Nini maana ya miguu kuwaka moto?
Miguu kuwaka moto ni tatizo kubwa sana kwa sasa. Maumivu haya yanaweza kuwa ya mda mfupi au yakakaa mda mrefu bila kuisha. Miguu yako itahisi hali ya kuungua na kufa ganzi. Maumivu huwa makali sana hasa nyakati za usiku.
Matibabu ya changamoto ya miguu kuwaka moto yanategemea na chazo cha tatizo lako. Endelea kusoma zaidi makala hii ili ujue chanzo cha tatizo lako na tiba sahihi inayokufaa.
Sababu 10 zinazokufanya upate tatizo la miguu kuwaka moto
1.Miguu kuwaka moto kwasababu ya kisukari-Diabetic Neuropathy
Kisukari kinapokusumbua kwa mda mrefu kinapelekea mishipa midogo ya fahamu kuathirika. Mishipa inapoathirika inakwamisha pia usafirishaji wa taarifa ndani ya mwili.
Taarifa zisiposafirishwa vyema inapelekea changamoto kwenye kuhisi matukio ya ndani na nje ya mwili. Pia kisukari kinaharibu mishipa ya damu ambayo inabeba hewa safi ya oksijeni ndani ya mwili.
Mishipa ya fahamu inaweza kuathiriwa maeneo mbalimbali ya mwili. Na athari hii inaongeza endapo una
- uzito mkubwa na kitambi
- presha ya kupanda imeongezeka
- unavuta sigara
- kunywa pombe
Aina za ganzi ya kisukari
Athari za mishipa ya fahamu kitaalamu tunaita neuropathy, lakini kuna aina za neuropathy. Aina kubwa ambayo inawatokea zaidi wagonjwa kisukari ni peripherial neuropathy.
Peripherial maana yake ni maeneo ya pembezoni, hivo ni athari ya mishipa ya fahamu iliyo kwenye viungo vya pembezoni mwa mwili. kama vidole vya miguuni na mikononi.
Dalili zingine za hii peripherial neuropathy ni pamoja na
- kuhisi mguu na mikono kufa gani
- kuhisi kama umevaa kitu cha kubana mfano wa sox
- maumivu makali ya haraka na kupotea
- kutokwa jasho jingi kupita kiasi na
- miguu na mikono kukosa nguvu
Ni muhimu sana kumwona daktari endapo umegundua una dalili za ganzi ya kisukari. Kwenye kutibu tatizo lako utatakiwa kurekebisha kwanza kisukari ili mishipa isiendelee kuathirika zaidi.
2.Matumizi ya pombe
Watu wanaokunywa sana pombe wapo kwenye hatari ya kuathirika mishipa ya fahamu, na hii kitaalamu inaitwa alcoholic neuropathy. Aina hii ya ganzi inaweza kusababisha maumivu kwenye unyayo na miguu kukosa nguvu.
Tiba kwa ganzi ya aina hii kuacha kwanza pombe na kubadili lishe yako kwa kula mlo kamili. Endapo utaacha pombe itapunguza athari zaidi na pia kuondoa zile dalili mbaya.
3.Upungufu wa lishe.
Upungufu wa Vitamin B kwenye lishe yako kunaweza kupelekea upate tatizo la miguu kuwaka moto.
Kupungukiwa damu pia inatokana na upungufu wa vitamin B.
Dalili zingine za kwamba una upungufu wa damu na kupelekea ganzi ni pamoja na kukosa nguvu, uchovu, kushindwa kupumua vizuri na kizunguzungu
4.tatizo kwenye tezi ya shingo-thyroid
Kuna changamoto mbili za tezi ya shingoni. Ni aidha tezi inafanya kazi chini ya kiwango- hypothyrpoidsm au inafanya kazi kupita kiasi-hypethyrodism. Tezi inapofanya kazi chini ya kiwango, yaweza kupelekea mishipa ya fahamu kuathirika na hivi kukufanya miguu yako iwake moto.
5.Magonjwa ya kuambukiza
Mishipa ya fahamu inaweza kuathiriwa kutokana na magonjwa mbalimbali ya kuambukiwa, na hivo kukufanya upate ganzi kwenye miguu. Magonjwa haya ni pampja na
- ukimwi
- kaswende
- mkanda wa jeshi
Kama unahisi una magonjwa haya ya kuambukiza, ongea na daktari ili aweze kukupima.
6.Fungus ya Miguu-athletes foot
Hii ni aina ya fungus ya miguu inayoambukizwa kwa kasi sana, na inaathiri unyayo, mikono na kucha pia. Ugonjwa huu pia huitwa tinea pedis.
Dalili kubwa ya fungus kwenye miguu mi kuwasha kwenye unyayo na dali zingine ni pamoja na
- malengelenge kwenye unyayo
- ngozi kunyonyoka katikati ya vidole na kwenye unyayo
- ngozi kuwa kavu pembeni ya mguu na kwenye unyayo
- kucha kugeuka rangi kuwa yeusi na nene sana kuliko mwanzo
7.Magonjwa ya figo
Kazi ya figo ni kuchuja mkojo na kutoa taka kupitia njia ya mkjo na jasho. Kama figo hazifanyi kazi vizuri, inapelekea sumu kujikusanya kwenye mfumo wako. Sumu zinapojikusanya zaweza kupelekea ganzi kwenye na miguu kuwaka moto.
Karibu asilimia kumi ya watu wenye magonjwa ya figo wanapata hili tatizo la kuvimba miguu kunakoambatana na kuwaka moto.
Wagonjwa wa figo waliopo kwenye huduma ya kusafisha damu yani dialysis, wanapta hii changamoto ya miguu kuwaka moto. Hii ni kwasababu wanakuwa na upungufu mkubwa wa virutubishi mwilini. Tiba ya kusafisha damu-dialysis inaondoa vitami B1 kwenye damu.
Kufeli kwa figo oia kunasababisha dalili hizi
- kuvimba miguu
- muwasho
- kichwa kuuma
- maumivu
- joint kuwa ngumu na kujaa maji
- kuhisi ganzi na viungo kukosa nguvu
8.Peripherial artery disease
Artery ni mishipa inayosafirisha damu yenye hewa safi ya oksijeni mwilini. Kwahivo kama damu isipofika eneo fulani la mwili, inapelekea ganzi na hali ganzi na kuwaka moto maeneo ya miguu na vidole vya mikono.
9.Matibabu ya Chemotherapy
Tiba hii inahusisha matumizi ya dawa zenye nguvu sana ili kuharbu seli za saratani. Chemotherapy ina madhara kiasi kwenye mwili, ikiwamo kuleta matokeo mabaya kama
- ganzi na kuchoma kwenye miguu na mikono
- uchovu mwingi na kukosa hamu ya kula
- misuli kulegea na
- maumivu
10.Kukaa kwenye mazingira yenye sumu
Unapofanya kazi maeneo yenye kemikali nyingi, mfano viwandani au kwenye mionzi yaweza kukupelekea uathirike mishipa ya faham na hivo kupelekea miguu kuwaka moto. Pia dawa baadhi mfano za ukimwi na kifafa zaweza kupelekea athari kwenye mishipaya fahamu.
Tiba ya nyumbani itakayokupa nafuu kwa miguu kuwaka moto
- Chovya miguu yako kwenye maji baridi au kwenye barafu kwa dakika chache kisha utoe
- Chovya miguu yako kwenye maji yenye chunvi au apple cider vinegar. Kama una kisukari muulize kwanza daktari wako kama njia hii ni sahihi
- Tumia chai ya manjano. Manjano ya kiambata cha curcumin ambacho kinapunguza maumivu kwenye neva
- Fanya masaji kwenye mguu ili kurahishisha usafirishaji wa damu.