Hedhi Nzito ya Mabonge

hedhi nzito

hedhi nzito

Kwanini Hedhi yangu ni nzito sana? Hedhi nzito sana yenye mabonge kitaalamu huitwa menorrhagia. Wanawake wengi sana wanapatwa na shida hii.

Hedhi inachukua siku nyingi zaidi ya siku 5 na inakuwa nzito ikiambatana na maumivu makali sana, kitu ambacho kiafya siyo salama. Ukiwa na tatizo hili waweza kubadilisha pedi kila baada ya saa 1 kwatika siku nzima.

Na pia maumivu ya tumbo na kiuno yatakuwa makali sana kiasi ya kushindwa kufanya shughuli zako.

Kama unapatwa na shida hii tambua kwamba siyo jambo la kawaida na waweza kuwa na shida ingine kubwa ya kiafya ambayo ndio chanzo. Muhimu umuone daktari mapema upate vipimo na tiba kabisa.

Dalili Zingine Zinazoambatana na Hedhi Nzito

Baadhi ya wanawake kupata hedhi nzito yaweza kuwa ni tatizo la muda mrefu tangu walipoanza hedhi. Kwa wengine tatizo huanza baada ya miaka mingi kupita tangu hedhi ya kwanza.

Kwa vyovyote vile kumbuka ni muhimu umuone daktari na uzungumze nae kuhusu shida yako ya hedhi nzito, hasa kama tatizo ni jipya kwako hujalizoea. Hedhi nzito sana yaweza kupelekea ukapungukiwa na damu na kukufanya kuwa mdhaifu.

Wanawake wenye tatizo hili la menorrhagia hukutana na mambo haya wakati wa hedhi yao

  • kubadili pedi kila baada ya saa
  • kubadili pedi usiku
  • kuvaa pedi mbili ili kudhibiti damu nyingi sana inayotoka
  • kuacha kufanya baadhi ya kazi zao kwasababu ya maumivu makali
  • hedhi inaweza kuchukua zaidi ya siku 7
  • mwili kuchoka sana
  • kupata damu ya hedhi katikati ya mzunguko

Chanzo Cha Hedhi nzito ya inayochukua Siku Nyingi

Sababu kuu za hedhi nzito ni pamoja na

Kuvurugika kwa homoni

Kila mwezi kwenye kizazi ukuta hujijenga ili kujiandaa kwa ajili ya kupokea kiumbe kitakachozaliswa kama yai itarutubishwa na mbegu ya kiume. Pale inapotoea yai halijarutubishwa ndipo ukuta huu unabomoka na kutolewa kama hedhi.

Endapo homoni/vichocheo vimevurugika inasababisha ukuta unaojengwa kuwa mnene zaidi na kutoa mabonge ya damu wakati wa kubomoka. Kama mayai yanayozalishwa hayatatolewa(ovulation) ni sababu pia ya kuvurugika kwa homoni.

Uvimbe kwenye tumbo la uzazi(uterus)

Uvimbe wowote kwenye kizazi kwa majina fibroids ama polyps ni chanzo cha kupata hedhi nzito.

Matumizi ya kitanzi

Wanawake wengi sana wanapendelea kutumia kitanzi kupanga uzazi. Kama unatumia kitanzi na wapata hedhi nzito basi fahamu hiki ndipo chanzo cha tatizo lako

Mimba kutungwa Nje ya Kizazi(ectopic pregnancy)

Katika hali isiyo ya kawaida na inayotokea mara chache sana , baada ya mbegu za yai kukutana, kiumbe kinachozalishwa chaweza kujishikiza nje ya tumbo la uzazi.

Hii yaweza kupelekea matatizo makubwa ya uzazi kama kutokwa damu nyingi sana ambayo damu hii unaweza kufikiri ni ya hedhi kumbe siyo. Mimba kuharibika pia yaweza kusababisha mwanamke atokwe na damu nyingi kupita kiasi.

Saratani

Saratani ya shingo ya kizazi ama kwa alugha rahisi saratani ya kizazi inaweza kupelelekea upate kuvuja damu nyingi, damu hii waweza kufikiri ni hedhi lakini siyo hedhi.

Matumizi ya dawa

Baadhi ya dawa hasa za kupunguza damu kuganda (blood thinners) kama asprini zinaweza kuwa chanzo cha hedhi nzito

Magonjwa mengine pia yanachangia upate hedhi nzito: Magonjwa haya ni kama

  • endometriosis(kukua kupita kiasi kwa ukuta wa ndani wa kizazi)
  • matatizo ya tezi ya shingoni kama goiter
  • maambukizi kwenye kizazi (PID)
  • magonjwa ya figo
  • magonjwa ya ini

Daktari atafahamu vipi kama una tatizo la hedhi nzito

Unapoenda hospitali daktari atakuuluza historia ya ugonjwa wako na dalili unazopata. Daktari anaweza kuagiza ufanyiwe vipimo vya damu, utrasound na kipimo cha kizazi kuona kama una saratani (pap smear test).

Pia daktari anaweza kuchukua sampuli ndogo ya nyama kwenye kizazi na kupeleka maabara kwa ajili ya vipimo zaidi.

Tiba kwa tatizo hili la kutokwa hedhi nzito na nyingi

Unapoenda hospitali tegemea kupata tiba kati ya hizi.

Vidonge vya kuanga uzazi(birth control pills): Vidonge vya uzazi wa mpango vitabadili mpangilio wa homoni na kukata damu ya hedhi isiendelee kutoka.

Upasuaji: Endapo itagundulikwa kwamba chanzo cha kupata damu nyingi ni uvimbe kwenye kizazi basi tegema kwamba utafanyiwa upasuaji kuondoa hizo vimbe ndipo hedhi itakoma kutoka nyingi na nzito.

Kuondolewa kizazi chote(hysterectomy):Kama changamoto yako ni kubwa sana na inapelekea kupoteza damu nyingi daktari anaweza kushauri ufanyiwe upasuaji kuodoa kizaiz chote. Baada ya upasuaji huu, hutaweza kushika mimba tena na pia hutapata tena hedhi.

Madhara ya tatizo la hedhi nzito sana

Kutokwa na damu nyingi sana kunaweza kupelekea ukapata changamoto zingine kama

  • kupoteza damu nyingi(anemia)
  • kupungukiwa na madini chuma
  • mwili kukosa nguvu na uchovu sana
  • maumivu makali ya tumbo na kiuno

Tumia Evecare kurekebisha hedhi yako

Tiba ya hedhi kuvurugika

Evecare ni dawa asili na imetengenezwa nchini India kupitia mimea ya Ashoka, Asaparagus na lodh tree. Kwa miaka zaidi ya mitano ambayo tumekuwa tukihudumia wagonjwa wetu wa matatizo ya hedhi na homoni, tumepokea shuhuda lukuki. Evecare inakuwa na vidonge 30, unameza vidonge viwili kila siku kwa muda wa wiki mbili

Baada ya kutumia Evecare tegemea kupata matokeo haya

  • Hedhi kutoka vizuri na nyepesi kwa siku chache siyo zaidi ya siku 4 ama 5
  • Maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi kuisha kabisa
  • Homoni kubalansi
  • Mzunguko wa hedhi kurekebika na kuanza kupata kila mwezi
  • Kizazi kuimarika sana hata kuongeza chansi ya kushika mimba kama wewe ni muhanga wa kukosa mimba kwa muda mrefu.

Bei ya Evecare ni Tsh 75,000/= Tunapatikana Dar, Magomeni.

Angalizo

Kuna wimbi kubwa la wajasiliamali mitandaoni wanauza vidonge fake vya evecare, tena wanauza kwa bei rahisi sana. Watu hao siyo madaktari wala siyo wataalamu wa afya na wanauza bidhaa feki ambazo ni hatari wa afya yako. Wengi wao hawana hata ofisi, ukipata madhara unakosa pa kuuliza. Kuwa makini na watu hao, wamejaa sana insta na fb.

Chati na daktari kwa whatsapp no. 0678626254 kuanza tiba.

Bofya kusoma makala inayofuata: Hatua za kupunguza maumivu kipindi cha hedhi

3 replies on “Hedhi Nzito ya Mabonge”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *