Dawa ya Flagyl au Metronidazole

dawa ya metronidazole
metronidazole au flagyl

Dawa ya flagyl au metronidazole ni antibiotic, kwa maana ya dawa inayopambana na na vimelea wa bakteria. Metronidazole kwa jina lingine flagyl inafanya kazi kwa kuzuia ukuaji wa bakteria kupita kiasi. Dawa hii inatumika kutibu baadhi tu ya maambukizi ya bakteria. Haitumiki kutibu magonjwa ya virusi.

Kutumia antibiotic pale isipohitajika ni hatari kwa afya yako. Ni tabia mbaya kujinunulia dawa famasi na kuanza kumeza bila kushauriwa na daktari. Metronidazole pia yaweza kutumika pamoja na dawa zingine kutibu baadhi ya magonjwa ya tumbo kama vidonda vya tumbo vilivyosababishwa na bakteria wa H. pylori

atOptions = { 'key' : 'bc224a96d104b51eec13c7a0704a5aa2', 'format' : 'iframe', 'height' : 250, 'width' : 300, 'params' : {} }; document.write('');

Meza dawa hii kwa maji kama ulivyoelekezwa na daktari hospitali. Kuepusha tumbo kuvurugika meza dawa hii baada ya kula au kunywa maji au maziwa glass moja. Kumbuka dozi yako itategemea na hali ya ugonjwa unaokusumbua.

Kupata matokeo mazuri zaidi, yatakiwa kutumia antibiotic katika mwenendo wa masaa yale yale kila siku. Mfano saa 2 asubuhi kila siku. Endelea kutumia dozi yako mpaka umalize, hata kama umepata nafuu mapema. Kukatisha dozi ni hatari kwani itafanya bakteria kurudi tena na kushambulia kwa kasi.

Kizunguzungu, kichwa kuuma , tumbo kuvurugika, kichefuchefu, kutapika, kukosa hamu ya kula, kuharisha, choo kigumu na mdomo kuwa mchungu ni dalili za kawaida kuzipata ukiwa kwenye dozi ya metronidazole. Kama mojawapo ya dalili hizi itakuwa mbaya zaidi, muone daktari mapema kwa usaidizi.

Dawa hizi pia zinaweza kufanya mkojo kuwa mchafu ama brown. Dalili hizi wala isikupe hofu, kwasababu itaisha haraka ukishamaliza dozi.

Kumbuka kwamba daktari amekupatia dawa hii kwasababu amepima na kuona madhara ni madogo kuliko faida utakazopata. Watu wengi hawapati madhara baada ya kutumia metronidazole.

Lini yatakiwa kumwona daktari

Mjulishe daktari mapema endapo umeanza kupata dalili kama maambukizi kwenye koo yasiyoisha, homa kali, kutokwa damu, maumivu makali ya tumbo na maumivu wakati wa kukojoa.

Nenda hospitali haraka endapo umeanza kupata hali ya kusahau, kubadilika kwa mood, kukosa fahamu, kushindwa kuzungumza. Kupungua uwezo wa macho kuona na kuetetemeka kwa miguu na mikono. Hizi siyo dalili nzuri na zinahitaji huduma ya kitabibu mapema.

Dawa ya flagyl yaweza kuleta fangasi na aleji

Kutumia metronidazole kwa muda mrefu inaweza kupelekea fangasi mdomoni. Muone daktari mapema kama utaona utando mweupe mdomoni na mabadiliko ya uteute ukeni.

Wagonjwa wachache mno wanaweza kupata aleji baada ya kutumia metronidazole. Baadhi ya dalili kama muwasho wa ngozi na kuvimba uso, ulimi au koo na kukosa usingizi ni dalili za aleji.

Makala hii inaweza isiandike dalili zote mbaya unazoweza kuzipata. Ni muhimu kwako kufatilia mwili na kama utagundua dalili mbaya zaidi, rudi hospitali upate huduma.

Tahadhari unapotumia Dawa ya flagyl

Kabla ya kuanza kumeza metronidazole, mjulishe daktari au nesi anayekuhudumia kama una aleji na dawa au una aleji yoyote. Dawa hii inaweza kuwa na viambata vinavyosababisha aleji.

Kabla ya kuanza kutumia metronidazole, mjulishe daktari historia yako ya magonjwa. Hasa kama unaugua ini, figo na magonjwa ya damu.

Pumzika kutumia pombe na bangi

Usitumie pombe wakati unaendelea na dozi ya metronidazole. Kutumia dawa na pombe zenye viambata vya propylene glycol, itachochea dalili mbaya za kutapika, maumivu ya kuchwa na kichefuchefu. Subiri mpaka siku tatu baada ya kumaliza dozi ndipo uanze kunywa pombe.

Dawa hii itakufanya uwe na kizunguzungu. Kutumia pombe na bangi kunachochea zaidi tatizo. Usiende gari wala chombo chochote cha moto wakati upo kwenye dozi ya metronidazole. Mjulishe pia daktari kama unatumiaga bangi.

Dawa ya metronidazole na Ufanisi wa chanjo na upasuaji

Matronidazole inaweza kupunguza ufanisi wa chanjo hasa chanjo ya taifodi. Usipate chanjo wakati unatumia metronidazole.

Kabla ya upasuaji, mjulishe pia daktari kama unatumia metronidazole ama dawa zozote zingine ikiwemo tiba asili.

Wakati wa ujauzito dawa itumike tu pale penye ulazima.

Dawa hii hupita mpaka kwenye maziwa ya mtoto. Kama unanyonyesha, inabidi umujulishe daktari mapema kabla ya kuanza dozi.

Muhimu

Usichangie dozi ya metronidazole na mtu mwingine. Wala usitumie dawa zilizoachwa na mgonjwa mwingine.

Kama unatibiwa kwa magonjwa ya zinaa, hakikisha na mpenzi wako ametibiwa. Itakusaidia usipate maambukizi mengine kwa haraka. Wakati wa tiba epuka kufanya ngono ama utumie kondomu kwa kila tendo.

Dawa hii umepewa kwa changamoto yako ya sasa. Baada ya kupona kama dawa zimebaki zitupe, na usitumie kabisa tena kwa wakati ujao.

Bofya kusoma kuhusu: Kaswende sugu na hatua za kufuata ili upone

One reply on “Dawa ya Flagyl au Metronidazole”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *