaidi ukubwa wa tatizo kwa kukusababishia maumivu makali sana. Kwa mtu mzima anaweza kuugua bawasili baada ya kuanza kuliwa tigo kwasababu mishipa ya mkundu italegea sana na hivo kusababisha kuvimba haraka kwa mishipa ya damu.
Kuugua Fistula kupitia tendo kinyume na maumbile
Wanawake wengi wanaofanya tendo kinyume na maumbile wapo kwenye hatari zaidi ya kuugua fistula. Fistula ni tatizo la kutokwa na mkojo na kinyesi bila kujizuia.
Misuli ya mkundu hulegea sana kutokana na kuliwa tigo, hivo kupelekea ushindwe kubana haja kubwa kwa muda mrefu. Utajikuta unajinyea pasipo kujua kwasababu misuli ya haja kubwa imelegea.
Athari za kisaikolojia
Endapo mgonjwa atafanya kitendo hiki kisha baadae akaamua kuacha, anaweza kujihisi mkosaji kupita kiasi. Hali hii yaweza kumsumbua na kuleta msongo mkubwa wa mawazo, hasa kama muhusika amepata athari kubwa ikiwemo maambukizi sugu. Mgonjwa anaweza kuwa mwenye aibu sana na wasiwasi kwa kufanya kitendo kisichozoeleka.
Hitimisho
Kufanya ngono kinyume na maumbile siyo salama na siyo jambo jema kabisa hata kiimani. Kama tayari ulishaanza, basi jizuie kufanya tumia njia ya kawaida ya uke iliyoumbwa kwa ajili hiyo. Nenda hospitali mapema kama tayari umepata madhara ya kushindwa kubana choo ili upate matibabu.
23 replies on “Madhara ya tendo kinyume na maumbile”
So nice message
Karibu na endelea kusoma makala zetu kupitia ukurasa huu.
Absolutely
Thank you for thic nice education.
Karibu endelea kufatilia
Shukran
Endelea kuelimisha kweli wapo na niwengi pongezi kwako
Asante kwa kutambua mchango wetu
endelea kufatilia makala zetu
Mm nmekutana na mdada mmoja nmesha fanya nae kitendo hik zaid ya mara 10 je na weza nkapata madhara??
Ni hatari kufanya jambo hili, tafadhali acha mara moja. Athari zake ni mbaya zaidi
Hongera kwa elimu
asante na karibu tena
good edcasion
Nimependa elim yako
ujumbe mzuri
Good unawafumbua vijana
thankyou for education
Swaf kbsa maan wanawake cku iz wanatega popote yan
Endelea kuelimisha
Asante sana dakitari tunatambua mchango wenu hakika mnaifikia jamii kwa sehemu kubwa sana.
MUNGU AWABARIKI.
Asante xana doct
Sawa!