UTI ni maambukizi ya bakteria kwenye njia ya mkojo. Tukisema njia ya mkojo tunamaanisha kuanzia kwenye uke, kibofu, mirija ya kibofu na figo.Makala yetu itaaangazia kwa kina sababu za kuugua UTI baada ya tendo la ndoa.
UTI inawezaje Kuambukizwa
Japo mkojo wako hauna bakteria lakini bakteria waliopo maeneo ya uke wanaweza kupenya kwenye mfumo wa mkojo na kukufanya uumwe. Bakteria hawa wanaposhambulia njia ya mkojo ndio kwa kifupi tunasema UTI.
Kuna sababu nyingi zapelekea upate UTI ikiwemo tendo la ndoa. Tutajifunza zaidi vitu gani waweza kufanya upunguze hatari ya kuugua UTI baada ya kumaliza tendo la ndoa. Utajifunza pia vihatarishi vingine ukiacha tendo la ndoa.
Je Unaweza Kuugua UTI baada ya Tendo La Ndoa?
Jibu ni ndio, unaweza kuugua UTI kwa kufanya tendo la ndoa, hasa kwa mwanamke.
Wakati wa tendo la ndoa zile purukushani za kuingiza uume na kutoa na msuguano unaotokea unaweza kupelekea bakteria kuinginzwa kwenye njia ya mkojo.
Ukaribu wa njia ya mkojo na mkundu wa mwanamke unafanya urahisi wa kusafiri kwa bakteria wa E. coli ambao ndio husababisha UTI.
Unaweza Kuugua UTI Kupitia ngono ya mdomo pia
Ni muhimu kuweka akilini pia kwamba unaweza kuuugua UTI kwa kufanya ngono kwa mdomo(oral sex). Kitendo cha mwanume kunyonya au kulamba uke kinaweza pia kuhamisha bakteria hawa na kuwapelekea kwenye njia ya mkojo.
Namna gani upunguze hatari ya Kuuugua UTI baada ya tendo la ndoa?
Japo ni ngumu kujizuia asilimia mia, kuna baadhi ya hatua ukizingatia zitakusaidia kuepuka kuugua UTI bada yatendo la ndoa. Hizi ndizo hatua zenyewe
- Siku zote bada ya kumaliza tendo hakikisha unaenda kukojoa ili kuwasukuma nje bakteria wote ambao walishaanza kusafiri kwenda kwenye kibofu kuleta madhara.
- Hakikisha pia unakojoa kabla ya kuanza tendo
- Osha nyeti zako kwa maji ya uvuguvugu kabla ya tendo kusaidia kupunguza hatari ya kuugua UTI
- Kuwa mwangalifu kabla hujaanza kutumia baadhi ya njia za uzazi wa mpango kama kitanzi maana zinaongeza hatari ya kuugua UTI
Kama unaugua sana UTI mara kwa mara daktari anaweza kushauri umeze dawa za antibiotics kila unapomaliza tendo. Hakikisha usizeme dawa hizi bila ushauri wa daktari kwani zaweza kufaya mwili ukawa sugu.
Je kuna Watu walio kwenye hatari zaidi ya Kuugua UTI?
Japo kila mtu anaweza kuugua UTI ila tafiti zinasema kwamba wanawake wapo kwenye hatari zaidi mara nane kuugua kuliko wanaume. Wanawake walikomoma hedhi na wakavu sana ukeni pia wapo kwenye hatari zaidi.
Sababu zingine zinazoongeza hatari ya kuugua UTI ni pamoja na
- kufanya tendo kwa nguvu mara kwa mara
- kufanya tendo na wanaume tofauti tofauti
- kushika mimba haraka haraka
- uzito mkubwa na kitambi
- kisukari
- kupungua kwa kinga ya mwili
- kuwa na maumbile yasiyo ya kawaida sehemu za siri
Ni zipi dalili za UTI
Baadhi ya dalili kubwa za UTI ni pamoja na
- kupata hamu ya kukojoa mara kwa mara
- maumivu wakati wa kukojoa
- kuhisi kitu kizito chini ya kitovu
- damu kwenye mkojo
- mkojo kuwa na rangi ya wingu na wenye harufu mbaya
- maumivu mkunduni kwa wanaume
Kwa kulingana na ukubwa wa tatizo unaweza pia kupata dalili kama maumivu ya mgongo na tumbo kushoto au kulia. Hii itakuwa ni kiashiria kwamba maambukizi yamesambaa mpaka kwenye kibofu. Daili zingine unaweza kupata ni pamoja na kichefuchefu, kutapika na homa kali
Sababu zingine zinazopelekea mtu kuugua UTI ni pamoja na
Matatizo kwenye kibofu kushindwa kutoa mkojo wote, kuziba kwa njia za mkojo kutokana na mawe ya figo na kukua kwa tezi dume, matumizi ya catheter na matumizi ya mara kwa mara ya antibiotics na hivo kuvuruga mazingira ya njia ya mkojo.
Lini unatakiwa Kumwona Daktari
Kama unapata dalili hapo juu, hakikisha unatembela hospitali ya karibu yako uonane na daktari kupata vipimo na tiba.
Matibabu ya UTI
Kwa wagonjwa wengi tiba kubwa ni antibiotics. Kwa ajili ya kupunguza dalili kama maumivu daktari anaweza kukupatia pia dawa za maumivu.
Namna gani Ujikinge na Kuugua kwa UTI mara kwa mara
Ukiacha swala la dawa fuata ushauri huu ili kuzuia usiugue UTI tena
- kunywa maji ya kutosha kila siku kila unapopata kiu
- kwa wanawake hakikisha unakojoa kabla na baada ya tendo la ndoa
- kwa wanawake tena hakikisha unajisafisha kutoka mbele kwenda nyuma
- kuwa msafi kwenye eneo la siri
- usitumie marashi au sabuni ukeni
- usivae jeans na chupi za kubana sana
4 replies on “Kwanini Unaugua UTI Baada ya Tendo la ndoa”
Nashkru sana kwa ushauri wenu mzur natamn kuonana na nyie
Nawezaje kuonana na nyie jamn Nina mda mrefu sijazaaa
Karibu tuandikie kwa whatsapp namba 0678626254 kupata huduma ya tiba.
Matibabu ya punyeto