Categories
Afya ya mwanamke na uzazi

Dalili Mbaya Kwa Mjamzito

dalili mbaya kwa mjamzito
mjamzito

Kipindi cha ujauzito kinaambatana na mabadiliko mengi sana ya mwili, pamoja na mabadiliko ya kimaisha pia kwenye kujiandaa kumpokea mwanafamilia mpya. Ni kipindi pia ambacho waweza kuwa na hofu sana kuhusu mimba yako, na utakuwa mwangalifu sana. Hapa chini ni maelezo a kina juu ya dalili mbaya kwa mjamzito na hatua za kuchukua mapema.

Mabadiliko mengi ambayo utayaona mwilini mwako, jua kwamba ni kawaida na ni lazima uyapitie. Dalili nyingi mfano kuumwa nyonga, tumbo kuunguruma, kukosa choo, kizunguzungu nk zinakuja na kupotea.

Je dalili mbaya zinaisha mapema?

Baadhi ya dalili waweza kukaa nazo mpaka siku unajifungua, na kuna zingine zinakuja na kupotea. Hapo ndipo yatakiwa kuwa makini kwa kila dalili unazopata. Kuna dalili zingine hatari ambazo haitakiwi upitishe hata siku 1 bila kwenda hospital, endapo utaziona.

Dalili za Kawaida Ambazo siyo hatarishi

Dalili nyingi kati ya hizi siyo hatari, na haitakiwi kupata hofu sana. Japo unaruhusiwa kumpigia daktari wako na kumuuliza ili upate uhakika zaidi. Dalili nyingi ya hizi zinajitokeza mimba ikiwa changa, na zingine baadae

  • kutapika
  • kutokwa na uchafu mwingi ukeni
  • kichwa kuuma
  • uchofu na kizunguzungu
  • maumivu yanayokuja kwa haraka na kupotea
  • kupungua uzito
  • kuhisi joto kali
  • kushindwa kuvuta hewa vizuri
  • mawazo, na kupata hofu ana kushindwa kufanya kazi zako vizuri

Dalili mbaya kwa mjamzito.

Dalili hizi zinatokea mda wowote wa ujauzito. Japo mimba inapokuwa changa zaidi ndipo hatari ya mimba kuharibika inakuwa kubwa, ila watakiwa kuwa makini kipindi chote.

Dalili hatarishi ni pamoja na

1.Kuvuja damu

Kitendo cha kutokwa damu/bleed ukiwa na mimba siyo ishara nzuri hata kidogo, ni kiashiria kwamba kuna tatizo. ikiwa unatokwa damu nzito, na una maumivu makali ya tumbo upande wa kushoto au kulia na unajihisi kuishiwa nguvu, hii inaweza kuashiria mimba imetunga nje ya kizazi.

Mimba ikitunga nje ya kiazi haiwezi kukua, inatakiwa kuondolewa ma[pema kwa upasuaji. Mimba hiozi huitwa ecopic, endapo haitaondolewa mapema, mgonjwa anaweza kupoteza maisha.

Kama damu zinatoka nzito, tumbo linauma kuzunguka kitovu, hii inaashiria mimba imeharbika, na hii inatokea zaidi mimba ikiwa chini ya wiki 12. Sisemi kwamba mimba kubwa kubwa haziharbiki, hapana. Ni kwamba mimba nyingi zinaharbika zikiwa changa.

2.Kutapika na kichefuchefu kupita kiasi

Kwa mjamzito ni kawaida kupata kichefuchefu, lakini kama tatizo ni kubwa inaweza kuashiria shida kubwa ya kiafya. Kama unashindwa mpaka kula au kunywa chochote, hapo utaishiwa maji. Na kuishiwa maji inaweza kuhatarisha ujauzito wako.

Kama unahisi kizunguzungu kinakutesa sana, ongea na daktari atakupa dawa ya kupunguza makali yake.

3.Mtoto kuacha kucheza

Mtoto kupunguza kucheza inaweza kuashiria kachoka, hii ni kawaida isikupe hofu. ila kama hachezi kabisa kwa siku nzima, hapo kuna shida kubwa.

Sasa ili kugundua tatizo, inashauriwa ukiona mtoto hachezi mda mefu, jaribu unywe kitu cha baridi. Kisha lala kwa ubavu, na fatilia kama mtoto ataanza kucheza.

Mpigie daktari, ama nenda hospital haraka endapo utagundua mtoto ameacha kucheza. Daktari atafanya vipimo kuona kama kuna hatari yoyote.

4.Kupata uchungu mapema mimba ya miezi 7

Kupata uchungu na mimba haijatimiza umri wa kujifungua, ni dalili mbaya. Kama tumbo linavuta na kuachia na hii hali itokee mara chache na kuisha hilo ni kawaida. Kwani hata ukifika kileleni baada ya tendo, lazima utahisi tumbo kuvuta.

Lakini endapo tumbo linavuta na kuachia, kisha baada ya dakika 10 linaanza tena kuvuta na kuachia, hiyo ni ishara ya kuelekea kuzaa njiti. Mpigie daktari mapema endapo utaona hali hii.

5.Chupa kupasuka mapema ni dalili mbaya kwa mjamzito

Tunaposema chupa, tunamaanisha ule mfuko unaobeba mtoto. Mfuko huu unakuwa na maji yanayomlinda mtoto asiumie. Mfuko unapasuka pale mama akianza uchungu na yupo tayari kujifungua. Endapo mfuko utapasuka mapema na mtoto akaendelea kubaki tumboni, mtoto atakosa hewa na kupoteza uhai.

Maji haya ni tofauti na mkojo, kwani hayaishi mapema yakianza kuvuja. Kwahivo tazama ukiona dalili ya kuvuja maji ukeni, tena maji mengi, nenda hospitali haraka.

6.Maumivu makali yasiyoisha kwenye kichwa, tumbo na kushindwa kuona vizuri

Hizi dalili zinaweza kuashiri kupanda kwa presha kitaalamu (preeclampsia) . Hili ni tatizo baya na linaweza kupelekea kifafa cha mimba. Tatizo linaambatana na dalili za presha kupanda na protini nyingi kwenye mkojo, hasa inatokea baada ya week 20 za ujauzito. Hakikisha unaenda hospital haraka endapo unahisi dalili hizo.

Nawezaje kujizuia nisipate dalili mbaya kwa ujauzito wangu?

Ukweli ni kwamba ni vigumu sana kujizuia asilimia zote kupata dalili mbaya kwenye ujauzito. Lakini kuna vitu vichache unaweza kufanya kupunguza hatari ya mimba kuharibika kabla ya muda wake.

Hudhuria clinic zote na upate dawa za kuongeza damu mapema kabisa. Unapoenda clinic daktari atachukua historia yako na kukwambia endapo upo kwenye kundi hatarishi. Utapewa ushauri wa kina kuhusu lishe na afya ya akili pamoja na afya ya tendo la ndoa.

Bofya kusoma kuhusu kifafa cha mimba

4 replies on “Dalili Mbaya Kwa Mjamzito”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *