Depo- Provera au sindano ya depo ni jina la brand za sindano za uzazi wa mpango kuzuia mimba. Sindano inakuwa na homoni iliyotengenezwa maabara. Dawa ambayo inafanya kazi vizuri kuzuia mimba ndani ya miezi mitatu baada ya kuchoma.
Sindano za Uzazi wa mpango-depo inavyofanya kazi
Sindano ya depo inafanya kazi kwa kuzuia yai lisipevuke na kutolewa kwenye mfumo wa mayai(ovary). Bila mayai kupevuka mimba haiwezi kutungwa. Sindano pia inafanya uteute wa ukeni kuwa mzito sana na hivyo kuzuia mbegu kuogelea kwenda kurutubisha yai.
Kila sindano nguvu yake inaisha baada ya miezi mitatu. Baada ya hapo unatakiwa kwenda hospitali kuchoma sindano ingine ili usishike mimba isiyotarajiwa. Ni muhimu kufika hospitali mapema kabla nguvu ya sindano ya kwanza haijaisha.
Kuchelewa kuchoma sindano nyingine
Endapo hutachoma sindano mapema pengine kwa kuchelewa kwenda hospitali, unatakiwa kutumia njia ingine mbadala. Mfano kondom ili kuzuia usishike mimba wakati unajiandaa kwenda hospitali.
Haishauriwi kuchoma sindano zaidi ya miaka miwili, labda tu kama njia zingine za kupanga uzazi zimekukataa.
Matumizi ya Sindano ya depo
Kwanza kabisa daktari anatakiwa kuhakikisha kama ni salama kwako kupata sindano ya depo. Weka appointment na daktari ili upate sindano. Daktari atakuchoma sindano ya depo kwenye tako au eneo la juu la mkono, kokote unapopendelea
Endapo utachoma sindano siku tano baada ya kuanza hedhi ama siku tano baada ya kujifungua, tayari unakuwa umejikinga na uko salama kufanya tendo. Utahitaji kurudi hospitali kila baada ya miezi mitatu kupata sindano ingine. Kama miezi mitatu imeshapita, daktari atakupima kwanza mimba kabla ya kukuchoma sindano.
Ufanisi wa sindano ya depo ukoje?
Sindano ya uzazi wa mpango ya depo ina ufanisi wa asilimia 99 kuzuia mimba ndani ya miezi mitatu. Kwa maana hiyo kati ya wanawake 100 wanaochoma sindano, ni mwanamke mmoja tu anaweza kushika ujauzito kwa bahati mbaya.
Madhara/ matokeo ya sindano za uzazi wa mpango za depo
Wanawake wengi waliochoma sindano ya depo wanapata hedhi nyepesi. Hehdi yako inaweza kuoma kabisa endapo utaendelea kuchoma sindano kwa mwaka mzima. Wanawake wengine wanaweza kupata hedhi nzito sana na ya muda mrefu.
Madhara mengine yanayowapata wanawake wengi ni kama
- Kichwa kuuma
- Maumivu ya tumbo
- uchovu
- Kupungua kwa hamu ya tendo
- Kuongezeka uzito hasa ukitumia zaidi ya mwaka mmoja
Madhara yanayotokea kwa wanawake wachache ni pamoja na
- Kuota chunusi
- Tumbo kujaa
- Kutokwa jasho jingi hasa usiku
- Kukosa usingizi
- Maumivu ya joints
- Kichefuchefu
- Msongo wa mawazo na
- Kupoteza ubora wa nywele
Pia wanawake wanaotumia sindano za uzazi wa mango wanaweza kupata shida ya mifupa. Hii inatokea pale unapotumia kwa muda mrefu zaidi. Hali itatengemaa na mifupa kujengeka tena pale ukiacha kuchoma sindano. Daktari atapendekeza upate virutubishi vyenye madini ya calcium kwa wingi na vitamin D kulinda mifupa yako.
Je naweza kushika mimba baada ya kuacha kuchoma sindano?
Jibu ni ndio unaweza kushika mimba mapema ndani ya miezi mitatu au minne baada ya kuchoma sindano ya mwisho. Japo kwa baadhi ya wanawake inawachukua mpaka miezi 8 kushika mimba. Lakini baadhi ya wanawake huchelewa sana kushika mimba. Wachache huhitaji mpaka kutumia dawa za kupevusha mayai ya kusafisha kizazi ili kushika tena mimba.
Makundi gani hayakiwi kupata sindano ya depo?
Kila mwanamke ataruhusiwa kutumia sindano ya depo isipokuwa kama una matatizo haya
- Magonjwa ya ini
- Saratani ya matiti
- Kutokwa damu ukeni bila sababu ya msingi
- Tatizo la kuganda kwa damu
Madhara Makubwa ya Sindano za uzazi wa mpango
Japo madhara haya ni mara chache sana lakini yanaweza kujitokeza. Unatakuwa kwenda hospitali mapema endapo utaanza kuona dalili hizi wakati unatumia sindano ya depo.
- Sonona
- Usaha na maumivu eneo ulilochmwa sindano
- Ngozi kuwa ya njano
- Vimbe kwenye matiti na
- Maruweruwe (migraines)
Unatafuta mimba bila mafanikio baada ya kutumia sindano? ama unataka kurekebisha hedhi iliyovurugwa na sindano? Soma hapa.
Makundi machache ya wanawake hupata changamoto sana kushika mimba baada ya kuchoma sindano ya uzazi wa mpango. Kutokana na hali hiyo tulikuja na suluhisho kupitia dawa asili za mimea. Dawa hizi zimechakatwa na kuwekwa kwenye mfumo wa vidonge.
Ongea na Daktari
Endapo unataka kufahamu kuhusu njia zingine za kupana uzazi, zungumza na daktari wako. Atakusaidia kuchagua njia sahihi kulingana na afya yako.
Kwanini nakushauri kutumia Evecare kurekebisha homoni na hedhi?
Nakushari kutumia evecare kwasababu zitarekebisha homoni zako na uanze kupata hedhi vizuri. Pia kurudisha tena uwezo wako kushika mimba, uwezo uliopotea baada ya kutumia sindano ya depo.
Baada ya kutumia Evecare, tegemea haya
- Hedhi kurudi kuwa vizuri
- Homoni kurekebika
- Kupata tena uteute wa kuvutika kwenye siku za hatari
- Kurejesha hamu ya tendo la ndoa ilopotea kutokana na sindano za uzazi wa mpango.
Angalizo
Kuna wimbi kubwa la wajasiliamali mitandaoni wanauza vidonge fake vya evecare, tena wanauza kwa bei rahisi sana. Watu hao siyo madaktari wala siyo wataalamu wa afya na wanauza bidhaa feki ambazo ni hatari wa afya yako. Wengi wao hawana hata ofisi, ukipata madhara unakosa pa kuuliza. Kuwa makini na watu hao, wamejaa sana insta na fb
15 replies on “Sindano za uzazi wa mpango-Depo”
Kama naumwa na kichwa tiba n gan?
Nini chanzo cha kichwa chako kuuma?? yatakiwa kutambua kwanza chanzo cha tatizo
Tumbo linajaa na maumivu mpaka kushindwa kutembea ila period sipati
Tafadhali tupigie kwa namba zetu 0678626254 upate msaada wa haraka
unatakiwa kukaa mda gan kukutana na mwanaume baada ya kuchoma sindano iyo?
kama umechomwa wakati wa hedhi hakuna muda wa kusubiri, lakini kama umechomwa kipindi kingine basi subiri walau siku 10 ndipo uanze kufanya tendo
Dozi Sindano inapoisha yaani miezi mitatu uliyochoma ikiisha inachukua muda gani mwanamke kufanya tendo na kutopata Ujauzito?
Muda wowote anaweza kushika mimba endapo matumizi ya sindano yamefikia kikomo
jaman mm nimechom depo mwezi wa 6 lakn damu zimegoma kukata na titi lina jipu alf nanyonyesha ni wiki ya 2 sasa tangu nipatwe ili jipu msaada jaman nateseka
unatakiwa kwenda hospital haraka upewe dawa ya kukata hii damu
Nimetumia shindano ya miezi tatu miaka nane na nimewacha mwezi wa pili huu mwaka naweweza shika ujauzito au haiwezekani
Nimewacha kutumia sindano ya depo mwaka mmoja sasa lakini cjepata ujauzito,lakini nilitumia baada ya kuafya mimba ya mwezi mmoja je kuna uwezekano wa kubeba mimba tena ,kwa sababu nimetafuta ujauzito lakini cjepata
Kuna hatari ya kupata mimba ukitoka kuchoma sindano na kufanya tendo la ndoa?
Nateseka na kuumwa sehemu za siri nifanyaje ili nipone haraka
Tuandikie kwa whatsapp no 0678626254 tukupatie tiba