Kwanini unapata muwasho mkunduni?
Muwasho mkunduni kwako ni hali mbaya inayokufanya ukose kabisa kujiamini. Kama wewe ni mwenye tatizo utagundua kwamba ni vigumu kujizuia usijikune pale unapokutwa na muwasho mkali.
Madakatari wakati mwingine wanaweza kushindwa kun’gamua chanzo cha tatizo lako kwa haraka, ila fahamu tu kwamba baadhi ya tabia na lishe vinaweza kupelekea upate muwasho mkunduni.
Baadhi ya vitu vinavokufanya upate muwasho mkunduni
Kutosafisha vizuri mkundu baada ya haja kubwa: Kama hujisafishi vizuri baada ya kwenda haja kubwa, mabaki ya haja kubwa yanaweza kupelekea upate muwasho. Muhimu jisafishe baada ya kujisaidia kwa maji au wipe zenye unyevunyevu kisha jikaushe kwa tishu au kitambaa laini.
Kujisafisha kupita kiasi: kusafisha mkundu kwa nguvu kwa kutumia wipes husababisha muwasho. Pia kutumia sabuni kujisafisha na manukato kwenye eneo la haja kubwa inaongeza tatizo kwani vitu hivi vinavuruga bakteria wazuri na kuharibu mazingira ya mkundu.
Lishe yako;Kama unatumia zaidi kahawa upo kwenye kundi la watakaopata muwasho mkunduni. Vitu vingine ni pamoja na chokolate, pilipili, energy drinks, beer na matunda yenye uchachu.
Chupi. Chupi yako inaweza kuwa ndio chanzo cha tatizo hasa kama ukivaa kwa muda mrefu bila kubadilisha na mwili wako ni wa kutoa jasho jingi. Anza kutumia chupi za pamba na ubadili chupi baada ya mazoezi au baada ya mihangaiko ya siku nzima.
Bawasili: kama unaugua bawasili ni lazima utapata muwasho eneo la haja kubwa. Muwasho huu hutokana na kuvimba kwa mishipa midogo ya damu eneo la mkundu. Kunywa maji ya kutosha, na kula vyakula vyenye kambakamba kwa wingi kupunguza nguvu unayotumia wakati wa kutoa haja. Nenda hospitali mapema endapo tatizo lako la bawasili litafikia pabaya.
Vidonda mkunduni: Majeraha yoyote na vidonda eneo la mkundu vinaweza kusababisha upate maumivu na muwasho. Utapata majeraha haya hasa ukiwa unapata choo kigumu kinachokufanya utumie nguvu kubwa kujisaidia mpaka kuchana mishipa midogo ya damu. Sababu ingine ya majeraha haya na kuchanika ni kuharisha kwa muda mrefu.
Fistula ya haja kubwa:Ukiwa ana fistula haja kubwa pamoja na mkojo huvuja pasipo kujizuia na kisha kusababisha upate muwasho sana. Kama unajihisi tayari una fistula nenda hospitali haraka kwani matibabu yake ni bure kabisa.
Maambukizi sehemu za siri: Maambukizi ya fangasi kwenye eneo la mkundu yanaweza kusababisha upate muwasho sana na ujisikie kujikuna.
Genital warts: hizi ni vimbe au masundosundo yanayoweza kuota eneo la ukeni, kwenye uume na hata kusambaa mpaka kwenye mkundu. Warts husababishwa na virusi aina ya papiloma(HPV). Warts zinaweza kuleta maumivu na muwasho mkali sana. Nenda hospitali haraka endapo umegundua kuna vinyama visivyo vya kawaida vimeota sehemu za siri.
Minyoo: minyoo unaweza kupata kwa kunywa maji yasio salama au kula chakula kisicho salama. Vitu vingine kama toy,vyombo vya kulia chakula na mishikio ya bafuni inaweza kupelekea upate minyoo. Ukiwa na minyoo muwasho hutokea hasa usiku pale minyoo ya kike inapotaga mayai. Unaweza kuona kwenye chupi yako au kwenye choo baada ya kujisaidia.
Wewe na Daktari Hospitalini
Daktari atakuuliza baadhi ya maswali ili kugundua chanzo cha muwasho wako mkunduni, dakari atakuuliza dalili unazopata, historia ya afya yako na pia namna unavojali afya yako.
Kama daktari atahisi kwamba waweza kuwa na minyoo atapendekeza upeleke choo maabara kwa ajili ya kipimo. Daktari anaweza pia kupendekeza ufanye kipimo cha damu kuona kama kuna maambukizi yoyote. Kama ikitokea huna tatizo basi itahitajika umuone daktari wa magonjwa ya ngozi ili akusaidie zaidi.
Nini cha kufanya kabla ya kumwona daktari
Wakati unajiandaa kwenda kumwona daktari kumweleza shida yako ya muwasho eneo la haja kubwa, kuna baadhi ya mambo ya kufanya. Mambo haya ni kama
- Kuwa na list ya dalili zote ambazo umekuwa ukizipata
- Ni kwa muda gani umekuwa ukipata dalili hizi za muwasho mkunduni
- List ya dawa zote na virutubisho ambazo umekuwa ukitumia pamoja na maswali ambayo unataka kummuliza daktari.
Maswali muhimu ya kuuliza daktari endapo utafika hospitali
- nini chanzo cha tatizo langu?
- vipimo gani natakiwa kuvifanya?
- je tatizo langu litapona?
- tiba gani zinapatika kwa ajili ya tatizo langu?
- kuna haja ya kumwona daktari bingwa?
- je una kipeperushi chochote naweza kupata kuhusu shida yangu, au unapendekeza site gani ya mtandaoni nikasome kujifunza zaidi kuhusu tatizo langu?
Tegemea pia kuulizwa maswali haya na daktari atakayekuhudumia
- je dalili zako zinatokea muda wote ama zinakuja na kuondoka?
- maumivu unayopata ni makubwa ama ya kawaida?
- je umepata kuharisha hivi karibuni?
- aina gani ya sabuni unayotumia au manukato yoyote ya kupaka?
- je kitu gani ukitumia kinapunguza muwasho mkunduni?
- kitu gani ukitumia kinaongeza tatizo lako?
- kuna mabadiliko yoyote ya mwili umepata kutokana na muwasho huu?
- je ndugu zako wengine nyumbani wanapata tatizo kama hili?
Ushauri wa kufuata kuepuka Muwasho mkunduni
- Jisafishe taratibu baada ya kujisaidia kwa kutumia maji, kisha kausha kwa kitambaa safi au pamba.
- Usijikune: Kujikuna zaidi kutafanya uvimbe . Unaweza kupaka maji ili kupunguza muwasho. Kabla ya kupaka maji hakikisha kucha zako ni fupi.
- Vaa chupi nyeupe za cotton: Chupi za cotton zinvyonza vizuri majimaji na kukfanya uwe mkavu.
- Badili lishe yako: usitumie vyakula kama pombe, pilipili, kahawa chochote, na nyanya kwani vitakufanya uharishe
- Pakaa kilainishi cha zinc oxide(unaweza kununua famasi). Paka kwenye eneo la mkundu ili kupunguza muwasho na ukavu pia.
- Kula zaidi vyakula vya kambakamba, vitakusaidia kupata choo imara kisicho cha uharo.
Tumia mafuta tiba ya black seed
Mafuta tiba haya hutengenezwa kupitia mbegu za black seed. Yanazalishwa zaidi nchini Pakistan kwa ajili ya kutibu muwasho mkunduni na bawasili. Huhitaji kuagiza nje ya nchi maana tayari tumekuletea tiba asili na salama.
Matumizi: Kutibu muwahso na bawasili yako, osha eneo la haja kubwa kwa maji kidogo yenye chunvi, kisha pakaa mafuta tiba haya mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni. Tumia hivyo kwa wiki mbili utapona.
Tembelea ofisi zetu hapa magomeni, ama ulipie tukutumie kwa mkoani.
3 replies on “Muwasho Mkunduni”
Jamani
Yes karibu
Samahani, ninasumbuliwa na tatizo la bawasiri kwa muda mrefu kwa sasa nina miaka 3 toka nimegundua tatizo na nimesha jaribu tiba mbali mbali za asili na hospitali pia lakin tatizo linajirudia kwa sasa nimekaribia kukata tamaa