Categories
Uncategorized

Kiwango cha mayai ya mwanamke

yai la mwanamke

Mwanamke ana mayai mangapi?

Natambua una kiu sana ya kutaka kufahamu idadi ya mayai uliyonayo, na kama bado una uwezo wa kushika mimba kulingana na umri wako wa sasa. Makala hii itajibu maswal yako mengi kuhusu mayai ya mwanamke na uzazi.

Je watoto wa kike wanazaliwa na mayai?

Jibu ni ndio, watoto wa kike huzalishwa na mayai yote wanayotakiwa kuwa nayo. Hakuna mayai mapya yatazalishwa tena kwenye maisha yako kama mwanamke.

Mayai mangapi mwanamke anazaliwa nayo?

Pale kichanga kinapokuwa bado tumboni mwa mama kinakuwa na mayai karibu millioni 6. Mayai haya yanakuwa hayajapevuka na huitwa oocytes. Mpaka kufikia kuzaliwa mayai yanapungua mpaka milioni 1 mpaka 2.

Kwanini mtoto mdogo hapati hedhi wakati tayari ana mayai?

Hili ni swali zuri sana, kwamba nini sasa kinazuia mtoto asianze hedhi wakati tayai ana mayai? Mzunguko wa hedhi husubiri mpaka kipindi cha kubalahe ama kuvunja ungo. Balehe huanza pale ubongo unapoanza kuzalisha homoni ya GnRH-Gonatrophin-releasing hormone.

GnRH inachochea tezi ya pitutary ambayo huzalisha homoni ya FSH-follicle stimulating hormone. FSH ndio inachochea sasa mayai kuanza kupevuka.

Hedhi huanza kama miaka miwili baada ya matiti kuota. Wanawake wengi huvunja ungo na kuanza hedhi wakiwa na miaka 12 mpaka 15. Wachache sana huvunja ungo mapema wakiwa na miaka 8.

Mwanamke ana mayai mangapi anapovunja ungo?

Pale mwanamke anapofikia balehe, anakuwa na idadi ya mayai laki 3 mpaka laki 4. je nini kimetokea kwenye mayai mengine? Hili ndio jibu sahihi:- ni kwamba mayai mengi karibu 10000 yanakufa kila mwezi kabla ya balehe, yaani hayafikii kwenye kupevuka.

Mayai mangapi yanakufa kila mwezi baada ya mwanamke kuvunja ungo?

habari njema ni kwamba idadi ya mayai uanayokufa kila mwezi inapungua sana baada ya kuvunja ungo. Tafiti zinasema kwamba mwanamke anapoteza mayai 1000 kila mwezi baada ya kuanza hedhi/kuvunja ungo. Hii ni kama kusema unapoteza asilimia 30 mpaka 35 ya mayai kila mwezi.

Kila mwezi ni yai moja tu linapevuka na kuwa tayari kwa mimba kutunga kwenye siku za hatari. Ni mara chache sana inatokea mayai mawili yakawa tayari kwa kurutubishwa. Hapo ndipo wanapatikana mapacha wasiofanana.

Mwanamke ana mayai mangapi kwenye miaka ya 30s?

Mwanamke anapofikia miaka 32 uwezo wake wa kushika mimba unapungua sana na unashuka zaidi anapofika 37. Kuanzia miaka 35 mpaka 37 mayai yanakuwa chini ya laki 1. Hii ni sawa na kusema mayai yamebaki asilimia 3 tu ya hifadhi yote.

Mayai mangapi yanabaki kwa mwanamke wa miaka 40?

Pengine uko na miaka 40 na bado una kiu ya kushika mimba. Sasa unawaza umebakiwa na mayai kiasi gani. Tafiti zinasema kwamba kikawaida mwanamke anapofika miaka 40, idadi ya mayai inapungua chini ya 18,000/=. japo chansi ya kushika mimba iko chini, haimaanishi kwamba huwezi kushika mimba, bado inawezekana kubeba ujauzito katika umri huu.

Nini kinatokea baada ya kukoma hedhi?

Pale unapokoma hedhi na mayai kuisha, mifuko ya mayai inakoma kuzalisha homoni ya estrogen. Na hivo utaanza kupata dalili za tofauti kama ukavu ukeni, uchovu, kukosa hamu ya tendo. Endapo ulizaliwa na mayai mengi, kuna chansi kubwa ukaweza kushika mimba na ukapata mtoto hata kwenye miaka ya 40s.

Hitimisho

Umri mzuri wa kubeba mimba na kuzaa ni miaka ya 20s. Hapo ndipo mwanamke anakuwa na mayai ya kutosha na chansi ya kushika mimba ni kubwa sana. Kama unatafuta mimba kwa muda mrefu bila mafanikio, inahitaji uonane na daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake. Wote wawili me na ke mfanyiwe vipimo kujua chanzo cha tatizo.

Unahitaji maoni na Ushauri? Tuandikie kwa Whatsapp namba 0678626254. Usipige simu namba ni ya whatsapp tu

Unataka kusafisha kizazi na kuongeza uzalishaji mayai? bofya hapa upate dawa asili zenye ubora

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *