Categories
Uncategorized

Dalili za yai Kupevuka kwenye siku za hatari

yai kupevuka

Ikiwa unatafuta kushika mimba, kukwepa kushika mimba isiyotarajiwa au pengine unataka tu kuelewa mwenendo wa mwili wako, kuelewa mzunguko wako ni jambo la muhimu sana. Yai kupevuka kitaalamu tunaita ovulation, ni kipindi kifupi sana lakini chenye matokeo makubwa kwa mwili wako.

Nini maana ya yai kupevuka?

Kwanza muhimu kujua ovulation ni nini? Ovulation ni kipindi katika mzunguko wa hedhi wa mwanamke ambapo yai lililokomaa linatolewa kwenye mfumo wa mayai(ovari), kwa ajili ya kufanyiwa urutubishaji na mimba ifanyike. Yai likishatolewa kwenye ovari, linaenda mpaka kwenye mrija wa uzazi, hapo yai linaweza kuishi mpaka saa 48. Endapo hakuna mbegu imerutubisha yai basi litavunjika na kutolewa nje.

Je ni Lini yai linapevuka kwenye mzunguko wa hedhi?

Hili ni swali zuri sana ambalo kila mwanamke huwa anajiuliza. yai linatolewa hasa baada ya siku 14 hedhi ilipoanza, kwa mzunguko wa siku 28.

lakini muhimu ujue kwamba siyo kila mwanamke basi siku yake ya hatari ni ya 14. Wengine wana mzunguko mfupi zaidi mpaka siku 21 na wengine miznunguko mirefu mpaka siku 35. Endapo hujui mzunguko wako basi bofya makala hii (Jinsi ya kufatilia siku za hatari kwa mizunguko yote) usome kwanza kisha urudi kumalizia makala ya sasa.

Je ovulation inaisha baada ya masaa mangapi?

Mchkato mzima wa yai kutolewa inachukua masaa 36. Kitendo chenyewe cha yai kutoka kwenye ovari ni cha haraka, ispokuwa mabadiliko ya homoni kuelekea zoezi husika yanaanza mapema zaidi.

Ni zipi dalili za yai kupevuka?

Habari njema ni kwamba mwili wa mwanamke unatoa viashiria vingi kuonesha kwamba hizi ni siku za hatari na yai limevevuka tayari kwa kurutubishwa. Siyo kila mtu atapata dlaili hizi zote, lakini lazima kuna dalili kadhaa utaziona endapo utausikiliza mwili vizuri. Kwahivo usijione mnyonge na kuhisi yai halijapevuka endapo utapata dalili chache katika hizi nitakazokuelezea leo.

1.Uteute wa kuvutika

Lazima utakuwa umewahi kusikia kuhusu ute wa uzazi ama ute wa ovulation, ama kuona uchafu mwembemba unaovutika kwenye chupi. Huu ndio ute unaoashiria kwamba yai limepevuka na litatolewa ndani ya masaa 24 tang ute umeanz akutoka. Uteute huu unakuwa mwepesi kama yai, unavutika na hauna harufu.

2.Tumbo kujaa kipindi ya yai kupevuka

Yawezekana umewahi kuhisi tumbo kujaa katika siku flani katikati ya mzunguko wa hedhi na usijue kwanini. Mabadiliko ya homoni hasa kuongezeak kwa homoni la LH inaweza kufanya tumbo kubakiza maji na hivo kuvimba kiasi. Lakini usiogope sana hali hii ni ya masaa machache na utakuwa sawa.

3.Kichefuchefu kwenye siku za yai kupevuka

Unaweza kupata hali ya kuhisi kichefuchefu ukiwa kwenye siku ya ovulation, hii pia ni kutokana tu na mabadiliko ya homoni.Endapo utapata na hali hii, jaribu kutembea nje upate hewa safi na utafune tangawizi.

4.Mabadiliko ya joto la mwili kipindi cha cha yai kupevuka

Kwenye siku za hatari, hasa siku yenyewe yai linapotolewa, joto la mwili huongezeka kidogo kwa centigrade 0.3. Unaweza kununua kipimajoto pharmacy ukajipima mwenyewe nyumbani na kuona mbadiliko haya.

5.Maumivu ya tumbo upande mmoja, kutokwa na matone ya damu

Je wafahamu kwamba unaweza kupata maumivu kipindi cha yai kutolewa? Maumivu haya yanatokana na kitendo cha yai kutoka kwenye kikonyo chake ambacho ni mfumo wa mayai(ovari). Kitendo hiki pia chaweza kupelekea damu itoke kwenywe kovu na hivo ukaona matone kidogo kwenye chupi. Kuanzia sasa endapo utaona damu kidogo katikati ya mzunguko basi usiogope, jua tu kwamba ni yai linatolewa.

Ni muda gani sahihi kufanya tendo endapo unatafuta mimba kwa mda mrefu bila mafanikio?

Pengine sasa unajiuliza wewe na mwenzi wako mkutane lini ili kuongeza chansi ya kupata mimba haraka? Siku nzuri na yenye chansi kubwa kupata mimba ni siku ambapo yai limetolewa na masaa 24 yanayofuatia. Na pia siku 5 kabla ya yai kutolewa.

Kwanini siku 5 kabla? kwasababu mbegu zinaweza kuishi mpaka siku 5 kwenye kizazi baada ya kufanya tendo. Kwahivo kumbe mbegu zaweza kulisubiri yai litolewe hukohuko ndani.

Categories
Afya ya mwanamke na uzazi

Namna ya Kuhesabu umri wa mimba na Siku ya kujifungua

umri wa mimba

Nawezaje kujua umri wa mimba? Mpaka sasa umeshapima kwa UPT na umejua una mimba. Bilashaka una furaha sana maana sasa unakaribia kuitwa mama. Lakini pengine una kiu ya kujua mimba yako iliingia lini au ina umri gani. Pengine una wapenzi wawili na wote umekutana nao katika muda usiozidi wiki moja, sasa unawaza mimba hii ya nani?.

Lengo la makala hii ni kukwelekeza jinsi gani unaweza kuhesabu na ukajua umri wa mimba,bila hata kwenda hospitali.

Namna ya kuhesabu umri wa mimba

Kwanza muhimu ujue tafsiri ya hivi vifupi kwa maana vitatumika sana.
LMP yaani last menstural period, ikimaanisha siku ya kwanza kuanza hedhi yako ya mwisho kabla hujashika mimba na EDD-Estimated delivery date, yaani makadirio ya siku yako ya kujifungua.

Watoa huduma yani manesi na madaktari huwa wanapima umri wa mimba kwa kucheki kwanza lini ulipata hedhi yako ya mwisho. Kama mzunguko wako ni ule wa kawaida yani siku 28 maana yake siku ya hatari ni ya 14, kwahivo hapo mimba ilitungwa week mbili baada ya LMP. Sasa kwenye kuhesabu umri wa mimba hizi week mbili huwa zinaongezwa.

Kumbuka kwamba haya ni makadirio na siyo umri sahihi wa mimba. Kupima siku ya kujifungua, ongeza siku 280 ambazo ni wiki 40 kwenye siku yako ya kwanza kuanza hedhi ya mwisho, endapo una mzunguko wa siku 28.

Nitajuaje ni lini siku nilishika mimba?

Kitaalamu tunaita conception date- ni siku ambapo mimba ilitungwa. Kwasababu mbegu zinaweza kukaa kwenye kizazi mpaka siku 6, urutubishaji unaweza kutokea siku yoyote katika hizo siku 6 baada ya tendo. Mimba kutungwa kunategemea na yai limepevuka na kutolewa lini. Kama yai lipo tayari limeshatolewa na mbegu zimeingia, basi ndani ya masaa 24 mimba inatungwa.

Siku ya kujifungua

Mwanzoni utakuwa na hamu ya kujua umri wa mimba, ila kadiri miezi inavosogea sasa utakuwa na kiu ya kujua lini utajifungua? Muhimu fahamu tu kwamba unaweza kupata uchungu kabla a baada ya siku ya makadirio. Pengine daktari amekufatilia na ameona unahitaji kufanyiwa upasuaji, au kuchomwa sindano ya uchungu mapema. Vyote hivi vinachangia mabadaliko ya siku ya makadirio.

Kipimo cha utrasound kugundua umri wa mimba

Utrasound ni kipimo kinachotumia mawimbi ya sauti kupata picha za ndani ya mwili. Kujua ukubwa wa mimba na hata jinsia, watoa huduma wanaweza kutumia kipimo hiki cha utrasound. Pia utrasound inaweza kugundua kama mtoto ana changamoto za kiafya kama kushindwa kukua vizuri.

Vipi kama nilipandikiza kwa IVF, najuaje umri wa mimba?

Kwanza muhimu kujua IVF ni nini. IVF ni kifupi cha invitro fertilization, ni njia ya kupandikiza mimba ambapo mbegu na yai zinarutubishwa nje ya mwili, kisha kiume kinapandikizwa kwenye kizazi ili kikue.

Kwavile mimba hujapata kiasili, hata naman ya kufanya madadirio ya umri wa mtoto ni tofauti.

  • Kama yai fresh limetumika, utajumlisha siku 266 kutoka kwenye siku yai limetolewa kwenye kizazi chako kwa ajili ya urutubishaji
  • kama yai lilitunzwa kwa siku 3 basi jumlisha siku 263 kutoka kwenye siku ya upandikizaji
  • Kama mayai yalitunzwa kwa siku 5, basi utajumlisha siku 261 kwenye siku ya upandikizaji.

Namna ya kuhesabu siku ya kujifungua

Kujua siku ya makadirio yaako, muhudumu anaangalia siku ya mwisho kuanza hedhi na pia utrasound yako ya kwanza. Kisha watajumlisha siku 280 yani wiki 40 kwenye LMP. Baada ya hapo wnalinganisha na makadirio kwenye utrasound na kutoa siku ya kujifungua.

Categories
Afya ya mwanamke na uzazi Tendo la ndoa Uncategorized

Nini kinatokea baada ya kupoteza bikira yako?

kupoteza bikira

Bikira ni kitu gani??

Tafsiri iliyozoeleka ya bikira ni mwanamke ambaye hajawahi kabisa kufanya tendo la ndoa katika maisha yake. Kwahivo mwanamke anapoingiliwa ukeni kwa mara ya kwanza anapoteza ile bikira yake.

Nini kinatokea mwilini baada ya kupoteza bikira?

Tendo la ngono laweza kupelekea mabadiliko mengi ya mwili. Hapa chini ni maelezo ya kinatokea

1.Mabadiliko ya ukeni

Watu wengi huamini kwamba tendo la ndoa linafanya uke kutanuka na kuwa mkubwa ama kulegea. Kumbuka uke unaweza kutanuka na kuzaa mtoto na kisha ukarudia hali yake ya mwanzo. Uume ni mdogo sana ukilinganisha na mtoto na hauwezi kufanya uke kulegea.

Kwa baadhi ya wanawake wanapoanza tendo hawapati raha, hasa kama uke wako ni mkavu naa hukuandaliwa vizuri. Hakikisha unafanya michezo mingine ya kutomasana kwa mda mrefu kabla ya kuanza tendo lenyewe.

2.Matiti

Kwa baadhi ya watu kufanya tendo kunaweza kupelekea matitti na chuchu kuvimba. Hii inatokea kwasababu zile hisia na muhemko wa kutaka kufanya tendo inapelekea mzunguko wa kasi wa damu kuelekea kwenye matiti, uke na uume pia.

3.Mabadiliko ya homoni

Wakati wa tendo ubongo unatoa vichocheo vingi sana kuelekea kwenye damu.Kazi ya vichocheo hivi ni kukufanya ujiskie raha ya tendo lenyewe na kuongeza upendo kati yako na mpenzi wako.

Je unaweza kushika mimba siku ya kwanza kufanya tendo?

Jibu ni ndio, unaweza kushika mimba siku ile tu ya kwanza kukutana na mwanaume. Mbegu tu zikiingia ndani ya uke unaweza kushika mimba. Kama hutaki kushika mimba mapema basi hakikisha unatumia condom muda wote wa tendo ama waweza kumeza p2.

Je ni umri gani sahihi wa wanawake wengi kupoteza bikira?

Wastani wa umri wa kupoteza bikira kwa wanawake wengi ni kati ya miaka 16 na 17. Katika umri wowote ule, kufanya tendo kwa mara ya kwanza ni jambo la tofauti sana na hisia zake zinatofautiana. Siyo kila mtu hufurahi tendo siku ya kwanza, wengi hupata maumivu na kuhisi kujuta. Na wengine hupata mawazo sana na hofu pengine wameshapata mimba au magonjwa ya zinaa

Jinsi ya kufanya tendo na kupoteza bikira bila maumivu

Hakuna njia moja ya kuondoa maumivu asilimia 100 siku ya kwanza unapofanya tendo, ila kuna vitu vichache vya kufanya kupunguza maumivu. Ukiwa na mpenzi asiye na haraka ya kuingiza uume, na pia awe mwelewa itakusaidia sana kufurahia tendo na kupunguza maimivu siku ya kwanza. Kuna mambo mengine mengi waweza kufanya yakakusaidia, endelea kuyasoma hapa chini

1.Ongea na mpenzi wako kabla ya tendo

Usiogope kuongea na mtu wako namna unavojiskia, vitu unavyoogopa na usichokipenda. Una kila haki ya kujieleza kwa uwazi ili akuvumilie. Kuongea na mwenzio kunasaidia kupunguza ile hofu ulokuwa nayo kuhusu kufanya mapenzi.

2.Fanya maandalizi ya kutosha

Hakika uke unaloa vizuri na kuwa mlaini sana kabla ya kuingiliwa na mwenzako hii inapunguza sana maumivu. Maandalizi haya ni pamoja na michezo kadhaa mkiwa uchi, kushikana sehemu za siri, kunyonyana uke na uume, na ndimi na kuambiana maneno matamu.

Chukueni walau nusu saa mpaka lisaa la maandalizi kabla ya tendo, msiende haraka.

3.Jaribu mikao na style tofauti za kufanya tendo

Kama unapata maumivu kwenye aina moja ya style ya kufanya tendo jaribu kubadili na utumie style zingine. Hizi ni baadhi ya style za kufanya tendo.

Style ya kwanza:Tumia mto chini ya mgongo na kukufanya ubinuke kidogo. Kunja magoti kisha chanua miguu yako ili uke ubaki wazi.

Style ya pili:Mwanamke kushika ukuta, na kubinuka kidogo kisha mwanamume anakunja kwa nyuma na kumuingilia ukeni

Style ya kifo cha mende: Hii ni nzuri kwa kuanzia, karibu kila mwanafunzi wa mapenzi anaanzia hapa: ukizoea hii style ya mwanamke kulala chini na mwanaume kuja kwa juu ndipo uanze kujaribu style zingine

4.Usijiwekee malengo makubwa kivile

Kutokana na kukua kwa teknoligia, lazima utakuwa umeshatazama picha na video za ngono namna watu wanavoingiza kwenye movie chafu za ngono. Na kwenye akili yako umeweka matazamio flani, kwamba unachokiona ndicho kitatokea utakapioanza mapenzi. Hii siyo kweli, wanaoigiza na kurekodi vidoe za ngono wanatumia madawa kuamsha hisia zao na ni wazoefu sana kufanya tendo.

Usijilinganishe nao, kuwa mpole na jipe muda, huwezi kuwa mzoefu kwa siku moja. Siku ya kwanza unaweza kushindwa kabisa kufanya tendo na baadae ukaweza. Hivo tuliza mihemko na ufanye taratibu

5.Hakikisha Eneo la kufanya tendo ni tulivu

Siku yako ya kwanza kufanya tendo inatakiwa kufanyika mahali pazuri pasio na kelele wala vitu hatari.Yatakiwa iwe sehemu ambapo wote wawili mke na mme mnatulia kiakili. Siyo kwenu vichaka au kwenye gari.

Kitanda ni sehemu nzuri zaidi ya kufanya tendo siku ya kwanza. Fanya usafi kwenye chumba chako na kuondoa kelele zozote. Hakikisha hakuna watu wengi eneo hilo na uzime simu. Unaweza kufungulia redio kwa mbali ili upate mziki wa kukusindikiza.

Categories
Ulaji mzuri na Afya ya Tumbo

Njia 7 za kulainisha choo

Kukosa choo na choo kigumu ni moja ya matatizo makubwa zaidi hapa kwetu. Kwani kila siku zaidi ya wagonjwa watano hunitafuta kwa shida hii. Pamoja na kwamba kuna dawa nyingi za kulainisha choo unazoweza kuzipata pharmacy, bado utakuwa hujasolve chanzo cha tatizo. Utaendelea kukosa choo na kupata choo kigumu baada tu ya kumaliza dawa zako.

Tiba na njia asli za kurekebisha mfumo wako wa chakula ndio suluhisho la kudumu. Njia hizi asili zinajumuisha vajula, mimea tiba na hata vitu unavyokunywa.

Mfumo wa ulaji ni tatizo

Dunia ya sasa imebadili mfumo wa ulaji na kutamnguliza biashara zaidi. makampuni makubwa ya kutengeneza vyakula yanashindana kupata faida na kufanya mauzo zaidi ya vyakula vyao, bila kuzingatia afya ya mlaji.

Miili yetu imeumbwa kwa namna ya kipekee sana ya kusafisha sumu, tunachotakiwa tu kuupa mwili malighafi stahiki na maji salama ili mtambo ufanye kazi. Muhimu sasa ujue kwanza chanzo cha tatizo lako kabla hujaanza kujitibia. Tuendelee..

Nini kinapelekea ukose choo na kupata choo kigumu?

Sababu hizi ndio chanzo cha tatizo lako

  • kula vyakula vya kusindikwa kiwandani visvyo na kambakamba
  • msongo wa mawazo
  • kukosa usingizi wa kutosha na
  • kutokunywa maji ya kutosha
  • kutoshugulisha mwili-mazoezi

Je Unatakiwa Kunya Mara ngapi kwa siku/wiki?

Wataalamu wengi wanapendekeza kwamba ni muhimu kwenda haja kubwa walau mara tatu au zaidi kwa wiki. Japo hili linatofautiana sana kwa kila mtu, kulingana na aina ya kazi anazofanya, chakula anachokula na hata mazingira aliyopo mtu huyu.

Kiujumla kama huendi kunya walau mara 3 kwa wiki, unatakiwa kufanya mabadiliko kwenye lishe yako na kutibu tatizo. Endelea kusoma kujua njia 10 zilizothibitishwa kukutibu choo kigumu.

Njia 7 za kulainisha choo na kukufanya upate choo kila siku

1.Kambakamba/fibers zinasaidia kulainisha choo

Hii ni hatua ya kwanza kabisa kwenye kurekebisha mfumo wako wa chakula. Anza kwa kuongeza vyakula vyenye kambakamba kwenye mlo wako kila siku. Na hakikisha unapata kambakamba hizi kutoka kwenye vyakula asili(ambavyo havijakobolewa na kusindikwa)

Matunda na mboga zenye kambakamba kwa wingi ni pamoja na

  • maparachichi
  • zabibu
  • bamia
  • spinach na

2.Kunywa maji ya kutosha

Kumbuka viungo vyako kama ini na figo vinahitaji maji mengi ili kusafisha damu, kuzalisha mkojo na kutoa taka mwilini.
Kama hutumii maji mengi, anza kubadili sasa ratiba yako, kunywa maji kila unapopata kiu, usinywe soda au pombe.

3.Tumia zaidi Vyakula vinavyoongeza bakteria wazuri tumboni

Kwenye tumbo kuna uwiano wa bakteria wazuri na wabaya. Endapo bakteria wabaya wataongezeka kupita kiasi, mazingira ya uchakataji chakula yatavurugika. Hapo taanza kupata dalili mbaya kama kukosa choo na choo kigumu, tumbo kujaa gesi na chakula kutosagwa vizuri.

Kuimarisha uwiano huo hakikisha unakula zaidi vyakula kama maziwa mtindi, chiaseed na flaxseed. Hakikisha tu unaoponunua maziwa, nunua yale asili. Achana na maziwa ya pakiti siyo salama kwako.

4.Aloe vera

Ukiniambia ni mmea gani utalainisha choo kwa haraka zaidi, nitakwambia ni Alo vera. Ni mmea unaotumika tangu miaka ya kale. Aloe vera pia inasaidia kupambana na vimelea wabaya, gesi tumboni na kuharakisha usagaji wa chakula.

Kwavile mmea wa aloe vera ni mchungu sana hakikisha unapata vidonge, ama juisi yake kutoka kwenye chanzo cha kuaminika. Unaweza pia kufika ofsini kwetu tukakupa vidonge vya aloevera.

5.Chia Seeds

chakula cha kulainisha choo

Moja ya faida ya chia seeds ni uwezo wake wa kufyonza maji kwenye mfumo wa chakula, na hivo kukuletea choo kilaini.

Chia seed zinatoa gram 10 za kambakamba kwa ujazo wa kijiko kimoja cha chakula. Muunganiko wake na majimaji unatengeneza jelly inafofanya choo kisukumwe kwa uzuri sana bila kutumia nguvu. Hakikisha unatumia vijiko vi3 kwa siku.
Matumizi: zioshe mbegu zako vizuri kisha ziloweke kwenye maji kwa nusu saa(vijiko viwili kwa ujazo wa kikombe kimoja cha chai). Tengeneza juis yako au salad, kisha weka chia seeds na blend pamoja.

6.Mboga za majani za kijani

Ukiacha kambakamba, mboga zilizokolea ukijani zina madini mengi ya magnesium. Magnesium ni madini muhimu kwenye kulainisha choo chako. Pasipo magnesium, ni ngumu kwa choo kusafiri kwenye mfumo wako.

7.Tui la nazi

Tui la nazi pamoja na maji ya madafu ni mazuri sana kwako wewe mwenye shida ya choo. Pamoja na utamu wake kutokana na sukari yake asili, maji haya yanalainisha choo kwasbaabu ya uwepo wa madini ya potasium ndani yake. Anza sasa kunywa maji ya mdafu na tui la nazi. Unaweza kuongeza viungo kama tangawizi, kisha ukachemsha kidogo tui pamoja na machicha kwa dakika 5 kabla ya kuchuja na kunywa.

Maelezo ya mwisho

Dawa za hospital za kulainisha choo siyo tiba kwako, ni suluhisho la mda mfupi tu, kisha unarudi kule kule. dawa hizi ukitumia mda mrefu zitavuruga mazingira ya tumbo na tatizo kuwa kubwa zaidi.

Baadhi ya vyakula na mimea tiba zitakusaidia kurekebisha mfumo wa ko wa chakula, bila dawa za pharmacy. Na njia hizi ni salama na zinapatikana sokoni tu.

Kurekebisha mfumo wa chakula siyo jambo la siku moja. inataka kujiwekea malengo ya mda mrefu na kufatilia kila siku. Ukishajijengea tabia ya kula vyakula asili usiache endelea nayo siku zote, hapo hautapata tena shida ya choo.

Categories
Mifupa na Joints

Mifupa kusagika

mifupa kusagika

Mifupa kusagika kitaalamu tunaita osteoarthritis, ni ugonjwa uliopo kwenye kundi la degenerative disease. Haya ni magonjwa yanayosababishwa na kuchoka au kuharibika kwa muundo wa kiungo mpaka kupelekea kuzorota kwa ufanisi wake siku hadi siku.

Mifupa kusagika ama osteoarthritis inatokea zaidi mtu anavozeeka ama umri kwenda. Mabadiliko yanayopelekea mifupa kusagika yanatokea taratibu sana na yanaweza kuchukua miaka mingi mpaka kuleta athari. Japo katika mazingira flani hali yaweza kujitokeza katika umri mdogo.

Kuvimba na majeraha kwenye joint kunapelekea mabadiliko ya mifupa, kulegea na kuvunjika kwa maungio na hivo kupelekea maumivu na kuvimba kwa joint.

Kuna aina kuu mbili za mifupa kusagika (osteoarthritis)

primary osteoarthritis ambayo inaathiri zaidi vidole, uti wa mgongo,hips, magoti na kidole gumba.
Secondary: hii inatokea kutokana na tatizo lililokwepo awali mfano jeraha la kujirudia, baridi yabisi kama gout na rheumatoid arthritis na magonjwa ya kurithi ya joints.

Nani anaweza kupata shida ya kusagika mifupa?

Karibu asilimia 80 ya watu wazima wenye umri zaidi ya miaka 55 wanapata osteoarthritis. Kati ya hawa, asilimia 60 wana dalili za mifupa kusagika. Na inakadiriwa kwamba zaidi watu milioni 240 duniani kote wana dalili za mifupa kusagika. Wanawake waliokoma hedhi wapo kwenye hatari zaidi kutokana na kupungua kwa uzalishaji wa homoni ya estrogen.

Magonjwa au vitu gani hatarishi hupelekea mifupa kusagika?

Ukiacha swala la umri na magonjwa ya joints kama baridi yabisi, kuna mazingira na magonjwa yanayoongeza hatari ya kutokea kwa tatizo la mifupa kusagika. Fatilia maelezo yake kwa kina hapa chini.

1.Uzito mkubwa na kitambi: uzito mkubwa na kitambi unapelekea sana mifupa na jonits kusagika hasa eneo la magoti. Mwili unapokuwa mzito unaleta mgandamizo mkubwa eneo la joint na kupelekea tatizo. Ni muhimu kuweka sawa uzito wako ili upunguze hatari ya mifupa kusagika.

2.Kisukari na mafuta mengi. Kisukari na mafuta mengi kwenye mwili yanaongeza hatari ya kututumka ama kuvimba viungo vya ndani na kwenye joints na hivo kuongeza hatari ya mifupa kusagika. Kuongezeka kwa sukari kunapelekea sumu kuongezeka na kuleta hatari kwenye maungio.

3.Kupungua kwa homoni ya estrogen baada ya kukoma hedhi: Estrogen ni kichocheo ama homoni inayosaidia kulinda mifupa na maungio ya mifupa. Mwanamke anapofikia umri wa kukoma hedhi, kichocheo hiki kinapungua uzalishaji wake na hivo kuongeza hatari ya tatizo.

4.Magonjwa ya kurithi: Baadhi ya watu wanaweza kuugua magonjwa ya mifupa kwa kurithi kutoka kwa mababu. Hili ni ngumu kuepukika.

Je nitajuaje kama nina tatizo la mifupa kusagika?

Tofauti na magonjwa mengine ya joints, tatizo la osteoarthritis linaanza kukutafuna taratibu na kuchukua mika mingi mpaka kujionesha. Linaongezeka zaidi kutokana na kazi unazofanya na namna unavoshugulisha zaidi mwili kwako mfano kutembea na kukimbia. Hali ya maumivu na kuvimba kwenye maungio pia kunaongezeka siku hadi siku.

Kusagika kwa mifupa haisababishi wekundu kwenye kiungo kama ilivyo kwa baridi yabisi.

Unapoenda hospital daktari atachukua historia yako ya kuumwa na dalili unazopata. Anaweza kukufanyia kipimo cha X ray na MRI endapo ataona inafaa zaidi. Kama maungio yako yamejaa maji, daktari anaweza kuamua kufyonza maji yaliyopo .