Categories
Afya ya mwanamke na uzazi

Namna ya Kuhesabu umri wa mimba na Siku ya kujifungua

umri wa mimba

Nawezaje kujua umri wa mimba? Mpaka sasa umeshapima kwa UPT na umejua una mimba. Bilashaka una furaha sana maana sasa unakaribia kuitwa mama. Lakini pengine una kiu ya kujua mimba yako iliingia lini au ina umri gani. Pengine una wapenzi wawili na wote umekutana nao katika muda usiozidi wiki moja, sasa unawaza mimba hii ya nani?.

Lengo la makala hii ni kukwelekeza jinsi gani unaweza kuhesabu na ukajua umri wa mimba,bila hata kwenda hospitali.

Namna ya kuhesabu umri wa mimba

Kwanza muhimu ujue tafsiri ya hivi vifupi kwa maana vitatumika sana.
LMP yaani last menstural period, ikimaanisha siku ya kwanza kuanza hedhi yako ya mwisho kabla hujashika mimba na EDD-Estimated delivery date, yaani makadirio ya siku yako ya kujifungua.

Watoa huduma yani manesi na madaktari huwa wanapima umri wa mimba kwa kucheki kwanza lini ulipata hedhi yako ya mwisho. Kama mzunguko wako ni ule wa kawaida yani siku 28 maana yake siku ya hatari ni ya 14, kwahivo hapo mimba ilitungwa week mbili baada ya LMP. Sasa kwenye kuhesabu umri wa mimba hizi week mbili huwa zinaongezwa.

Kumbuka kwamba haya ni makadirio na siyo umri sahihi wa mimba. Kupima siku ya kujifungua, ongeza siku 280 ambazo ni wiki 40 kwenye siku yako ya kwanza kuanza hedhi ya mwisho, endapo una mzunguko wa siku 28.

Nitajuaje ni lini siku nilishika mimba?

Kitaalamu tunaita conception date- ni siku ambapo mimba ilitungwa. Kwasababu mbegu zinaweza kukaa kwenye kizazi mpaka siku 6, urutubishaji unaweza kutokea siku yoyote katika hizo siku 6 baada ya tendo. Mimba kutungwa kunategemea na yai limepevuka na kutolewa lini. Kama yai lipo tayari limeshatolewa na mbegu zimeingia, basi ndani ya masaa 24 mimba inatungwa.

Siku ya kujifungua

Mwanzoni utakuwa na hamu ya kujua umri wa mimba, ila kadiri miezi inavosogea sasa utakuwa na kiu ya kujua lini utajifungua? Muhimu fahamu tu kwamba unaweza kupata uchungu kabla a baada ya siku ya makadirio. Pengine daktari amekufatilia na ameona unahitaji kufanyiwa upasuaji, au kuchomwa sindano ya uchungu mapema. Vyote hivi vinachangia mabadaliko ya siku ya makadirio.

Kipimo cha utrasound kugundua umri wa mimba

Utrasound ni kipimo kinachotumia mawimbi ya sauti kupata picha za ndani ya mwili. Kujua ukubwa wa mimba na hata jinsia, watoa huduma wanaweza kutumia kipimo hiki cha utrasound. Pia utrasound inaweza kugundua kama mtoto ana changamoto za kiafya kama kushindwa kukua vizuri.

Vipi kama nilipandikiza kwa IVF, najuaje umri wa mimba?

Kwanza muhimu kujua IVF ni nini. IVF ni kifupi cha invitro fertilization, ni njia ya kupandikiza mimba ambapo mbegu na yai zinarutubishwa nje ya mwili, kisha kiume kinapandikizwa kwenye kizazi ili kikue.

Kwavile mimba hujapata kiasili, hata naman ya kufanya madadirio ya umri wa mtoto ni tofauti.

  • Kama yai fresh limetumika, utajumlisha siku 266 kutoka kwenye siku yai limetolewa kwenye kizazi chako kwa ajili ya urutubishaji
  • kama yai lilitunzwa kwa siku 3 basi jumlisha siku 263 kutoka kwenye siku ya upandikizaji
  • Kama mayai yalitunzwa kwa siku 5, basi utajumlisha siku 261 kwenye siku ya upandikizaji.

Namna ya kuhesabu siku ya kujifungua

Kujua siku ya makadirio yaako, muhudumu anaangalia siku ya mwisho kuanza hedhi na pia utrasound yako ya kwanza. Kisha watajumlisha siku 280 yani wiki 40 kwenye LMP. Baada ya hapo wnalinganisha na makadirio kwenye utrasound na kutoa siku ya kujifungua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *