Nini kinaweza kusababisha utokwe na uchafu wa njano? Uke hutoa aina mbalimbali za uchafu katika kujisafisha. Ni jambo la kawaida kwa mwanamke kutokwa na uchafu ukeni katika mzunguko wake wote.
Mabadiliko ya homoni ya estrogen ndiyo hupalekea mabadiliko ya aina ya uteute unaotolewa. Kiwango kikubwa cha estrogen katikati ya mzunguko wako kinaweza kupeleka upate uteute mzito mwanzoni na mwishoni mwa mzunguko unakuwa mwepesi.
Baadhi ya dawa za kupevusha mayai na zingine za uzazi wa mpango zinaweza kupelekea kuongezeka kwa homoni hii ya estrogen na kukupelekea utokwe na uchafu mwingi zaidi.
Uchafu wa Njano na Afya Yako
Utokaji wa uchafu ni kishiria kikubwa juu ya afya yako. Baadhi ya aina za uchafu ni salama na kuna aina zingine za uchafu zinaweza kuashiria una maambukizi kwenye kizazi ama ukeni. Uchafu mweupe usio na harufu ni salama. Uteute wa njano ukeni kabla ya hedhi ni kawaida pia lakini pia unaweza kuashiria maanbukizi.
Uchafu wa njano ukeni kabla ya hedhi
Uchafu wa njano unaweza kuwa tofauti katika harufu yake kwa kulingana na siku ya mzunguko na pia kama una mamabukizi. Hapa chini ni sababu kubwa kwanini unatokwa na uchafu wa njano kabla ya hedhi.
Uchafu wa njano ukeni kuashiria hedhi imekaribia
Sifa ya uchafu huu unakuwa mwepesi sana na njano mpauko. Ni kawaida kabisa kupata uchafu huu wakati unakaribia hedhi. Hii ni kwasababu uke wako unazalisha uteute mwingi sana. Uchafu huu wa njano unaweza kutokana na kuchanganyika kwa damu kidogo ya hedhi pamoja na uteute mweupe wa kawaida. Endapo unapata ute wa njano kabla ya hedhi na hauna harufu basi kuwa amani.
Mzunguko mfupi wa hedhi
Sifa kubwa ya uchafu unakuwa na brown na njano. Uchafu huu hutokea zaidi kutokana na damu ya hedhi. Kama una mzunguko mfupi unaweza kuona uchafu wa brown ulichonaganyika na njano kabla ya hedhi kuanza.
Wanawake wanaokaribia kukoma hedhi(menopause) wanaweza kuona uchafu wa namna hii pia kutokana na mabadiliko ya homoni.
Uchafu wa njano ukeni unaweza kuashiria maambukizi
Sifa za uchafu huu unakuwa na njano na wenye harufu kali. Endapo unapata uchafu wa namna hii muhimu kuwahi hospitali kupata tiba mapema.
Ugonjwa Trichomoniasis
Sifa ya uchafu huu unakuwa wa njano, kijani na wenye harufu ya shombo la samaki. Wakati mwingine kutokwa na uchafu wa njano ukeni unaweza kuashiria maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama trichmoniasis. Uchafu huu huwa na harufu mbaya na huleta muwasho ukeni na maumivu wakati wa kukojoa na kufanya tendo.
Ugonjwa wa gonorrhea au chlamydia
Magonjwa ya zinaa kama gonorrhea na chlamydia mara nyingi yanaweza kutoonesha dalili mapema lakini yakakufanya ukapata uchafu usio wa kawaida wa njano kama usaha.
Pelvic infammatory disease(PID)
Sifa kubwa ya uchafu huu ni wa njano au kijani,wenye harufu mbaya. PID ni maambukizi kwneye njia ya uzazi inatokea endapo maambukizi yoyote ya ya zinaa yasipotibiwa mapema na kusambaa mpaka kwneye kizazi.
Dalili zingine ya kwamba una PID ni pamoja na
- maumivu chini ya kitovu
- homa kali
- hedhi kuvurugika
- kichefuchefu na
- maumivu wakati wa tendo la ndoa
Maambukizi ya bakteria
Maambukizi haya hutokea pale kiwango cha bakteria wazuri wanapopungua ukeni. Vihataraishi vikubwa ikiwa ni uvutaji wa sigara, kuwa na wapenzi wengi na kuosha sana uke mpaka ndani. Uchafu huu unaambatana na harufu ya shombo la samaki.
Kuvimba kwa shingo ya kizazi
Sifa za uchafu huu ni kuwa wa njano,kama usaha na wenye harufu mbaya.
Kuvimba na kututumka kwa shingo ya kizazi kunaweza kusababiswa na magonjwa ya zinaa, kukua kwa bakteria kupita kiasi na aleji ya vitu mbalimbali mfano kondomu na tampon.
Dalili zingine za kuvimba kwa shingo ya kizazi ni pamoja na
kukojoa mara kwa mara kunakoambatana na maumivu makali, maumivu makali wakati wa tendo, na kutokwa na damu baada ya tendo
Mabadiliko ya lishe
Katika mazingira fulani kutokwa na uchafu wa njano ni matokeo ya matumizi ya vyakula fulani na matumizi ya virutubishi vya vitamin.
Lini unatakiwa Kumwona Daktari?
Kutokwa na uchafu wa njano ukeni kwa kiasi kikubwa ni dalili ya maambukizi. Unatakiwa kumwona daktari mapema endapo uchfu huu unaambatana na dalili za
- harufu mbaya
- muwasho ukeni
- maumivu wakati wa kukojoa na
- maumivu wakati wa tendo la ndoa
Daktari atachukua historia ya tatizo lako na kukuuliza baadhi ya maswali. Daktari pia anaweza kuamua kuchukua sampuli ya uchafu na kuupeleka maabara kuufanyia kipimo.