Categories
Hedhi salama Menopause

Kukoma hedhi mapema

kukoma hedhi

Kukoma hedhi kitaalamu menopause ni kipindi katika ukuaji wa mawanamke ambapo damu ya kila mwezi inakata kutoka. Jambo hili hutokea hasa miaka ya 40 au wengine mpaka 50. Ni kipindi ambacho kinaambatana na mabadiliko mengine makubwa ya mwili ikiwemo kupungua hamu ya tendo, mashavu ya uke kusinyaa na mifupa kuwa dhaifu.

Kukoma hedhi mapema zaidi

Kwa wanawake wengi kukoma hedhi hata siyo jambo la kuliwazia mpaka pale utakapofikia miaka 40s au 50s. Japo mmoja kati ya wanawake 100 anaweza kukoma hedhi mapema zaidi akiwa na miaka 20s au 30s, kuliko ilivozoeleka.

Menopause inapoanza mapema zaidi kabla hujafikisha miaka 40, tunaita primary ovarian insufficiency au primary ovarian failure.

Kundi gani la wanawake wanaweza kukoma hedhi mapema zaidi?

Wakati unaanza kukoma hedhi, mifuko ya mayai yani ovary zinapunguza uzalishaji wa homoni za estrogen. Kukoma hedhi siyo kipindi kifupi, ni mlolongo wa miaka inaweza kuchukua hata miaka 5 au 10 kukoma kabisa hedhi. Utaanza kwa kukosa hedhi miezi mi3 mpaka 6 kisha baadae unakoma mwaka mzima.

Hichi kipindi cha kukosa hedhi ndicho chaweza kudumu mpaka miak 5 au 10 kabla hujakoma moja kwa moja.

Sababu nyingi zinaweza kupelekea mwanamke akome hedhi mapema kabla ya mda wake. Sababu hizi ni pamoja na

Dalili za kukoma hedhi mapema

Wanawake waliokoma hedhi mapema wanapata dalili za

Kumbuka siyo kawaida kwa mwanamke aliye kwenye umri wa kuzaa kupata dalili hizi, hivo hakikisha unamwona daktari mapema apate kupima homoni zako”

Daktari atahitaji kupima kiwango cha homoni ya estrogen na FSH kujiridhisha kama kweli umekoma hedhi.

Ushauri gani wa kuzingatia na Lishe ukiwa kwenye menopause?

Vyakula vya kutumia mara kwa mara ukishakoma hedhi

Unapojaribu kuekebiusha homoni zako zilizovurugika na kupunguza madhara ya menopause, lishe yako inatakiwa kujumuisha madini ya kutosha na mafuta mazuri. Unapokula lishe hii kwa wingi itakusaidia kuweka sawa homoni na pia kukupunguzia mafuta mabaya mwilini.

Weka akili kwamba kadri unavozeeka utahitaji kupunguza kiwango cha mlo wako kwasababu kasi ya shuguli za mwili inapungua na umri. Ni muhimu sana kujizuia vyakula vilivyosindikwa na kupendelea kula chakula safi. Vyakula vitakavyokusaidia ni pamoja na

1.Vyakula vyenye madini ya calcium kwa wingi

Mifupa kudhoofika ni moja na changamoto inayotokea baada ya kukoma hedhi. Japo mwanzoni huwezi kuona lakini madhara yake yanaweza kuonekana miaka ya baadae.

Mwili wako unajenga mifupa kuanzia ukiwa mdogo mpaka kufikia miaka 30. Baada ya hapo unaanza kupoteza mifupa. Kwa mwanamke kutokana na kupungua kwa homoni ya estrogen, kasi ya kumomonyoka mifupa inakuwa kubwa zaidi baada ya kukoma hedhi.

Ndiomaana tunashauri upendelee kula kwa wingi vyakula vyenye madini ya Calcium kama

  • maziwa
  • yogurt
  • mboga za majani za kijani kilichokolea na
  • dagaa
  • mboga zingine jamii ya kabeji kama broccoli, cauliflower na asparagus

2.Vyakula vyenye fiber/kambakamba kwa wingi

Vyakula vyenye kambakamba ni muhimu sana kwa afya ya moyo na mfumo wa chakula, pamoja na kuweka sawa uzito wako. Baadhi ya tafiti zinasema ulaji wa vyakula vya kamba kwa wingi unasaidia pia uzalishaji wa homoni ya estrogen. Homoni ambayo inapungua sana kwa walikoma hedhi.

Vyanzo vizuri vya kambakamba ni pamoja na karanga, parachichi, mbegu, maharage, nafaka, mbogamboga na matunda.

3.Mafuta yenye omega 3

Omega 3 ni kiambata kinachopatikana kwenye samaki na mbegu za maboga. Kiambata hiki kinasaidia kuimarisha moyo , kumarisha ngozi na kuzuia mwili kututumka . Mafuta haya yanapatikana zaidi kwenye samaki aina ya saladini na salmon. Tafiti zinasema kwamba kutumia omega 3 mara kwa mara kunasaidia uzalishaji wa homoni na kuzuia makali ya menopause.

4.Vyakula vya mafuta mazuri

Ni kweli kwamba vyakula vya mafuta havipandishi sukari kwenye damu ukilinganisha na vyakula vya sukari na wanga. Ndiomaana hata wenye uzito mkubwa na kitambi na wenye kisukari tunawashauri wale zaidi vyakula vya mafuta.

Pia vyakula hivi vinapunguza mpambano ndani ya mwili. Mafuta ndio yanayounda homoni zako mwilini. Hakikisha unapata mafuta mwali ambayo hayajachakachuliwa wala kuongezwa kemikali mbaya. Mafuta haya ni yale ya nazi, olive, vyakula kama nazi, parachichi, karanga ,ufuta na mbegu za maboga.

Categories
Afya ya mwanamke na uzazi Tendo la ndoa

Maumivu ukeni wakati wa tendo

maumivu ukeni wakati wa tendo

Tendo la ndoa ni moja na tukio tamu na la kufurahisha sana katika maisha ya mwandamu. Tendo linaimarisha ukaribu na upendo baina ya mke na mume. Pamoja na hayo ,watu wengi wanapata maumivu makali wakati wa tendo na hawafurahii kabisa. Kuna mambo mengi yanapelekea maumivu ukeni wakati wa tendo. Soma zaidi kujua nini cha kufanya kuondoa tatizo.

Maumivu kwenye tendo la ndoa ni kitu gani hasa?

Kitaalamu huitwa dyspareunia ni neno linalomaanisha maumivu ya via vya uzazi wakati wa tendo au baada ya tendo. Tatizo hili linawapata karibu asilimia 75 ya wanawake wote duniani.

Maumivu kwenye tendo yanaweza kuvuruga mahusiano, kukufanya ujihisi mpweke na huna thamani na kukosa kujiamini mbele ya mpenzi wako. Baadhi ya wanawake huamua kutojihusisha tena na tendo la ndoa baada ya kupata maumivu.

Pamoja na kwamba tatizo linatibika kwa kiasi kikubwa, watu wengi ni waoga sana kuelezea changamoto hii kwa kuogopa aibu ama kudharaulika.

Dalili za maumivu kwenye tendo

  • maumivu ya haraka
  • hali ya kuungua ukeni
  • kukosa hamu ya tendo
  • kushindwa kufika kileleni
  • maumivu ya tumbo

Je haya maumivu yanatokea ukeni tu?

Maumivu kwenye tendo yanatofautiana kwa kila mtu. Baadhi ya wanawake wanahisi maumivu wakati uume unaingia, na wengine wanapata maumivu wakiguswa tu kwenye via vya uzazi. Baadhi wanapata maumivu ya tendo baada ya kukoma hedhi.

Maumivu yanaweza kutokea

  • ndani ya ukeni
  • kwenye mashavu ya ukeni
  • chini ya mgongo
  • ndani ya kizazi
  • kwenye nyonga
  • tumboni chini ya kitovu na
  • kwenye ukuta unaotenganisha uke na mkundu

Baadhi ya wanawake wanapata maumivu baada tu ya kumaliza tendo, na wengine wakati wa kukojoa.

Nini kinapelekea maumivu kwenye tendo?

Baadhi ya sababu kubwa zinazopelekea mwanamke kupata maumivu ni pamoja na

1.Ukavu ukeni

Hii ni sababu kubwa zaidi ya maumivu kwenye tendo kutokana na kukosekana na ute ukeni na hivo msuguano kuwa mkubwa. Ukavu ukeni inatokea zaidi baada ya kukoma hedhi. Mabadiliko ya homoni yanapelekea kupungua kwa uzalishaji wa ute kwenye uke baada ya kukoma hedhi.

Sababu zingine zinazopelekea ukavu ukeni ni pamoja na kutumia njia za kisasa kupanga uzazi, kunyonyesha, stress na mwanamke kutoandaliwa vya kutosha.

2.Maambukizi

Maambukizi aina tofauti yanaweza kupelekea maumivu kwenye tendo. Maambukizi haya ni pamoja na

  • maambukizi ya bakteria ya ni bacterial vaginosis
  • fungus ukeni: dalili zake ikiwa ni pamoja na kutokwa uchafu unaoganda mzito, muwasho
  • kisonono
  • UTI kali
  • PID na
  • Chlaydia

Pia magonjwa mengine kwenye kizazi yanaweza kupelekea maumivu kwenye tendo. Magonjwa haya ni pamoja na

  • Endometriosis- yani ukuta wa ndani wa kizazi kuvimba
  • vaginismus: hii ni hali ya uke kugoma kuruhusu kitu chochote kuingia
  • Fibroids: Vimbe kwenye ukuta wa kizazi
  • Ovarian cyst: Vimbe kwenye mayai
  • Bartholin abscess: hizi ni vimbe kweye tezi za uke
  • Cervicitis: yani maambukizi kwenye mlango wa kizazi na kupelekea kuvimba kwake

Kumbuka magonjwa haya ni ngumu kwako kuyagundua ukiwa nyumbani. Ni mpaka kwenda hospitali, na kufanyiwa vipimo ndipo daktari atakwmabie endapo una uvimbe nk

Nini cha kufanya kuondoa maumivu?

Tiba ya tatizo inategemea na chanzo chake. Unapojiskia vibaya, hatua ya kwanza ni kwenda hospital na kuonana na daktari ili akusaidie kugundua chanzo cha tatizo.
Daktari atakuuliza baadhi ya maswali kujua historia ya tatizo, na aatapendekeza vipimo vya kufanyiwa.

Baada ya vipimo ndipo utapewa dawa sahihi ili uanze tena kufurahia tendo la ndoa.

Mawasiliano baina ya wapenzi

Mawasiliano ni nguzo muhimu sana kwenye mahusiano, itasaidia wapenzi kujuana kuhusu changamoto zao. Mpenzi wako ataweza kukuvumilia wakati unaendelea na tiba. Kumbuka kuendelea kufanya tendo wakati unapata maumivu ni mbaya, kwani itakuathiri kisaikolojia na kukfanya uchukue tendo la ndoa.

Kama chanzo cha tatizo ni ukavu ukeni, ni muhimu sana mtumie muda mwingi kwenye kuandaana.

Weka kwenye akili kwamba kutumia vilainishi vya kuganda kulainisha uke, yaweza kuleta madhara kwenye tishui laini za uke. Ni vizuri kutumia vilainishi vye maji maji pamoja na condom.

Kama maumivu unapata siku kadhaa tu, basi jaribu kubadili style ya kufanya mapenzi. Ongea na mwenzi wako akuingilie taratibu bila nguvu nyingi.

Lini unatakiwa kumwona daktari?

Muone daktari haraka endapo tatizo linajitokeza mara kwa mara, na maumivu yanazidi kila unapojaribu kufanya tendo. Pia kama unajihisi unaugua magonjwa kama fungus, unatokwa uchafu usio kawaida ana unapata maumivu ya tumbo muone daktari haraka.

Categories
Afya ya mwanamke na uzazi

Maumivu ya tumbo chini ya kitovu

maumivu ya tumbo chini ya kitovu

Maumivu ya tumbo yanaweza kusababishwa na vitu vingi sana na yanaweza kuhusisha zaidi ya kiungo kimoja cha mwili. Na maumivu ya tumbo chini ya kitovu yanahusisha viungo vyote vya uzazi, na viungo vingine kama figo na kibofu. Maumivu yanapoanza inaweza kuwa ngumu kujua chanzo cha tatizo ndiomaana ni muhimu kwenda hospital.

Nini kinapelekea maumivu ya Tumbo chini ya kitovu?

Maumivu chini ya kitovu yanakuja kutokana na athari kwenye viungo vya karibu. Viungo hivi ni pamoja na

  • utumbo mdogo
  • utumbo mkubwa
  • kizazi
  • mifuko ya mayai
  • kibofu cha mkojo
  • mirija ya kubeba mkojo kutoka kwenye figo mpaka kibofu na
  • Nyonga

Mara chache inaweza kutokea athari ikaanzia viungo vya mbali kabisa, lakini maumivu yakasafirishwa mpaka eneo la chini ya kitovu. Wakati ukipata hitilafu kwenye figo, figo zipo eneo la juu na maumivu yake yaweza kusambaa mpaka chini ya kitovu. Pia kama korodani zako zinauma maumivu yanaweza kusambaa mpaka chini ya kitovu

Aina za maumivu ya tumbo chini ya kitovu

Maumivu ya tumbo yanaweza kuwa ya muda mfupi ama ya mda mrefu. Maumivu ya mda mfupi yanaweza kusababishwa na jeraha au maambukizi kwenye kiungo husika. Magonjwa makubwa yanaweza kupelekea maumivu ya mda mrefu. Muone daktari mapema endapo maumivu yako yanaongezeka kila siku na hayaishi.

Je maumivu ya tumbo chini ya kitovu ni tatizo kubwa?

Kama tulivoona hapo juu, maumivu ni kiashiria kwamba kuna tatizo fulani la kiafya kwenye mwili. Ni ngumu kutambua chanzo kwa kufatilia maumivu pekee. Ni muhimu kumwona daktari akupime kugundua chanzo cha tatizo. Daktari atakupa dawa za kupunguza maumivu wakati huo atashugulika kujua chanzo.

Nini chanzo kikubwa cha maumivu ya tumbo chini ya kitovu?

Viungo kama utumbo mkubwa na mdogo vipo eneo la tumbo la chini, na vinachukua nafasi kubwa sana pale. Kwa sababu hiyo changamoto yoyote inayoathiri utumbo basi yaweza kuwa chanzo cha maumivu chini ya kitovu.

Changamoto hizi za kila siku ni pamoja na

  • gesi tumboni
  • chakula kutosagwa vizuri
  • kuharisha na
  • kukosa choo na choo kigumu

Kama chakula hakisagwi vizuri na tumbo kujaa, waweza kuwa na aleji na aina fulani ya chakula, ama tumbo lako haliwezi kusaga aina fulani cha chakula. Suluhisho ni kuacha kabisa kutumia aina ya chakula ambacho unaona mwili umekikataa.

Pia yawezekana utumbo umebimba kwa ndani. Magonjwa yanayopelekea utumbo kuvimba ni pamoja na

  • vudonda vya tumbo
  • maambukizi ya bakteria
  • Celiac disease (ambapo mwili unashambulia kiambata cha guleten ambacho hupatikana kwenye ngano)
  • Majeraha kwenye utumbo mdogo na mpana na
  • Saratani kwenye utumbo

Je nini chanzo cha maumivu ya tumbo kwa mwanamke?

Kama wewe ni mwanamke, viungo vya uzazi vipo eneo la chini ya kitovu. Viungo hivi ni chanzo kingine kikubwa cha maumivu ya tumbo chini ya kitovu. Japo maumivu ya tumbo la hedhi ni kawaida kwa kila mwanamke, sometime yanaweza kuashiria uwepo wa changamoto flani ya kiafya kama

  • PID
  • Vimbe kwenye kizazi (fibroids)
  • Kizazi kututumka (endometriosis)
  • Saratani ya kizazi
  • Vimbe kwenye mayai

Magonjwa ya Figo

Kama tatizo siyo kwenye mfumo wa chakula, basi yawezekana kuna shida kwenye njia ya mkojo ambako figo zinahusika. Ugonjwa mkubwa kwenye njia ya mkojo ni UTI yani maambukizi ya bakteria kwenye njia ya mkojo. UTI inaweza kuathiri kibofu cha mojo, mirija ya kusafirisha mkojo na hata figo pia. Na matatizo yote haya huzalisha maumivu kwenye kitovu.

Vipi kama maumivu ya tumbo yanatokea upande wa kushoto au kulia?

Maumivu ya tumbo upande wa kushoto chini ya kitovu yanaweza kutokana na athari kwenye utumbo mpana. Yawezekana kukawa na bakteria waliojificha eneo hilo na kupelekea kututumka mpaka kuleta maumivu.

Maumivu yakiwa eneo la chini kulia, yaweza kuwa ni appendix. Hiki ni kifuko kidogo ambacho huhifadhi mawe. Kifuko kinaweza kushambuliwa na bakteria ama kikajaa uchafu na hivo suluhishi ikawa ni kukiondoa kabisa.

Pia Maumivu kulia na kushoto kwa chini inaweza kutokana na athari kwenye mifuko ya mayai ama figo. Uvimbe kwenye yaia au mawez kwenye figo vyote hupelekea upate maumivu. Pia kama yai linatolewa kwenye kikonyo siku ya hatari, laweza kupelekea maumivu haya.

Je lini natakiwa kumwona daktari?

Muone daktari haraka sana kama

  • Maumimvu yamekuja haraka na ni makali sana
  • Maumivu yanazidi kuwa makali siku hadi siku
  • umeshindwa kwenda haja ndogo au kubwa kwa siku kadhaa
  • unapata dalili za unjano kwenye macho
  • unapata homa kali, kichefuchefu na kutapika
  • Tumbo lako ni gumu au laini sana ukishika
  • ulipata ajali hivi karibuni na maumivu yameendelea
  • una mimba
Categories
Afya ya mwanamke na uzazi

Makovu kwenye kizazi

makovu kwenye kizazi
kizazi

Makovu kwenye kizazi kitaalamu Asherman’s syndrome ni tatizo analopata mwanamke ukubwani kwenye mfuko wa uzazi. Tishu hizi za makovu huanza kujitengeneza na kukua kupita kaisi mpaka kupunguza ile nafasi ya ndani ya kizazi kuwa kidogo kuliko kawaida.

Hali hii yaweza kuleta maimivu sana ya nyonga na tumbo, hedhi nyepesi sana na kushindwa kushika mimba.

Nani anaweza kupata makovu kwenye kizazi?

Muhimu ifahamike kwanza ugonjwa huu siyo wa kurithi, unaupata kulingana na changamoto za kiafya unazopitia ukubwani. Hatari ya kupata tatizo inaongezeka zaidi endapo

  • uliwahi kufanyiwa upasuaji kwenye kizazi mfano kuondoa uvimbe
  • kutolewa mimba kwa vyuma (dilation & currettage) au upasuaji wakati wakujifungua(c-section)
  • historia ya kuugua PID mda mrefu
  • unatibiwa saratani

Zipi ni dalili kwamba una makovu kwenye kizazi?

Ukiwa na ugonjwa wa makovu kwenye kizazi unaweza kupata dalili nyingi. Dalili hizi ni pamoja na

  • kupata hedhi nyepesi sana(hypomenorrhea)
  • kukosa hedhi kabisa au kutokwa na damu nyingi kupita kiasi
  • kuhisi maumivu makali ya tumbo na nyonga
  • kushindwa kushika mimba mapema

Kwa baadhi ya wanawake hawapati dalili zozote kabisa, na wengine wanapata hedhi vizuri tu. Kama unahisi hitilafu kwenye via vya uzazi na hedhi yako na unatafuta mimba mda mrefu, muone daktari ili akupime kujua shida iko wapi.

Nini kinapelekea makovu kwenye kizazi?

Makovu kwenye kizazi yanaweza kusababishwa na changamoto mbalimbali. Sababu hizi ni pamoja na

1.Upasuaji kwenye kizazi kitaalamu (hysterectopy):– huu ni upsuaji ambapo daktaru anaingiza kifaa kidogo chenye camera kupitia kwenye uke kwenda kwenye kizazi. Lengo ni kukata vimbe mfano fibroids.

2.Kusafisha kizazi kwa vyuma baada ya kutoa mimba(Dilation & curretege): Unapotoa mimba kuna mabaki ya tishu yaweza kusalia kwenye kizazi. Hivo hospitali utafanyiwa upasuaji mdogo wa kutanua mlango wa kizazi kisha kukwangua mabaki yaliyopo kwenye kuta za kizazi. Kitendo hichi chaweza kuacha makovu kwenye kizazi chako ukasindwa kushika mimba siku zijazo.

3.Upasuaji wakati wa kujifungua(C-section): Upasuaji huu unafanyika pale inaposhindikana kujifungua kwa njia ya kawaida ya uke. Katika baadhi ya wanawake, upasuaji huu waweza kupelekea kuota kwa makovu kwenye kizazi. Kwa mama anayejifungua kwa upasuaji, makovu hutokea hasa kama akipata maambukizi baada ya hili zoezi.

4.Maambukizi kwenye kizazi: Maambukizi pekee hayapelekei upate makovu kwenye kizazi. Lakini maambukizi yanapotokea wakati unafanyiwa upasuaji, hatari inaongezeka zaidi. Maambukizi haya ni pamoja na PID na cervicitis

4.Matibabu ya mionzi: Matibabu kwenye saratani ya shingo ya kizazi yanayohusisha mionzi yanaweza kuacha makovu.

Je kitanzi chaweza kupelekea makovu kwenye kizazi?

Kitanzi ni kifaa kidogo mfano wa herudi T ambacho hutumika kupanga uzazi. Kifaa hiki huwekwa ukeni na mtalamu wa afya hospitali na kinaweza kukukinga usipate mimba hata kwa miaka 7. Kitanzi kinapowekwa ukeni kunakuwa na hatari ya kupata maambukizi na makovu kwenye kizazi.

Je vipimo gani huafanyika kugundua uwepo wa makovu kwenye kizazi?
Vipimo vya picha

Vipimo vya picha humsaidia daktari kupata undani wa tatizo lako kwa kulinganisha na dalili unazopata. Vipimo hivi vya picha vyaweza kufanya juu ya ngozi ama kuhitaji kuingiziwa kifaa ndani ya uke. Vipimo hivi ni pamoja na

1.Utrasound: Aina hii ya kipimo inahusisha mawimbi ya sauti kutengeneza picha ya ndani ya viungo vyako. Utrasound yaweza kufanyika eneo la juu la ngozi ama kwa ndani ya uke(trans-vaginal utrasound)

2.Hysteroscopy: Kwenye kipimo hiki mtoa huduma, anaingiza kifaa kidogo chenye camera kupitia uke ili kuchunguza uwepo wa makovu.

Je tatizo linatibiwaje Hospital

Daktari wako atachukua maelezo na vipimo kisha atapendekeza tiba sahihi ya taizo lako. Kumbuka ukiwa na daktari ni muhimu ujieleze dalili zote unazopata na historia yako. usiogope kumweleza daktari kama ulishatoa mimba mbili ay hata tano.

Lengo kubwa la tiba ni kuondoa makovu na kurudisha kizazi kwenye shape yake ya mwanzo. Tiba hii itasaidia

  • kuondoa maumivu unayopata
  • kurejesha mpangilio wako wa hedhi
  • kurejesha tena chansi ya kushika mimba endapo hujafikia menopause

Daktari anaweza kuingiza kifaa kidogo hysteroscope ili kuondoa makovu kwenye kizazi. Kifaa cha hysteroscope kinakuwa na cemara ya kutazama kuta za kizazi, lakini pia chaweza kutumika kuondoa makovu. Hatari iliyopo kwenye nnia hii ni kuharbu kuta mpya, yani kutengeneza makovu mengine tena.

Je naweza kushika mimba baada ya kutibiwa makovu?

Kwa kiasi kikubwa jibu ni ndio, unaweza kushika tena mimba baada ya tiba. Ugumba sometime ni tatizo gumu sana maana chanzo cha tatizo chaweza kutojulikama kabisa. Kama muhudumu ameona makovu ndio chanzo, maana yake kuyatoa makovu ni tiba yako kushika tena mimba.

je makovu kwenye kizazi yanaweza kupelekea mimba kuharibika?

Kumbuka bado waweza kupata mimba hata kama una makovu kwenye kizazi. Makovu kwenye kizazi yanaweza kupunguza ukubwa wa chumba cha kizazi. Hii inaweza kuleta shida kwenye ukuaji wa mimba, na kupelekea matatizo kama mimba kuharbika, kuzaa njiti ama kukatika kondo la nyuma. Pia tishu za makovu zaweza kuziba mlango wa kizazi na mtoto kutozaliwa vizuri.

Ushauri kutoka Maisha Doctors

Kama utahisi maumivu makali wakati wa hedhi, maumivu chini ya kitovu au kukosa mimba mda mrefu na uliwahi kufanyiwa upasuaji ama kutoa mimba, muone daktari.

Kwa ushauri tuandikie kwa whatsapp namba 0678626254

Categories
Afya ya mwanamke na uzazi Hedhi salama

Hedhi nyeusi

hedhi nyeusi
hedhi

Kwanini unapata hedhi nyeusi?

Wanawake wengi wanaanza hedhi baada ya kuvunja ungo miaka 12 na 13, ikiwa hakuna tatizo lolote la kiafya. Hedhi ni damu inayotoka kila mwezi baada ya ukuta wa kizazi kubomoka, endapo mimba haikutungwa. Rangi na mwonekano wa hedhi yako ni kiashiria kikubwa kuhusu mwenendo wa afya yako ya uzazi.

Kwenye makala hii utajifunza

  • chanzo cha hedhi kuwa nyeusi
  • tiba ya tatizo na
  • lini unatakiwa umwone daktari

Mabadiliko ya rangi ya hedhi

Rangi ya hedhi yako inaweza kubadilika kutoka kwenye nyekundu ya kungaa, chungwa, brown na pia nyeusi. Ni muhimu kutambua kwamba hedhi nyeusi, siyo kwamba inakuwa nyeusi hasa hapana. Ni ile hali ya weusi usiokoleakama vile damu ilopigwa na upepo ikaganda.

Sometime hedhi nyeusi yaweza kuashiria changamoto fulani ya kiafya na ndiomaana tumeandika makala hii ujifunze.

Chanzo cha hedhi nyeusi

Damu nyeusi ya period inachukua muda mrefu sana kutoka nje ya kizazi, na hivo kupitiwa na hewa. Kitendo huitwa oxidation, yani damu kuachanganyika na hewa na kuifanya iwe nyeusi au ya brown, sawa na rangi ya kahawa.

Hedhi nyeusi na na kutokwa uchafu ukeni mara nyingi siyo ishu kubwa ya kukuletea mawazo. Uke unajisafisha kila siku na hedhi yaweza kutokea ukapata nyeusi mara chache. Pamoja na hivo unatakiwa kufatilia afya yako na aina za uchafu unaotoka ukeni.

Sababu 8 zinazofanya upate hedhi nyeusi

1.Hedhi nyeusi kuashiria mwanzo au mwisho wa hedhi

Speed ya kutoka damu inakuwaga ndogo sana mwanzoni na mwishoni mwa hedhi. Hedhi inavochelewa zaidi kiutoka ndipo uwezekano ni mkubwa ikapitiwa na hewa ya oksijeni na kuwa nyeusi.

2.Kuna Kitu kimekwama ukeni

Hedhi nyeusi sometime inaweza kuashiria uwezo wa kitu ukeni kilichokwama, vitu hivi ni kama condom, kitanzi, sex toy, sponge na tampon. Damu hii isipotoka inafanya uke kuvimba kwa ndani na kupelekea maammbukizi.

Dalili hizi zinaashiria kwamba tayari umepata maambukizi ukeni na kwenye kizazi

  • kutokwa uchafu unaonuka sana ukeni
  • muwasho maeneo ya uke
  • homa
  • maumivu wakati wa kukojoa
  • kuvimba na vipele ukeni
  • maumivu ya tumbo chini ya kitovu na nyonga

Kama utagundua kwamba hedhi yako ni nyeusi na inaambatana na dalili mojawapo kati ya hizo juu, jua kuna kitu ndani, jichunguze.

3.Mabaki ya hedhi iliyopita

Hedhi inapokwama kutoka nje ya uke, inabaki na kugandana ndani na hivo kubadilika kuwa nyeusi.
Maumbile ya uke yanaweza kupelekea hali hii, mfano wanawake bikira wanakuwa na utando ukeni. Utando huu unaweza kuzuia flow nzuri ya hedhi na kupeleke damu nyeusi.

Mara chache tatizo laweza kuwa kubwa zaidi na kupelekea ukose hedhi. Muone daktari endapo utakosa hedhi zaidi ya siku 40 na hakuna mimba.

4.Uwezekano wa saratani ya mlango wa kizazi

Japo inatokea mara chache sana, lakini endapo unapata damu nyeusi ya hedhi, inayoambatana na kutokwa damu baada ya tendo au katikati ya mzunguko inaweza kuashiria saratani ya shingo ya kizazi.

Saratani ya shingo ya kizazi mwanzoni huwa haioneshi dalili. Pale ikifikia stage mbaya ndipo utaanza kuona dalili kama uchafu mwingi, wenye damu na unaonuka ukeni.

Dalili zingine ni pamoja na

  • kuishiwa nguvu
  • hedhi kutoka zaidi ya siku 7
  • maumivu wakati wa tendo
  • uzito kushuka kupita kiasi
  • maumivu ya nyonga
  • kuvimba miguu
  • kushindwa kukojoa vizuri na
  • kushindwa kunya vizuri

5.Hedhi nyeusi baada ya kujifungua

Baada ya kujifungua inachukua week 6 mpaka nane kwa mama kupata damu ya kwanza. Lakini kabla ya hapo mama hutokwa nna damu tangu siku ya kuzaa, na damu hii kitaalamu huitwa lochia.
Damu hii ya lochia huaanza kutoka nyingi siku za mwanzo, na badae kupungua sana. Mwanzoni damu yaweza kupitiwa na hewa ya oksijeni na kawa nyeusi.

Siku kadhaa mbele damu hii itaanza kuwa nyepesi na ykekundu au ya njano kabla ya kustope kabisa. Muone daktari endapo damu yako baada ya kujifungua inaambatana na harufu mbaya siku chache baada ya kuzaa.

6.Mimba kuharibika

Mimba nyingi zinaharbika ndani ya wiki 20 za mwanzo. Wataalamu wanasema asilimia 10 ya mimba zinazotungwa hutoka mapema kabla ya mda wa kujifungua.

Baadhi ya wanawake wanachanganya hedhi na mimba iliyoharika. Mimba inapoharbika na damu zikachelewa kutoka, yaweza kupelekea damu nyeusi ya mabonge. Unachotakuwa ni kufatilia kama utavusha hedhi kwa wiki moja na ulifanya sex, nunua UPT upime mkojo kujua kama mimba imo.

7.Ukuta wa kizazi unabomoka baada ya mimba kutunga

Sometime waweza kuchanganya damu ya mimba kutungwa na hedhi. Mimba inapojishikiza kwenye ukuta wa kizazi, inapelekea eneo husika kubomoka a damu kutoka. Japo ni mara chache sana inatokea lakini inawezekana.

Damu hii ya mimba kutungwa inatokea siku 10 mpaka 14 baada ya yai lililorutubishwa kujishikiza kwenye kizazi. Damu huisha dani ya siku chache na mara nyingi inakuwaga nyepesi, na yaweza kuwa nyeusi kwasababu inachelewa sana kutoka ukeni.

8.Hedhi nyeusi na magonjwa ya zinaa

Hedhi nyeusi ina uhusiano na maambukizi ya zinaa kama kisonono na chlamydia. Dalili zingine za magonjwa ya zinaa ni pamoja na

  • uchafu ukeni unaonuka
  • kuungua wakati wa kukojoa
  • maumivu wakati wa tendo
  • kuhisi mgandamizo eneo la nyonga
  • muwasho ukeni
  • kupata damu katikati ya mzunguko

Magonjwa ya zinaa kama yasipotibiwa mapema yanaweza kupelekea PID, ambapo ni maambukizi kwenye njia ya uzazi. PID inaweza kuathiri via vya uzazi ikiwemo mirija na kupelekea ushindwe kushika mimba ingine mapema.

Mwisho kabisa damu nyeusi yaweza kuashiria uwepo wa changamoto kwenye kizazi kama uvimbe yani fibroids na mimba kutunga nje ya kizazi.

Matibabu kwa changamoto ya hedhi nyeusi

Matibabu ya tatizo yanategemea na chanzo, hakikisha unaenda hospital endapo hujui nini kimepelekea utokwe na damu nyeusi. Tiba zitakuwa kwenye mgawanyo huu

  1. Kama kuna kifaa kimekwama ndani ya uke, daktari atakuchunguza na kukitoa haraka.
  2. Magonjwa ya zinaa mara nyingi yanatibika kwa antibiotics. Hakikisha unafatilia matibabu yote mpaka unamaliza kwani usipomaliza dawa mwili unakuwa sugu.
  3. Kama utavusha hedhi zaidi ya wiki mbili, muone daktari. Unaweza kuwa na mimba ama uchafu umeganda ukeni.
  4. Saratani ya shingo ya kizazi inatibiwa kwa muunganiko wa tiba ikiwemo chemotherapy, ,mionzi na upasuaji kulingana na ukubwa wa tatizo. Hakikisha unafanya vipimo vya mlango wa kizazi kila mwaka kujua kama kuna vihatarishi.

Lini unatakiwa kumwona daktari?

Hedhi ya kawaida inachukua 3 mpaka 7 kuisha na inajirudia baada ya siku 21 mmpaka 35. Ukipata hedhi nyeusi nje ya mzunguko wako na zaidi ya siku zako za hedhi ulozoea maana yake kuna shida.

Kama unapata damu nyeusi wakati wa ujauzito au baada ya kujifungua, au baada ya kukoma hedhi, ni muhimu kumwona daktari haraka. Yaweza kuashiria shida kubwa.

Tumia Evecare kuweka sawa hedhi yako

Evecare

Evecare ni tiba asili kutoka india. imetengenezwa kwa muunganiko wa mimea tiba na kuwekwa kwenye mfumo wa vidonge 30 tu. Kama wewe unaamini kwenye tiba asili zenye ubora na una tatizo kwenye hedhi yako, basi usiache kutumia evecare. Lengo letu kukupa evecare ni kukusaidia

  • kuweka sawa hedhi yako ianze kutoka nyekundu ya kawaida
  • kurekebisha mzunguko wa hedhi na kuuweka sawa
  • kupunguza maumivu makali ya hedhi kipindi cha hedhi

Gharama ni Tsh 75,000/= Dozi ya week mbili tu.

Bofya kusoma kuhusu: Kupata hedhi mara mbili kwa mwezi