Kwanini tunasema hizi ni njia asili-natural contracepives? Ni kwa sababu hazibadili mpangilio wa homoni au vichocheo kwenye mwili. Badala yake njia hizi zinamwongoza mke na mume kutofanya ngono wakati yai limepevuka.
Yani lengo ni kutoruhusu mbegu ikalifikia yai lililokomaa kurutubishwa. Ni muhimu sana kufatilia kwa ukaribu viashiria vyote vya yai kupevuka.
Kikawaida yai hutolewa kila baada ya siku 14 kabla ya hedhi ijayo. Hapo kwenye siku 14 toa siku mbili nyuma au ongeza siku mbili mbele. Lakini kwasababu yai linaweza kuishi mpaka siku 3 au 4 baada ya kutolewa na mbegu inaweza kuishi siku mbili mpaka tano, kufanya mahesabu vizuri inabidi uzingatie kwa week na siyo kwa siku.
Njia asili za kupanga uzazi zinafanya kazi kwa asilimia mpaka 98, lakini zinataka ufatiliaji wa kila siku na kujicontrol hisia zako.
Njia ya kwanza ni calender
Hii inawafaa zaidi wenye mzunguko mzuri. Ni topic ndefu inayohitaji kusoma taratibu na kuelewa. Ni zoezi ambalo laweza kuchukua miezi miwili mpaka mia4 kulifatilia na kulizoea, kwani yatakiwa kurekodi na kufatilia matukio na mabadiliko yote ya mwili wako.
Hatua kwa hatua za kufatilia kalenda
- Kwa miezi 8 mpaka 12, rekodi siku ambayo unaanza hedhi na uhesabu siku zote za kila mzunguko. Siku ya kwanza ni ile unayoanza hedhi katika mwezi husika na hesabu mpaka siku unayoanza hedhi katika mwezi mwingine hapo mzunguko mmoja utakuwa umekamilika
- Rekodi mzunguko mfupi na mzunguko mrefu zaidi katika ufuatiliaji wako. Kupata siku yako ya kwanza ya hatari, chukua namba ya mzunguko mfupi zaidi toa 18, mfano mzunguko wako mfupi ni siku 27-18 inabaki 9.
- Kupata siku yako ya mwisho ya hatari kwenye mzunguko, chukua siku za mznguko wako mrefu toa 11. Mfano mzunguko wako mrefu ilikuwa siku 30-11 inabaki 19.Katika mahesabu hapo juu ni kwamba siku kati ya mzunguko mfupi na mrefu ndizo siku zako za hatari, kwa maaana ya kuanzia siku ya 9 mpaka siku ya 19 ndizo siku zako za hatari.
- Kama unataka usishike mimba basi usifanye ngono siku ya 9 ya hedhi mpaka siku ya 19, au utumie condomu.
Kufatilia joto la mwili-Basalm metabolic rate.
Joto la mwanamke hushuka masaa 12 mpaka 24 kuelekea mda wa ovulation, baada ya hapo joto huongezeka tena baada ya ovulation. Tukisema ovulation maana yake muda wa yai kutolewa kwenye kikonyo chake na kuwa tayari kw aurutubishaji. Mabadiliko haya ya joto ni madogo sana chini ya nyuzi moja.
Kupima joto hili tumia kipimajoto maalumu kinachopatikana famasi, na upime kila siku asubuhi kabla ya kuamka. Kutumia joto la mwili kama njia ya kujua siku za hatari, mwanamke anatakiwa asifanye ngono kwenye siku ambazo joto linashuka. Utasubiri masaa 48 mpaka 72 baada ya joto kupanda ndipo ufanye tendo.
Kufatilia ute wa uzazi.
Njia hii ya ute inataka kufatilia mabadiliko ya uteute kwenye uke katika siku tofauti za mzunguko wako. Mwanamke atazalisha ute mwingi laini, unaovutika kama yai kwenye siku za hatari. Sasa wewe kama mwanamke unatakiwa ujifunze kufatilia na kutofautisha ute huo kwa kutumia vidole viwili. Ingiza ukeni taratibu kisha fanya kama unavuta kuona kama unavutika. Kama hutaki kushika mimba basi usifanye kabisa tendo kwa siku 3 mpaka 4 tangu uone huo ute ute wa kuvutika.
Ovulation Kits
Mwanamke anaweza kutumia vifaa malumu vya kufatilia yai kupevuka. Vifaa hivi vina mfanano na kipimo cha mimba cha mkojo ya UPT. Vipimo hivi vinaangalia kiwango cha homoni ya lutenizing(LH) kwenye mkojo. Homoni ya lutenizing inaongezeka masaa 20 mpaka 48 kabla ya ovulation. Vifaa vya kupima vinapatikana kwenye famasi, unaweza kununua package yako ukaweka ndani.
Utaanza kupima siku mbili mpaka tatu kabla ya siku ambazo unafikiri yai linakarbia kutolewa. Kipimo hichi kama ilivyo kwa kile cha UPT, kinapima mkojo na kunyesha rangi nyekundu. Kama yai limeshatolewa mistari mwili iliyokolea itatokea, na kama bado mstari utakuwa mmoja mwekundu. Kama ovulation imekaribia basi mstari utakuwa umepauka.
Vipimo hivi kwa kiasi kikubwa hutumika kufatilia yai kupevuka ili mwanamke aweze kushiriki apate mimba, lakini unaweza kuvitumia pia kupanga uzazi ili usishike mimba mapema wakati hujatarajia.
Withdraw method (kuchomoa uume kabla mbegu hazijatoka)
Withdraw inahitaji mwanaume kutoa uume haraka kabla mbegu hazijatoka wakati wa tendo. Changamoto ya njia hii ni kwamba wanawaume wachache wanaweza kujizuia na wakatoa uume nje kwasababu ya hisia kali na utamu wa kufika kileleni. Lakini pia mbegu kidogo zinaweza kutoka wakati mwanaume anakarbia kilele na zikasababisha mimba. Njia hii ina ufanisi wa asilimia 75 mpaka 80 katika kuzuia mimba.
Lactational infertility.
Njia hii inamaanisha kwamba unapokuwa unanyonyesha mayai yanakuwa hayapevuki kwahivo mimba haitaingia. Wanawake wanaonyonyesha, mayai huanza tena kupevuka week 10 mpaka 12 baada ya kujifungua. Katika miezi sita ya kwanza ambapo mtoto ananyonya pasipo kula chakula kingine, njia hii inakuwa na ufanisi zaidi.
Mtoto yatakiwa anyonye walau kila baada ya masaa ma4 na usipitishe zaidi ya masaa sita bila kumnyonyesha mtoto. Hakikisha unatumia njia hii miezi 6 tu ya mwanzo baada ya kujifungua. Faida zake ni kwamba huhitaji kutumia kinga yoyote wala njia yoyote ya kemikali ili kuzuia mimba,badala yake ni kunyonyesha tu ipasavyo.
Njia hii siyo ya uhakika kutumika pasipo kuzingatia njia zingine hasa baada ya miezi 6 kuisha na mtoto kuanza kula. Mwanamke anayenyonysha anaweza kushika mimba pale mtoto akipunguziwa ratiba ya kunyonya kwa siku.
Kuosha uke na kukojoa baada tu ya tendo
Njia hii inahitaji mwanamke kila anapomaliza tendo kwenda haraka washroom na kuchuchumaa kisha kunawa na kutoa mbegu na uchafu wote ukeni. Wanawake wengi pia husimama haraka na kukojoa ili mbegu zitoke nje kabla ya kulifikia yai. Njia hizi hazina uhakika hivo hakikisha unatumia na njia ingine kuzuia mimba.
Kutofanya kabisa tendo
Hapa mwanamke na mwanaume wanaweza kuamua kutokutana kabisa ili kuepuka mimba. Hii ndio njia pekee yenye uhakika wa asilimia mia kukukinga usishike mimba ambayo hujatarajia. Badala yake kila mmoja anaweza kufanya punyeto ili kujiridhisha.