Fangasi mdomoni kwa kitaalamu oral thrish au oral candidiasis ni maambukizi ya fangasi aina ya candida kwenye kuta laini za mdomo.
Kwa watu wengi wenye fangasi ya mdomo haileti changamoto kubwa sana na wanaweza kuishi na wagonjwa na maisha yakaendelea. Japo kwa watu wenye kinga dhaifu fangasi wa mdomoni huleta athari sana na dalili mbaya zaidi.
Habari njema ni kwamba wagonjwa wengi wanapona vizuri kabisa wakipatiwa tiba kwa fangasi za mdomoni. Japo wagonjwa wengi huugua tena katika kipindi cha muda mfupi baada ya kupona hasa kama chanzo cha fangasi kwa upande ni uvutaji wa sigara. Katika makala hii tutakwelekeza chanzo cha fangasi mdomoni, dalili zake pamoja na tiba.
Dalili za fangasi mdomoni
Kwa watu wazima dalili kuu ya fangasi mdomoni ni utando mweupe mzito kwenye ulimi. Endapo utando huu ukikwanguliwa mgonjwa anaweza kutokwa na damu. Baada ya muda utando huu unaweza kubadilika na kuwa malengelenge ya rangi nyekundu.
Chanzo cha fangasi mdomoni
Fahamu kwamba fangasi aina ya candida wapo maeneo mengi sana ya mwili. Kama kwenye mdomo, ukeni, mkunduni, kwenye ngozi, na tumboni pia. Katika hali ya kawaida ya mwili, fangasi hawa hawana madhara kabisa.
Pale kinga ya mwili inaposhuka ndipo fangasi hawa wanapata muda wa kumea na kushambulia mwili. Kuvurugika kwa mazingira ya mdomo kutokana na kutumia dawa zingine ni chanzo pia cha fangasi hawa wa candida kukua na kuleta madhara.
Mazingira yanayongeza hatari ya kupata fangasi mdomoni.
Kwa watu wazima mambo yafuatayo yanakuweka kwenye hatari zaidi ya kupata fangasi ya mdomoni kiurahisi.
Watu wanaotumia meno bandia(dentures) ili kuziba jino lililon’golewa-hatari ni kubwa endapo meno bandia haya hayataondolewa wakati wa kulala ama yasipofitishwa vizuri.
Antibiotics– matumizi ya dawa za kuuma vimelea wa bakteria maarufu kama antibitics kwa muda mrefu yanakuweka kwenye hatari zaidi ya kuugua fangasi mdomoni. Kwani dawa hizi huua mpaka bakteria wazuri waliopo mdomoni ambao ni kinga dhidi ya fangasi wabaya.
Matumizi ya mothwash kwa muda mrefu–
Watu wanaotumia mouthwash kwa muda mrefu ili kutibu harufu mbaya mdomoni wako kwenye hatari zaidi ya kupata fangasi mdomoni, kwasababu mouthwash zinaua na bakteria wazuri.
Matumizi ya dawa za homoni(Steroid medication) kama zile za kusisimua misuli.
Kinga kushuka– watu wenye kinga dhaifu wanaugua sana fangasi mdomoni, kinga dhaifu inaruhusu fangasi kukushambulia kiurahisi.
Kuugua kisukari
Wagonjwa wa kisukari huwa na kinga dhaifu sana na hivo kushambuliwa haraka na fangasi wa mdomoni.
Mdomo mkavu-watu wenye mate kidogo kitaalamu(xerostomia) wako kwenye hatari zaidi ya kuugua fangasi mdomoni.
Lishe- ukosefu wa madini na vitamini muhimu mwili kutokana na lishe mbovu hupelekea kinga kushuka na hivo kuruhusu mwili kushambuliwa kiurahisi na fangasi mdomoni. Lishe yenye upungufu wa madini chuma, vitamin B12 na folic acid ni chanzo cha kuugua fangasi.
Kuvuta sigara- wavutaji wa sigara kupita kiasi wanapelekea kuvurugika kwa mazingira ya mdomo na hivo kuugua fangasi haraka.
Uchunguzi wa daktari hospitali ili kugundua Fangasi mdomoni
Kwa kiasi kikubwa uchunguzi wa fangasi mdomoni hufanyika kwa daktari kutazama kinywani mwako na kukuuliza baadhi ya maswali. Daktari anaweza kuchukua baadhi ya sample ya utando wako mdomoni na kuepeleka maabara kwa ajili ya vipimo. Kama daktari atagundua chanzo cha tatizo lako basi atakupatia tiba kulingana na chanzo husika.
Tiba Kupitia Vidonge vya Propolis
Ni vidonge asili viliyotengenezwa kupitia bidhaa adimu ya propolis ili kutibu mambukizi sugu ya fangasi mwilini. Dozi moja inatumika kwa wiki mbili, unameza kila siku vidonge viwili asubuhi na jioni. Huhitaji kufanya utafiti ni dawa ipi nzuri, tayari tumeshafanya hivo kwa zaidi ya miaka mitano sasa na kukuletea dawa hii iliyothibitishwa.
Baada ya kutumia propolis tegemea haya ndani ya wiki mbili
- Fangasi yako kupona kabisa
- Dalili zote mbaya mbaya muwasho na maumivu kuisha
- Kinga ya mwili kuimarika na fangasi kutojirudia