Karafuu kwa jina la kisayansi (Syzygium aromaticum) ni kiungo chenye harufu nzuri ambacho kimekuwa kikitumika na jamii ya watu mbalimbali kwa miaka mingi duniani kote. Leo utajifunza faida pia za mafuta ya karafuu.
Kama ilivyo kwa viungo vingine mmea wa karafuu pia unaweza kutengeneza mafuta tiba ambayo yanaweza kutibu changamoto nyingi za kiafya. Ni mafuta ambayo hutakiwi kuyakosa nyumbani kwako muda wote. Nchi zinazoongoza kwa uzalishaji wa karafuu ni pamoja na Indonesia, india, Zanzibar pamoja na Madagascar.
Faida 8 usizojua za Mafuta ya Karafuu.
- Kutibu magonjwa ya meno kama kuvimba fizi na maumivu makali ya meno
- Mfumo wa chakula: mafuta ya karafuu yanasaidia kutuliza misuli ya tumbo na hivo kuleta nafuu kwa changamoto za kutapika na tumbo kuchafuka.
- Kwenye ngozi: mafuta yanasaidia kutibu changamoto za chunusi, makovu kwenye ngozi na vigwaru/masundosundo.
- Kwenye mfumo wa hewa; mafuta yakitumika huleta nafuu kwa mwenye kikohozi kikali, pumu ,TB, pamoja na kufungua njia za hewa.
- Kuua vimelea wabaya na hivo kusaidia mweye fangasi, vidonda na majeraha kupona mapema.
- Marashi: kutokana na harufu yake nzuri mafuta ya karafuu yanatumika kutengeneza pafyumu .
- Kiungo cha chakula; ili kuongeza ladha karafuu inatumika kwenye chakula .
- Mafuta ya karafuu pia hutumika kwa masaji ya mwili ili kuondoa maumivu .
Namna ya Kutumia Mafuta ya Karafuu
- Kwa changamoto za upumuaji chemsha maji kidogo weka mafuta ya karafuu kisha vuta mvuke wake.
- Chovya kiasi kodogo cha mafuta pakaa kwenye ngozi ili kuweka ngozi nyororo
- Kwa maumivu ya jino. Chukua kiasi kidogo cha mafuta ya karafuu, changanya na kiasi kidogo cha mafuta ya nazi kisha fanya masaji kwenye eneo la jino lililoathorika.
- Kwa maumivu ya kichwa chonya kiasi kidogo cha mafuta ya karafuu kisha sugua eneo la mbele la kichwa kwa muda wa dakika 5
- Mafuta ya karafuu pia yanaweza kutumika kufukuza wadudu kama mbu endapo utajipaka kwenye ngozi.
- Kuondoa harufu mbaya ndani ya nyumba unaweza kuchanganya mafuta kiasi kwenye sufuria weka na maji kiasi kidogo, kisha chemsha maji katika moto mdogo taratibu mvuke utasambaa ndani ya nyumba na kuleta harufu nzuri.
Je Mafuta ya Karafuu ni Salama kutumiwa na kila mtu?
Kama ilivyo kwa mafuta tiba mengine, mafuta ya karafuu yanatakiwa kutumika kwa uangalifu, kwani kiwango kikubwa kinaweza kuleta athari kwenye mwili. Tahadhari zaidi ichukuliwe unapopakaa mafuta kwenye maeneo kama kwenye fizi.
Wanawake wajawazito na wenye mimba wanaweza kutumia karafuu kwenye chakula. Lakini siyo salama kutumia mafuta ya karafuu yenyewe.
Watoto wadogo chini ya miaka miwili wasitumie mafuta ya karafuu kwani yaweza kupelekea kuathirika kwa baadhi ya viungo vya mwili.
Kama umepangiwa kufanyiwa upasuaji inashuriwa usitumie mafuta ya karafuu week mbili kabla, kwani kampaundi ya eugenol iliyopo kwenye mafuta ya karafuu husababisha kuechelewa kupona kidonda.
2 replies on “Faida za Mafuta ya karafuu”
Asante kwa elimu yako nzuri.
karibu na endelea kufatilia makala zetu