Maumivu ya mgongo kwa mjamzito ni malaamiko ya wanawake wengi sana wenye kutarajia kupata mtoto. Katika ujauzito wako kwa miezi mine ya mwisho ni lazima tu utakutana na adha hii na hakuna kingine cha kukipa lawama zaidi ya tumbo kukua.
Habari njema ni kwamba kuna vitu baadhi unaweza kurekebisha na kupunguza maumivu haya
Nini Chanzo cha Mumivu ya Mgongo Kwa Mjamzito?
Mabadiliko ya Homoni
Wakati wa ujauzito mwili hutoa vichocheo/homoni ambazo zinasaidia kulainika kwa maungio ya nyonga na kuachia kidogo. Kitendo hiki ni muhimu sana ili ujifungue vizuri mtoto wako.
Lakini homoni hizi huleta mabadiliko kwenye maeneo mengine ya mwili pia na kuathiri joint zingine. Katika miezi mitatu ya mwanzo kulainika huku kwa joint huathiri mpaka mgongo na kupelekea upate maumivu.
Stress ni Chanzo Cha maumivu ya mgongo kwa Mjamzito
Msongo wa mawazo katika kipindi hiki pamoja na wasiwasi inapelekea maumivu ya mgongo. Mawazo kuhusu mimba, familia kazi ama kitu chochote kile, pengine kelele za mawifi na majirani wanaokuzunguka.
Mabadiliko ya Mvutano
Kitaalamu tunaita centre of gravity yaani ni ile nguvu inayovuta kitu chochote kuelekea chini(katikati ya dunia). Mfano unaporuka juu lazima urudi chini, au ukirusha jiwe hewani lazima lirudi chini, sasa ile nguvu inayokirudisha kitu chini huitwa centre of gravity.
Mimba inapozidi kuwa kubwa ie nguvu ya kukuvuta inasogea mbele kidogo kwa sababu ya ukubwa wa tumbo. Maana yake itakubidi kubadili namna unavosimama na kukaa na kukala. Kukaa vibaya, kusimama muda mrefu au kujikunja kutakufanya upate maumivu ya mgongo
Kuongezeka kwa Uzito ni Chanzo cha Maumivu ya Mgongo kwa Mjamzito
Tumbo linapoongezeka uzito wako unaongezeka, na yabidi mgongo wako usapoti uzito huu. Hapa ndipo mgongo unapozidiwa na kuanza kuuma. Wanawake wenye uzito mkubwa kabla hata ya kushika mimba wako kwenye hatari zaidi ya kupatwa na shida hii wakiwa wajawazito pia.
Matibabu kwa Maumivu Ya Mgongo kwa Mjamzito
Haijalishi mimba yako ina ukubwa gani, fahamu tu kwamba kuna mambo waweza kurekebisha na ukapunguza adha hii. Fuata step hizi hapa chini kisha utarudi kunishukuru siku ingine
- Kuwa makini unaposimama, hakikisha unanyooka, mabega juu na kifua kikiwa kimenyooka. Unapokaa pia fanya hivo hivo usikunye kabisa mgongo nyoosha.
- Epuka kusimama kwa muda mrefu
- Ukitaka kuchukua kitu cochote kilicho chini kumbuka kuchuchumaa na siyo kuinama
- Epuka kuinua vitu vizito
- Vaa viatu vyenye soli flati, usivae kabisa high hills wakati una mimba
- Fanya mazoezi kadhaa kama yoga ili kunyoosha viungo vyako
- Lala kwa upande wa kushoto au kulia, usilale kwa mgongo, weka mto chini ya tumbo na katikati ya miguu unapolala
- Unapokaa kwenye kiti hakikisha kiti chako kinakuweka comfortable, nyoosha miguu yako usikunje.
- Pata muda mwingi wa kupumzika pale inapobidi
Lini watakiwa Kumwona Daktari
Maumivu ya mgongo ni kawaida kwa mjamzito. Lakini kama ikiwa makali sana inaweza kuwa ni kiashiria cha mimba kutishia kutoka au maambukizi ya baketia(UTI). Maumivu ya mgongo yanayoambatana na homa, mkojo kuuma au kutokwa damu iyo kitu cha kupuuzwa. Hapa ndipo unahitaji kwenda hospitali haraka kupata huduma.
3 replies on “Maumivu ya Mgongo Kwa Mjamzito”
Thank you nimepata kujuwa wife anasumbuaga sana kiasi kwamba kunipa stress mie but rightnow
Endelea kufatilia makala zetu
Asant kwa ushaur