Kwanini unaumia wakati wa kutoa shahawa
Maumivu wakati wa kutoa shahawa au kumwaga mbegu ama kutoa shahawa kitaalamu dysorgasmia au orgasmalgia ni maumivu anayoyapata mwanaume pale anapofika kileleni na kumwaga mbegu kwa mwanamke. Maumivu haya husambaa kwenye uume, korodani na maeneo ya karibu.
Usichukulie kawaida, maumivu unapomwaga mbegu yanaweza kuwa na madhara mabaya sana kiafya. Endelea kusoma makala hii kujua kwanini hutakiwi kupuuza maumivu haya
Nini kinasababisha maumivu wakati wa kumwaga mbegu.
Hapa chini ni sababu kubwa tisa kwanini mwanaume upate maumivu unapofika kileleni
1.Maambukizi kwenye tezi dume(prostatistis)
Maambukizi kwenye tezi dume yanaweza kupelekea upate maumivu makali unapopiz na pia wakati wa kukojoa. Unaweza kufikiri una UTI kumbe siyo. Dalili zingine utakazopata ni pamoja na maumivu ya tumbo na kushindwa kudindisha kabisa.
Baadhi ya changamoto zinazopelekea upate maambukizi kwenye tezi dume ni pamoja na
- Kuugua kisukari
- Kupungua kwa kinga ya mwili
- Kuvimba kwa tezi dume kupita kiasi(BPH)
- Kufanya mapenzi kinyume na maumbile
- Matumizi ya cather (kifaa kinachoingizwa kwenye njia ya haja ndogo kukusaidia kutoa mkojo)
2.Upasuaji unaweza kuleta maumivu unapomwaga mbegu
Upasuaji kwenye via vya uzazi unaweza kuleta madhara ya kiafya ikiwemo kupata maumivu unapomwaga mbegu. Moja ya upasuaji ni ule wa kuondoa tezi dume iliyoathirika sana kwa saratani. Changamoto zingime za upasuaji huu ni pamoja na uume kutosimama na kukosa hamu ya tendo la ndoa. Upasuaji mwingine unaweza kupelekea maumivu wakati wa kumwaga mbegu ni ule wa hernia.
3.Matumizi ya dawa za msongo wa mawazo
Dawa za kupunguza msongo wa mawazo zinaweza kusababisha matatizo mengi ya uzazi ikiwemo maumivu unapofika kileleni.
4.Athari ya neva(pundeal neoropathy) kwenye nyonga.
5.Saratani ya Tezi dume
Saratani ya tezi dume husababisha maumivu wakati wa kumwaga mbegu. Madhara mengine ya saratani hii ni pamoja na kushindwa kukojoa vizuri, uume kutosimama na kutoa mkojo wenye damu au mbegu.
6.Tiba ya mionzi
Tiba ya mionzi kwenye maeneo ya via vya uzazi ni chanzo cha kupata maumivu wakati wa kufika kileleni
7.Magonjwa ya zinaa
Kama una historia ya kuugua magonjwa ya zinaa kama Trichnomisis, basi hicho chaweza kuwa chanzo chako kupata maumivu unapomwaga mbegu.
8.Matatizo ya kisaikolojia na
9.Kupiga punyeto kwa muda mrefu
Lini Unatakiwa Kumwona Daktari
Weka mihadi ya kuonana na dakatri mapema endapo utagundua unapata maumivu makali kila unapiz wakati wa tendo la ndoa. Vipimo kadhaa vitaweza kugundua chanzo cha tatizo lako na ukaanzishiwa dawa mapema.
Maandalizi Kabla hujaenda hospitali
Unapojiandaa kweda hospitali kwa vipimo, jiandae kwa kipimo cha tezi dume (digital rectal exam) . Ambapo daktari ataingiza kidole sha shaada kwenye haja kubwa kuona kama tezi imekua kupita kiasi.
Jiandae kutoa historia ya changamoto yako na kujibu maswali haya
- Ni kwa muda gani umekuwa ukipata dalili za maumivu?
- Maumivu yanachukua muda gani kuisha?
- Je ukifika kileleni unatoa mbegu au hutoi chochote?
- Unapata dalili gani zingine?
- Je unaumia unapoenda haja kubwa?
- Je mkojo ni wa kawaida ukiutizama?
- Umewahi kutibiwa kwa ugonjwa saratani?
- Unaugua kisukari?
- Je familia yako ina historia ya kuugua tezi dume?
Vipimo vingine unavyoweza kufanyiwa ni pamoja na vipimo vya mkojo kujua kama kuna maambukizi. PSA test kujua kama tezi dume ni kubwa kupita kiasi ama ina saratani. Kwa kulingana na majibu ya vipimo daktari anaweza kupendekeza ufanyiwe vipimo vingine zaidi.
Matibabu
Matibabu yanategemeana na chanzo cha tatizo. Kama una magonjwa kama kisukari basi daktari atapendekeza uanze tiba ya kisukari.
Kama una maambukizi ya bakteria kwenye njia ya mkojo unaweza kupewa sindano ama vidonge vya antibiotics.
Ikiwa chanzo cha tatizo ni kuziba kwa mirija ya mbegu, daktari atapendekeza ufanyiwe upasuaji mdogo.
Kwa habari ya dawa za msongo wa mawazo daktari anaweza kukupa ushauri zaidi namna gani utumie dawa pasipo kukupa madhara. Anaweza pia kukushauri namna zingine salama za kupunguza msongo wa mawazo bila kumeza dawa.
Tiba kwa Saratani na Magonjwa ya Zina
Kama chanzo ni saratani ya tezi dume. Utafanyiwa upasuaji haraka ili kuzuia saratani kusambaa.Unaweza kuanzishiwa tiba ya mionzi na chemotherapy.
Kwa magonjwa ya zinaa kama trichonomiasis-Utatibiwa kwa antibiotics. Utashauriwa pia umlete na mwenzi wako apate tiba kwanini anaweza kukwambukiza mara ya pili.
Kama shida imeanza baada ya kutibiwa kwa mionzi, jipe muda na uwe mvumilivu kwani tiba ikiisha utarejea katika hali yako ya mwanzo.
Hitimisho
kupata maumivu wakati wa kumwaga mbegu inaweza kuwa ni dalili ya tatizo kubwa la kiafya, usichukulie poa. Hakikisha unaenda hospitali mapema upate vipimo na kuanza tiba ili ulinde heshima kitandani. Baadhi ya matatizo kama saratani na tezi dume hupona mapema endapo ukiwahi hospitali.