Categories
Natural remedies

Hatua Tano za kusafisha meno kwa njia asili

kusafisha meno na kuwa na meno meupe
Kusafisha meno inachukua muda

Zaidi ya asilimia 18 ya watu hufisha meno yao wakati wa kupiga picha, wengi wakiogopa aibu ya kuonekana wan meno machafu. Kuwa na meno meupe ni jambo kubwa sana katika jamii yetu ya sasa. Leo nitakwelekeza hatua rahisi tano za kusafisha meno yako ukiwa nyumbani, bila kutumia dawa zenye kemikali.

Meno ya Kun’gaa ni kiashiria cha usafi

Meno yako ni kitu cha kwanza watu wanakiona wanapokutazama, ni kiashiria cha utimamu wa afya yako na chanzo chako cha kujiamini mbele za watu. Kuwa na meno ya rangi nyekundu au njano ni kiashiria kwamba hujali kabisa afya yako. Bilashaka unahitaji nawe kuwa na tabasamu mawanana mbele za watu bila kuogopa.

Baadhi ya watu, pamoja na kusafisha meno asubuhi, bado wanakuwa na utando kwenye meno. Hii ni kutokana na tabia kama za kunywa kahawa au chai na kuvuta sigara. Meno ya njano au kijivu yanaweza kuashiria tatizo kubwa zaidi la kiafya. Kusafisha meno pekee bado haitoshi kulinda afya ya kinywa, unahitaji na kurekebisha chakula unachokulana mtidno wako wa maisha.

Kwanini meno yanabadilika kuwa na wekundu ama njano?

Meno yanachafuka na kubadilika kuwa na wekundu , njano ama wakati mwingine kuwa na weusi, kwasababu ya kugandamana kwa uchafu. Pamoja na kwamba ni ngumu kwa meno kuwa na weupe ule ule miaka yote mpaka uzee, kuna sababu nyingi zinafanya meno kuchafuka na uanweza kuziepuka.

Sababu hizi ni kama

  • kunywa kahawa na chai nyeusi
  • kuvuta sigara
  • lishe mbovu ikiwemo vitu vya sukari, soda nk
  • tatizo la mdomo mkavu (mate husaidia kulinda meno)
  • kupumua kupitia mdomo na kuziba kwa njia za pua. Hali hii inapunguza kiwango cha mate mdomoni
  • matumizi ya antibitics kwa muda mrefu
  • matumizi makubwa ya vitu vyenye madini ya fluoride na
  • changamoto za kurithi

Njia asili za kusafisha meno yakawa na weupe

1.Brush meno baada ya kunywa ama kula

Njia nzuri ya kusafisha meno yako yawe meupe ni kupiga mswaki baada ya kumaliza kula ama kunywa. Japo siyo rahisi kufanya kila mara lakini inawezekana ukijizoesha. Inategemea pia na eneo ulilopo, aidha makazini ama shuleni, anza kwa kupiga mswaki kabla ya kulala. Fanya hilo zoezi kwa mwezi mmoja kila siku mpaka iwe ni tabia.

Acha kuvuta sigara, kunywa kahawa na soda kwa wingi, kula lishe nzuri ili kuepusha meno kuchafuka. Jiwekee tabia ya kunywa zaidi maji baada ya kula ama kunywa juisi yoyote, kusaidia kuepusha madhara ya kitu hicho kwenye meno.

2.Coconut oil pulling

Coconut oil pulling ni mja ya njia murua kabisa ya kusafisha bakteria wabaya mdomoni mwako na kukuacha na harufu nzuri ya kinywa sikuzote na meno meupe. Ni njia salama na ya asili isiyohitaji matumizi ya kemikali mbaya wala dawa ambazo zina madhara makubwa.

Nimekuwa nikishauri mamia ya watu na wamefanikiwa kuondoa adha hii ya kunuka mdomo na meno machafu kupitia coconut oili pulling. Wewe pia unaweza kuwa mmoja wa mashuhuda wetu kama tu utazingatia kwa makini step za kufuata.

Coconut oil pulling kama jina lake lilivyo ni kitendo cha kuvuta uchafu na bacteria ka vile sabuni inavyonyonya uchafu kwenye nguo wakati wa kufua nguo. Lakini kwenye upande wa kinywa unanyonya bacteria na uchafu kwenye meno kwa kutumia mafuta ya kupikia ya nazi.

Hatua za kusafisha meno kwa mafuta ya nazi

  1. Hakikisha unafanya oil pulling asubuhi unapoamka kabla ya kula na kunywa kitu chochote
  2. Chukua kijiko kimoja au viwili vya mafuta ya kupikia ya nazi kisha weka mdomoni, anza kuzungusha ulimi na kuyasambaza mdomo wote taratibu kwa dakika 10 mpaka 20
  3. Baada ya muda huu tema uchafu wote bila kumeza hata kidogo kisha safisha mdomo na maji, unaweza kutumia maji yenye chumvi ili kuondoa mafuta yote.
  4. Hakikisha usiteme kwenye sink tema nje ili kuzuia kuziba kwa mafuta kwenye sinki
  5. Brush meno yako kama kawaida
  6. Rudia kitendo hiki mara 3 mpaka 5 kwa week kupata matokeo mazuri

3.Apple cider vinegar

Pamoja na faida zake kwenye mapishi na kupunguza uzito, apple cider vinegar ni nzuri sana katika kutoa uchafu sugu uliogandamana kwenye meno yako. Apple vinegar inafaa sana kwa uchafu uliosababishwa na kahawa na sumu ya nicotine kwa uvutaji sigara.

Nini siri iliyopo kwenye apple cider vinegar?

ina viambata hai vya acetic acid, potasium, magnesium na viambata cvya kuchakata chakula (enzymes)ambazo zinaua bakteria wabaya pia hapohapo inachochea ukuaji wa bakteria wazuri kwenye mfumo wa chakula.

Hakikisha unatumia apple vinegar kw amuda mrefu kupata matokeo. Siyo njia ya kukuletea matokeo haraka, jipe walau mwezi mmoja kwa meno yako kuanza kun’gaa.

Matumizi: Chovya kiasi kidogo cha apple vinegar kwa kidole, kisha pakaa kwneye meno yako una usugue kwa dakika moja taratibu. Baada ya hapo brush meno yako kawaida kwa dawa uuliyozea kuitumia.

Angalizo; Vinegar ina utindikali hivo sugua meno taratibu sana unapotumia vinegar.

4.Tumia maganda ya limau au chungwa

Kama ilivyo kwa apple cider vinegar, maganda ya matunda haya yana kemikali ambazo husaisidia kuondoa uchafu kwene meno na kukuacha na tabasabu zuri. Matumizi: chukua ganda la limau au chungwa, sugua meno yako machafu kwa dakika moja, kisha osha kwa maji na upige mswaki kikawaida.

5.Mkaa

Mkaa husaidia kunasa vimelea wabaya na kufyonza sumu kwenye meno yako. Kufanya meno kuwa meupe kwa kutumia mkaa, chonya mswaki wako kwenye maji kisha pakaa unga kidogo wa mkaa na ubrush meno yako. Safisha zaidi kwenye meno machafu.

Baada ya hapo utasafisha meno yako kwa dawa ya meno. fanya zoezi hili mara tatu tu kwa wiki, sitisha zoezi kama utaisikia vibaya au kama una pumu.

Hatari ya kutumia njia za kisasa kusafisha meno

Tafiti zinaonesha kwamba kusafisha eno kupitia njia za kisasa zinaharibu na kufanya meno kuwa dhaifu. Dawa nyingi za kusafisha meno zinazouzwa famasi zina kemikali mbaya za carbamide peroxide. Kemikali hii huzalisha urea ambayo hupelekea meno kuoza na kubomoka. Kemikali hizi pia hufanya meno kuwa dhaifu na kushindwa kun’gata vitu vigumu.

Tumia njia hizi endapo tu njia asili nilizoeleza pale juu hazijakupa matokeo katika kipindi cha mwezi mmoja. Kumbuka tu kwamba njia nzuri ya kusafisha meno na kinywa chako ni kwa kula lishe bora. Kusafisha meno vizuri kila siku asubuhi na jioni, kuepuka vyakula hatarishi kama vya sukari na kuacha sigara.

16 replies on “Hatua Tano za kusafisha meno kwa njia asili”

Huwezi amin,nilikuwa na meno yenye rangi ya njano iliyochanganyikana na nyeusi lakini sasa nina white teeth weeeeh.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *