Majibu ya maswali yako kuhusu maziwa ya mama
Maziwa ya mama yamejaa virutubishi vya kutosha kwa ajili ya mtoto anayezaliwa. Tafiti zinaonesha kwamba maziwa ya mama siyo tu ya virutubishi vingi, bali kuna viambata vinavyokinga mwili wa mtoto dhidi ya magonjwa.
Ijapokuwa makampuni mbali mbali yamejaribu kutengeneza formula na lishe, lakini bado havikidhi vigezo kama maziwa ya mama. Maziwa ya mama yana viambata vingi muhimu kumkinga mtoto dhidi ya maambukizi, kuimarisha ukuaji wa viungo vya mwili na pia kuimarisha mfumo wake wa chakula.
Mtoto apate maziwa ya mama kwa zaidi ya mwaka na nusu
Kwasababu hizi mama alijejifungua anatakiwa kuelemishwa aendelee kunyonyesha mtoto bila kmpa chakula chochote kwa miezi sita. Na kuendelea kumnyonyesha mtoto zaidi ya mwaka mmoja na nusu.
Wamama wengi najua wanajiuliza maswali mengi sana kuhusu swala la kunyonyesha. Hivo nimewaandalia majibu sahihi kwa maswali yote yanayokutatiza kuhusu kunyonyesha.
Maswali nane yanayoulizwa zaidi kuhusu kunyonyesha.
1.Kwa muda gani natakiwa kunyonyesha mtoto?
Kwa mujibu wa wizara ya afya, mama anatakiwa kunyonyesha kwa miezi sita bila kumpa mtoto chakula chochote. Na baada ya hapo kuendelea kunyonyesha kwa miaka miwili au zaidi. Tafiti zinasema kwamba kunyonyesha kwa muda mrefu kunapunguza hatari ya mtoto kuugua magonjwa ya ubongo na neva, pia kinga ya mtoto inaimarika zaidi.
2.Natakiwa kula nini ili maziwa ya mama yawe na virutubishi vya kutosha?
Tafiti zinasema kwamba ubora wa maziwa ya mama unategemea na aina ya chakula anachokula. Kula zaidi vyakula vyenye mafuta ya omega-3 kama mbegu za chia, ufuta, samaki wadogo na mayai. Punguza ulaji wa mafuta ya omega 6 kama nyama na maziwa.
3.Je watoto wanatakiwa kutumia virutubishi vya Vitamin?
Kikawaida watoto wadogo hupewa Vitamin K. Upungufu wa vitamin zingine kwa watoto ni nadra sana. Kwasababu kiwango cha vitamin kwenye vyakula inatofautiana, inashauriwa mama aendelee kutumivia virutubishi vya multivitamin kipindi cha kunyonyesha.
4.Nawezaje kutunza maziwa baada ya kukamua?
Wamama wengi walio bize na kazi, hupendelea kukamua maziwa na kisha kumnyonyesha mtoto bila uwepo wake. Ni kawaida kwa maziwa kuwa na utofauti wa rangi na harufu kutokana na lishe anayopata mama. Utagundua pia kwamba maziwa ukishajikamua na kuyatunza, mafuta hujitenga juu. Hakikisha unazunguza chupa au kifaa chako taratibu mpaka maziwa yachanganyike.
Baada ya kujikamua, tunza maziwa kwenye friji ili yatumike muda ujazo. Endapo utatunza maziwa kwenye freeer, bakisha sehemu kidogo ya maziwa kutanuka kwenye chombo ulichohifadhai. Kabla ya kumnywesha mtoto maziwa, yapashe kidogo kwa dakika mbili.
5.Kwa muda gani naweza kutunza maziwa niliyojikamua?
Ni salama kutunza maziwa ya mama katika namna zifuatazo;
Katika joto la kawaida la chumba unaweza kutunza mpaka masaa sita.
Kama umetupia vipande kadhaa vya barafu kwenye chombo chako unaweza kutunza kwa msaa 24.
Kwenye friji yako unaweza kutunza kwa siku tatu. Kwenye freezer unaweza kutunza mpaka miezi miwili.
Kutunza maziwa kiusahihi hakuongezi hatari ya vimelea na bakteria kuvamia maziwa. japo kiwango cha virutubisho inaweza kupunga kidogo. Inashauriwa kwamba ili kutunza ubora wa virutubishi kwenye maziwa ya mama, usitunze maziwa zaidi ya siku mbili.
6.Naweza kupasha maziwa ya mama baada ya kuyatunza kwenye friji?
Maziwa ya mama usipashe kwenye microwave, inaweza kubadili ubora wa maziwa na kupelekea matone ya moto yanayoweza kumuunguza mtoto. Weka maziwa kwenye sufuria ndogo, kisha chemsha maji kwenye sufura nyingine. Weka sufuria ndogo yenye maziwa kwenye maji ya moto kisha subiri kwa muda kidogo mpaka yapate joto.
Kama ulitunza maziwa kwenye freezer, yatoe kisha yaache mpaka yayeyuke. Baada ya kuyeyuka ndipo unaweza kuyapasha.
7.Je pombe ina madhara kwenye maziwa ya mama?
Wamama wengi wanaweza kunywa pombe kidogo wakati wanaendelea kunyonyesha. Kama wewe ni mnywaji punguza kiwango cha pombe kwa kiasi kikubwa wakati wa kunyonyesha. Kama inawezekana uache kabisa mpaka umalize kunyonyesha.
8.Nawezaje kuongeza uzalishaji wa maziwa ya mama?
Wamama wengi wanaonyonyesha wanahofu kwamba pengine maziwa hayatoshelezi mahitaji ya mtoto na wanatafuta namna mbalimbali za kuongeza maziwa. Kuna vitu vingi ambavyo vinapunguza uzalishaji wa maziwa. Watakiwa kufahamu vitu hivyo kabla hujafikiria njia za kuongeza maziwa.
Jaribu kumyonyesha mtoto muda wote anapokuwa na njaa. Uhitaji zaidi wa maziwa utachochea mwili kuzalisha maziwa mengine zaidi. Tengeneza ratiba nzuri mtoto akiwa bado mchanga. Mnyonyeshe mtoto kila baada baada ya masaa mwili nyakati za mchana na unyonyeshe kila baada ya masaa manne nyakati za usiku. Na hakikisha unatumia matiti yote kwa kubadilisha.
Kunyonyeza huchochea uzalishaji wa maziwa
Kadiri mtoto anavyonyonya zaidi ndipo maziwa mengi zaidi yatazalishwa na mwili. Uchache wa maziwa unaweza kuchangiwa na mtoto kutopangwa vizuri ili anyonye inavotakiwa, pengine kutokana na usingizi mwingi au kuzoea maziwa ya chupa. Ongea na mtaalamu wa magonjwa ya watoto akushauri nana nzuri ya kunyonyesha.
Namna ingine ya kuongeza uzalishaji wa maziwa ni kuongeza kukamua maziwa, hasa kama mtoto wako hali chakula vizuri. Kamua maziwa mara mbili au tatu endapo unapanga kuwa mbali na mtoto.
Mwisho kabisa hakikisha unapata lishe nzuri. Kula chakula bora, jaribu kula makundi mbalimbali ya vyakula kila siku. Pendelea kula vyakula asili, epuka vilivyochakatwa kiwandani.