Hamu ya Tendo La ndoa Kwa Mjamzito

tendo la ndoa kwa mjamzito
mjamzito

Wakati wa ujauzito mwili wako unapata na mabadiliko mengi ya kihisia na kimwili pia. Homoni zako zitabadilika sana na pia kuongezeka kwa shnikizo la damu. Wanawake wengi pia huona mabadiliko kwenye matiti kuongezeka na hamu ya tendo la ndoa kwa mjamzito pia hamu ya kula kuongezeka zaidi.

Ni muhimu kufahamu kwamba kila mwanamke mjamzito anatofautiana katikana namna mwili wake unavohisi. Lakini kuna baadhi ya mabadiliko yanayotokea kwa wote . Hamu ya tendo la ndoa, mood, uzito, hamu ya kula, usingizi wako hubadilika sana.

Mabadiliko ya Mwili kwa Mjamzito

Miezi mitatu ya kwanza unaweza kupata kichefuchefu kikali, kutapika na mwili kuishiwa nguvu, na kwenye miezi mitatu ya pili wajawazito wengi huanza kuona afadhali kwa ukali wa dalili hizo kupungua.

Hamu ya kula inaweza kurudi na mwili kuwa na nguvu na hamu ya tendo yaweza kuongezeka. Ukiona dalili hizi wala usishangazwe maana mimba yaweza kukufanya ukazalisha vitabia vya ajabu mpaka wewe ukajishangaa.

Hapa chini ni maeneo makubwa matano ambayo mwili wako utabadilika wakati wa ujauzito.

Mabadiliko ya Homoni/Vichocheo

Miezi mitatu ya mwanzo homoni za estrogen na progesterone huongezeka sana na kuleta dalili kama kuishiwa nguvu, matiti kuongezeka msisimko na
hamu ya tendo kupungua

Katika week 10 za mwanzo homoni hizi mbili zitapungua, na ndipo mwili utarejea kuwa na nguvu , hamu ya tendo la ndoa kurejea na kupungua kichefuchefu.

Kwenye miezi mitatu ya ya mwisho, dalili kama kuongezeka uzito, maumivu ya mgongo na dalili zingine zinaweza kuathiri hamu ya tendo na kujikuta hutaki kufanya tendo wala kuhisi matamanio ya kukutana na mwanaume kimwili.

Unapopitia dalili hizi wala usishangae, fahamu tu kwamba kuelekea kujifungua mtoto utapitia vipindi vya milima na mabonde, kashkash za hapa na pale mpaka utakapozaa.

Msisimko wa matiti na presha ya damu vitaongezeka

Mimba inafanya shinikizo la damu kuongezeka hasa kwenye viungo vya via vya uzazi, matiti na kwenye mashavu ya uke.
Msukumo wa damu unapokuwa mkubwa ndipo hamu ya tendo na msisimko wa tendo utaongezeka sana.

Hili ni jambo la kawaida kwa mjamzito, itakufanya upate wakati mzuri sana wa kufurahia tendo na mwenzi wako.

Usishangazwe endapo utaona majimaji yakitoka kwenye chuchu zako, kumbuka tu mwili unabadilika sana kipindi hichi cha ujauzito, badala ya kushangaa furahia mabadiliko haya.

Hamu ya Tendo Yaweza Kuongezeka

Wanawake wengi wanapatwa na hali hii ya kuongezeka hamu kwenye miezi mitatu ya mwanzo na miezi mitatu ya katikati. Kuongezeka kwa hamu ya tendo kunaambatana na kuongezeka kwa utelezi kwenye uke na msisimko wa kinembe.

Pia kuongezeka kutokana na kuongezeka kwa msukumo wa damu. Ni wakati wako na mwenzi wako kufurahia mabadiliko haya kwani yanatokea mara chache katika maisha yako.

Mimba itakufanya uwe free kihisia na kimawazo

Wanawake wanakutana na changamoto nyingi sana kwenye mahusiano ukilinganisha na wanaume. Unakumbuka kipindi bado hutaki kuzaa, zile stress za kukutana na mwanaume bila kinga na kuanza kuwaza kama imeingia itakuwaje. Unawaza kuhusu utoaji wa mimba kama ikitokea imeingia.

Umeingia kwenye ndoa imepita miezi mitatu hujashika mimba unaanza kuwaza tena itakuwaje, mawifi watakufiiriaje, majirani je. Sasa mimba imeingia huna tena la kuwaza kujizuia kushika mimba au lini utashika mimba, unakuwa free kujiachia.

Je kufanya tendo la ndoa kunapelekea kuzaa kabla ya wakati?

Kwa wanandoa wengi hawa mimba ya kwanza inapofikia kipindi cha kujifungua, huwa wanajiuliza maswali mengi sana. Maswali haya ni pamoja na nini cha kufanya na kipi cha kuepuka ili kutomdhuru mtoto aliye tumboni.

Swali kubwa linakuwa kwenye tendo la ndoa, kama inafaa na haileti shida ya mimba kutoka mapema kabla ya muda wake. Je kufanya tendo kunasababisha mimba kuharibika au kujifungua kaba ya wakati?

Jibu ni ndio lakini siyo kwa wanawake wote.

Kama upo kwenye miezi mitatu ya pili au mitatu ya mwisho(third trimester) unaweza kuwa umegundua kizazi chako kuwa kama kigumu baada ya kumaliza tendo la ndoa. Dalili hizi ni kwasbaabu ya kufika kileleni na hivo kupelekea hali kama ya kutaka kijifungua (false labour contraction)

Kumbuka dalili hizi wala siyo za kweli, zinaishaga baada ya muda mfupi. Lakini kadiri unakaribia siku zako za kujifungua unatakiwa kuwa makini kwani kukaza huku wa kizazi yaweza kua ni kweli unataka kujifungua.

Jinsi gani tendo la ndoa linakufanya ujisikie dalili ya kutaka kujifungua.

Shahawa zina kemikali zinazoitwa prostaglandins. Wanasayansi wanaamini kwamba kemikali hizi zinazofanya kazi kama homoni. Pale mbegu zinapomwagwa ukeni zinajikusanya kwenye eneo la mlango wa kizazi na kulainisha eneo hilo kuliandaa kwa ajili ya kutanuka na hivo kupelekea kizazi pia kutanuka.

Kutanuka na kusinyaa pia kwa kizazi kunakosababishwa na hisia za kufika kileleni kunaweza kusababisha pia mimba kuanza kutoka kabla ya wakati wake.

Je kufanya tendo wakati wa ujauzito ni hatari?

Kama mwili bado hauko tayari kuzaa basi tendo la ndoa haliwezi kusababisha mimba kutoka. Tendo la ndoa katika umri wowote wa ujauzito bado ni salama. Kizazi chako kuwa kigumu pale unapofika kileleni isikutishe kwamba mimba inatoka hapana. Ni hali ya kawaida kabisa ya mwitikio wa mwili.

Imani potofu kwamba kufanya tendo kunaweza kupelekea mtoto kuchomwa na uume siyo za kweli. Uume unapoingia ukeni hauwezi kumchoma mtoto kwasbabau analindwa kwenye chupa yake yenye majimaji mazito.

Tendo la ndoa ni salama kwa mjamzito mpaka pale tu ukishauriwa vingine na daktari. Mfano kwa wanawake wenye matatizo ya mimba kuharibika mara kwa mara na wenye kizazi kilicholegea watatakiwa kutofanya tendo mpaka wajifungue.

Mambo ya kuzingatia kwa mjamzito kwenye tendo la ndoa

  • Tumia staili ambayo haikupi maumivu
  • Tumia condom pale unapokutana na mwanaume mpya ili kuepuka magonjwa ya zinaa
  • Usifanye ngono kupitia njia ya haja kubwa kwani unaweza kupata maambukizi ya bakteria
  • Usifanye tendo kama chupa yako imepasuka kwani mtoto anaweza kupata maambukizi kiurahisi, badala yake wahi hospitali
  • Nenda hospitali mapema endapo utaona dalili za maumivu au kutokwa na majimaji mazito ukeni, au kutokwa damu wakati wa ujauzito.

Utakubaliana na mabadiliko ya Mwili wako

Kwenye week zako 40 za mimba lazima uzito utaongezeka, unaweza kuongezeka kilo 10 mpaka 15. Japo baadhi ya wanawake hujisikia vibaya kwa mabadiliko haya baadhi hufurahia kuongezeka huku kwa uzito maana inawapa mwonekano mpya kimwili na kihisia.

Matiti kuongezeka, hips za duara na figure kuwa matata sana kiasi ya kukuongezea urembo wako.

Bofya kusoma kuhusu: Dalili hatari kwa mjamzito ambazo hutakiwi kupuuza

4 replies on “Hamu ya Tendo La ndoa Kwa Mjamzito”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *