Jinsi ya Kutambua Siku za hatari Kushika Mimba

mzunguko na siku za hatari
mzunguko

Je wazifahamu siku za hatari kushika mimba? Ni siku gani unaweza kushika mimba baada ya hedhi kuisha? Mbegu za mwanaume zinaweza kuishi ndani ya kizazi kwa siku mpaka tano baada ya tendo zikiwa hai. Na mimba inaweza kufanyika endapo mbegu ipo kwenye kizazi au kwenye mirija ya uzazi wakati yai linatolewa.

Yai kupevuka

Kwa wanawake wengi yai linapevuka siku ya 14 kwenye mzunguko. Japo kufanya tendo la ndoa wakati upo period au nyakati zingine ambazo siyo siku ya 14 siyo kigezo cha kutoshika mimba kwa aslimia mia. Bado mimba inaweza kuingia katika kipindi kingine mfano ukifanya tendo kipindi cha hedhi.

Je mimba yaweza kuingia kipindi cha hedhi?

Kwa wanawake wenye mzunguko mfupi yani siku 28 mpaka 30 kuna uwezekano wa kushika mimba hata ukifanya tendo wakati wa hedhi. Kutumia kinga kama kondomu bado ni njia ya uhakika zaidi ya kukuepusha kushika mimba usiyoitarajia. Soma zaidi kujua jinsi ya kupanga siku za kukutana na mme wake ili uepuke kushika mimba

Jinsi Mimba inavyofanyika katika siku za hatari

Yai linapokomaa hutolewa kwenye mfuko wa mayai(ovary)ili kurutubishwa,kitendo hiki huitwa ovulation. Kikawaida kila mwezi yai moja hukomaa na kutolewa kwenda wenye mirija ya uzazi lipate kurutubishwa.

Yai linakuwa salama masaa 12 mpaka 36 kusubiri mbegu ije irutubishe. Kama mbegu zinaweza kuishi mpaka siku 5 kwenye kizazi maana yake unaweza ukashika mimba ukifanya tendo la ndoa kwenye siku za mwisho za hedhi. Siku ambazo zinakaribiana na siku za yai kupevuka.

Uwezekano wa kushika mimba unapungua zaidi kadiri siku zinazofuata baada ya siku ya yai kupevuka. Kama yai lisiporutubishwa ukuta wa kizazi utabomoka na utaanza kuona damu ikitoka ambayo ndio tunaita hedhi.

Kufatilia siku za hatari kushika mimba kwenye mzunguko

Kufatilia siku zako za hatari itakusaidia usishike mimba ambapo hujatarajia. Ni zoezi ambalo laweza kuchukua miezi miwili mpaka mia4 kulifatilia na kulizoea, kwani yatakiwa kurekodi na kufatilia matukio na mabadiliko yote ya mwili wako.

Unajuaje siku za hatari kushika mimba?

Njia zifuatazo zitakusaidia kujua siku ya ovulation/siku za hatari

1.Kwa miezi 8 mpaka 12 rekodi siku ambayo unaanza hedhi na uhesabu siku zote za kila mzunguko. Siku ya kwanza ni ile unayoanza hedhi katika mwezi husika na hesabu mpaka siku unayoanza hedhi katika mwezi mwingine hapo mzunguko mmoja utakuwa umekamilika.

2.Rekodi mzunguko mfupi na mzunguko mrefu zaidi katika ufuatiliaji wako

3.Kupata siku yako ya kwanza ya hatari chukua namba ya mzunguko mfupi zaidi toa 18, mfano mzunguko wako mfupi ni siku 27-18 inabaki 9.

4.Kupata siku yako ya mwisho ya hatari kwenye mzunguko, chukua siku za mznguko wakko mrefu toa 11. Mfano mzunguko wako mrefu ilikuwa siku 30-11 inabaki 19.
5.Katika mahesabu hapo juu ni kwamba siku kati ya mzunguko mfupi na mrefu ndizo siku zako za hatari, kwa maaana ya kuanzia siku ya 9 na 19 ndizo siku zako za hatari. Kama unataka usishike mimba basi usifanye ngono siku ya 9 ya hedhi mpaka siku ya 19.

Je ni uhakika kiasi gani kutoshika mimba nikifatilia?

Kama una mzunguko usiovurugika ni rahisi zaidi kufatilia na kuepuka mimba. Fahamu tu kwamba siku ya ovulation inaweza kubadilika kulingana na mazingira kama stress, mazoezi, hali ya hewa na lishe.

Njia hii ya kufatilia siku ni hakika zaidi kama unatafuta mimba. Kwa habari ya kuzuia mimba uhakika wake unapungua mno. Ongea na daktari akujulishe njia zingine za hakika zaidi kuzuia mimba na kupanga uzazi.

Njia zingine za kuzuia mimba kwenye siku za hatari

Kuna njia nyingi za kisasa kuzuia usishike mimba ikiwa hujapangilia.Njia hizi ni kama

  • vidonge vya kuzuia mimba
  • kitanzi
  • sindano kama depo
  • njiti na
  • kondomu
  • njia hizi ni hakika zaidi kwa asilimia zaidi ya 90 endapo zikitumika kwa usahihi.

Unahitaji maoni ama ushauri? Tuandikie kwa whatsapp namba 0678626254 utajibiwa, Usipige simu namba ni ya whatsapp tu.

Kama hedhi yako inavurugika unatakiwa kubofya hapa na kusoma

29 replies on “Jinsi ya Kutambua Siku za hatari Kushika Mimba”

Thanks more doctor maisha on provision of awareness and we enjoy it, be blessed more.

Ivi kama mbegu za mwanaume znaweza kaa ndan ya ck5 kweny kizaz je ukimeza kidonge 1 t kabla hujafanya af hz mbeg kama bad zp kwnz kizaz xiwez pata mimba

kwa mwenye mzunguko wa siku 21 nae evolution yake hufanyika baada ya siku 14 ndipo anakuwa kweny hatari ya kushika mimba?

Asantee xana docktar kwaushauli mzuri,nilikuwa naswali binti ambaye nibikra akichukua mimba anaruhusiwa kufanya mapenzi kwamdagan ili ubikra utoke naajifungue salama?

Vizr xan docter kwa ushaul wako ila xaxa nina swal iv unawez kujizuia vp kufany tendo la ndoa mana kuna wengne 2nafany ili mlad ck ziende na ukizingatia ya kwamb kulala pa1 kwa unaxhindwa nn ufany

Mimi mbona mnanichanganya ninyi watoa ushauri..mara wengine mnasema ,ukitaka kupata au kujua sku yako ya hatar chukua mzunguko wako toa na 14 mfano 30-14=16 ndo sku ya uhakika kupata mimb ,wengne tena wanasema chukua 30-18=12 ..asa vp mbna hamueleweki nan tumwelewe sasa?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *