Kitendo cha kubanwa pumzi ni pale unaposhindwa kuvuta hewa safi kuelekea kwenye mapafu yako. Tatizo hili kitaalamu linaitwa dyspnea, na linaweza kuashiria uwepo wa changamoto kubwa ya kiafya.
Kwa mtu mzima, anavuta hewa ndani na kutoa nje walau mara 20 kwa kila dakika. Hii ni kama pumzi 30,000 kwa siku nzima. Kwa wale watu wa mazoezi hali inaweza kuongezeka zaidi maana uhitaji wa hewa safi huongezeka.
Dalili za kubanwa pumzi
Ukiwa na changamoyo ya kubanwa pumzi yani dyspnea utapata dalili za
- kushindwa kuvuta hewa
- kifua kubana na
- kupata kiu ya kuhitaji hewa
Kubanwa pumzi inaweza kuchukua muda mfupi (acute) ama ikachukua muda mrefu kuisha(chronic). Kukosa pumzi kwa muda mfupi huambatana na dalili zingine kama homa na kikohozi. Kukosa pumzi kwa muda mrefu inaweza kukufanya kubanwa na kifua kila siku ukiwa kwenye shuguhuli zako.
Wakati mwingine changamoto ya kukosa pumzi inaweza kupungua ama kuongezeka zaidi kulingana na ukaaji wako. Mfano, kulala chali kunaweza kupelekea kubanwa pumzi kwa wenye magonjwa ya moyo na mapafu. Muhimu kufatilia dalili unazopata na kumweleza daktari ili akupe tiba sahihi.
Nini chanzo cha kubanwa pumzi?
Pengine unajiuliza sana nini chanzo mpaka mtu akose pumzi? Changamoto nyingi zinaweza kupelekea ukakosa pumzi kwa kipindi cha muda mfupi (acute dyspnea). Sababu hizi zinazochangia ni pamoja na
- wasiwasi na hofu
- pumu
- kuganda kwa damu kwenye mishipa ya damu ya mapafu
- kuvunjika ubavu
- ujaa maji kwenye mazingira ya moyo
- kukohoa sana
- shambulizo la moyo
Sababu zingine ni
- moyo kufeli kusukuma damu
- mabadiliko ya mapigo ya moyo
- maambukizi kwenye mapafu yanayopelekea nimonia
- kuwa mjamzito
- aleji na
- kupungukiwa damu kwa haraka
Kwenye upande wa kukosa pumzi kila mara kwa muda wa miezi kadhaa, sababu hizi zinaweza kuchangia
- majimaji kwenye mapafu
- pumu
- uzito mkubwa na kitambi
- magonjwa ya moyo
- presha ya kupanda kwenye mpafu (pulmonary hypertension)
- makovu kwenye mapafu
- kuvimba kwa misuli ya moyo (cardiomyopathy)
Changamoto zingine kama saratani ya mapafu na kifua kikuu, vinaweza kukufanya ukose pumzi. Kama una tatizo hili na hujui chanzo chake, tafadhali nenda hospitali haraka upate huduma. Daktari ataweza kukusikiliza na kupendekeza baadhi ya vipimo.
Vipimo kwa changamoto ya kubanwa pumzi
Daktari atakusikiliza vizuri dalili unazopata na kucheki hali ya mapafu yako. Unaweza kupimwa kipimo cha mapafu kinachoitwa spirometry, kucheki kiwango cha hewa kinachoingia ndani na kutoka nje ya mapafu, na kwa kasi ya kiasi gani. Kipimo kitasaidia kujua kama una pumu ama njia za hewa zimevimba.
Vipimo vingine unavyoweza kufanyiwa ni pamoja na
Pulse oximetry: daktari anabana kitu kwenye kidole au sikio kupima kiwango cha hewa ya oksijeni kwenye damu.
Kipimo cha damu: kitagundua kama una upungufu wa damu ama maambukizi yoyote au damu kuganda.
X-rays au CT scan: vipimo hivi vinaweza kuonesha kama una nimonia ama magonjwa mengine ya mapafu.
ECG: kipimo cha moyo kucheki mapigo ya moyo na kama una shambulii la moyo.
Tiba ya kubanwa na pumzi
Mazoezi ya kuvuta hewa na kutoa nje yanaweza kusaidia mgonjwa wa changamoto hii. Lakini kwa kiasi kikubwa tiba yako itategemea na chanzo cha tatizo. Mfano kama una pumu, itahitaji upate kifaa cha kukusaidia (inhaler) kila unapobanwa na pumzi.
Kama kuna maji kwenye mapafu, daktari atahitaji kuyafonza. Kama ni maambukizi au damu imeganda utahitaji dawa. Wakati mwingine utahitaji kuwekwa kwenye mshine ya oxygen.
Lini unatakiwa kumwona daktari?
Kitendo cha kukosa pumzi, siyo cha kupuuza haa kidogo. Nenda hospitali mapema endapo kukosa kwako pumzi kunaambatana na dalili hizi
- kuvimba miguu na enka
- kushindwa kupumua unapolala chali
- homa kali na kukohoa
- kutoa sauti ya filimbi