P2 ni kifupi na Postinor-2, ni dawa inayotumika kwa dharula tu. Vidonge vya P2 havitakiwi kutumika kama njia ya mara kwa mara kuzuia mimba.
Vidonge vya p2 vinatakiwa kutumika tu endapo njia zingine za kuzuia mimba zimefeli. Kwa mfano kondomu kupasuka katikati ya tendo au umefanya tendo na kusahau kuvaa kinga na upo kwenye siku za hatari.
Vidonge vya P2 vinafanya kazi kwa kuzuia yai kupevuka wakati wa mzunguko wa hedhi. Pia P2 inafanya uteute wa ukeni kuwa mzito sana na kufanya mbegu kushindwa kuogelea kwenda kwenye yai. Kazi ingine ya P2 ni kubadili ukuta wa mji wa mimba ili kuzuia mimba kujishikiza.
Ufanisi wa Vidonge vua P2
Vidonge vya P2 viazuia kushika mimba endapo vitatumika ndani ya masaa 72 baada ya kufanya tendo bila kinga. Inakadiriwa kwamba P2 ina ufanisi karibu asilimia 85 kuzuia mimba. Endapo vidonge vitatumika ndani ya masaa 24 baada ya kufanya tendo, ufanisi unaongezeka zaidi ya asilimia 95. Ufanisi utazidi kupungua kadiri masaa yanavyosogea.
Kumbuka kutumia vidonge vya P2 hvitasaidia kama tayari una mimba na pia havikuzuii kupata magonjwa ya zinaa kama ukimwi, kisonono na chlamydia.
Dawa hii inaweza isifanye kazi vizuri kwa baadhi ya wanawake hasa wenye uzito mkubwa mfano uzito zaidi ya kilo 74 na kama upo kwenye dozi ingine ya dawa. Zungumza na daktari wako kama dawa itakufaa kulingana na afa yako.
Jinsi ya Kutumia Vidonge vya P2
Endapo unanua dawa famasi na kumeza, hakikisha unasoma vizuri maelekezo ya dawa kabla ya kuanza kutumia. Kama una maswali hakikisha unamuuliza mtoa huduma.
Meza vidonge vya p2 haraka iwezekananvyo baada ya kufanya tedo bila kinga. Matumizi yanaweza kutofautiana kwa bila brand ya dawa. Hivyo muhimu kumuuliza muhudumu wa famasi au daktari namna ya kumeza dawa. Tumia kama ulivyoshauriwa, mara nyingi ni vidonge viwili kwa wakati mmoja, au unameza kidonge kimoja kisha unasubiri masaa 12 unameza kidonge kingine. Dawa ya p2 inaweza kutumika baada au kabla ya kula.
Endapo utatapika ndani ya masaa mawili baada ya kumeza dawa yatakiwa umeze tena. Baada ya kumeza p2, tegemea mabadiliko kidogo kwenye siku ya kupata hedhi na pia aina ya hedhi yako. Endapo utachelewa zaidi ya siku 7 kuanza hedhi jaribu kupima kama mimba iliingia.
Madhara/Matokeo ya Kutumia Vidonge vya P2
Dalili kama kichefuchefu, kutapika, maumivu ya tumbo, kuchoka sana, mabadiliko ya uteute ukeni, matiti kulainika , kuharisha au maumivu ya kichwa vinaweza kutokea baada ya kumeza P2.
Madhara mengine ni
- hedhi kuwa nzito kupita kiasi
- chuchu kuuma
- kukosa kabisa hedhi
- na maumivu ya nyonga.
Kama dalili zitaendelea kuwa mbaya zaidi hakikisha unaenda hospitali kupata huduma. Mjulishe daktari haraka endapo dalili mbaya haziishie kama maumivu ya tumbo hasa baada ya wiki 3 mpaka 5 baada ya kumeza p2.
Tahadhari kabla ya kumeza P2
Kabla ya kuanza kumeza P2 mjulishe daktari au mfamasia anayekuhudumia kama una allergy na dawa au aleji ingine yoyote.
Kabla ya kumeza P2 mjulishe daktari historia yako hasa kama unatokwa na damu kila mara ukeni.
Dawa zinaweza kukufanya ukose balansi na utimamu wa mwili. Kutumia pombe au bangi inaweza kuongeza zaidi tatizo. Usiendeshe gari au chombo chochote cha moto au kufanya kazi yoyote inayohitaji umakini mkubwa.
Endapo unatarajia kufanyiwa upasuaji ia mjulishe daktari dawa unazotumia
Endapo unaugua magonjwa yoyote kama figo, moyo, kisukari, saratani, ini au stroke, hakikisha unamjulisha daktari kabla hujameza p2. Na usimze P2 kama tayari una ujauzito.
Mwingiliano wa Vidonge vya P2 na dawa zingine
Mwingiliano wa dawa unaweza kupelekea kupungua kwa ufanisi wa aina moja ya dawa na pia kuongeza hatari ya madhara ya dawa. Andiko hili halijumuishi maelezo yote juu ya mwingiliano wa dawa, ndiomaana kuna umuhimu wa kusoma karatasi ya ndani(leaflet) kwenye box la dawa. Kulingana na brand ya dawa maelezo ya mwingiliano yanaweza kutofautiana.
Hakikisha unamweleza daktari au mfamasia anayekuhudumia list yote ya dawa unazotumia ikiwemo tiba asili. Baadhi ya dawa hupunguza ufanisi wa P2, dawa kama za kifafa na Ukimwi.
Namna ya Kuhifadhi Vidonge vya P2
Dawa zibaki kwenye cover yake mpaka muda wa kumeza unapofika.
Hifadhi dawa zako eneo lenye joto la wastani. Joto linaweza kuathiri ufanisi wa dawa. Weka mbali na watoto.
Kurejesha hedhi baada ya kumeza P2
Kama dawa zimekuathiri na kupelekea ukose hedhi ama hedhi yako ivurugike, tunashauri utumie vidonge hivi asili visivyo na kemikali vya evecare. Ni dozi ya wiki mbili na hedhi yako itaerejea vizuri.
tahadhari
Kuna wimbi kubwa la wajasiliamali mitandaoni wanauza vidonge fake vya evecare, tena wanauza kwa bei rahisi sana. Watu hao siyo madaktari wala siyo wataalamu wa afya na wanauza bidhaa feki ambazo ni hatari wa afya yako. Wengi wao hawana hata ofisi, ukipata madhara unakosa pa kuuliza. Kuwa makini na watu hao, wamejaa sana insta na fb
Kumbuka vidonge hivi vya evecare siyo kwa ajili ya kuzuia mimba., bali ni kurekebisha hedhi yako ikia imevurugika baada ya kutumia P2 na dawa zingine za uzazi wa mpango. Gharama ya evecare ni tsh 75,000/=. Tuandikie whatsapp namba 0678626254 upate Evecare.
8 replies on “Vidonge vya P2, Matumizi, Faida na Madhara”
Nataka kujua mtu ‘hutoa mimba ikiwa n mwezi gapi?
Ooh sory Marcy, huwa hatushauri kabisa watu kutoa mimba
thank you for massage
Vidonge hvyo kwa mwanaume nihatal au nikwajil ya wanawak
havitumiki kwa wanaume, ni wanawake tu
Thanks for your advice doctor
Kwa mfano nilale na mwanaume ikiwa ni siku yangu ya mwixho kwa mzunguko kabla nipate hedhi alafu nimeze p2 inaeza nixaidia nisipate mimba
Inatakiwa imezwe kabla au baada ya tendo la ndoa?