Categories
Uzazi wa Mpango

Njia asili za kupanga Uzazi

ufatiliaji wa mzunguko-kushika mimba
kupanga uzazi kupitia kalenda

Kwanini tunasema hizi ni njia asili-natural contracepives? Ni kwa sababu hazibadili mpangilio wa homoni au vichocheo kwenye mwili. Badala yake njia hizi zinamwongoza mke na mume kutofanya ngono wakati yai limepevuka.

Yani lengo ni kutoruhusu mbegu ikalifikia yai lililokomaa kurutubishwa. Ni muhimu sana kufatilia kwa ukaribu viashiria vyote vya yai kupevuka.

Kikawaida yai hutolewa kila baada ya siku 14 kabla ya hedhi ijayo. Hapo kwenye siku 14 toa siku mbili nyuma au ongeza siku mbili mbele. Lakini kwasababu yai linaweza kuishi mpaka siku 3 au 4 baada ya kutolewa na mbegu inaweza kuishi siku mbili mpaka tano, kufanya mahesabu vizuri inabidi uzingatie kwa week na siyo kwa siku.

Njia asili za kupanga uzazi zinafanya kazi kwa asilimia mpaka 98, lakini zinataka ufatiliaji wa kila siku na kujicontrol hisia zako.

Njia ya kwanza ni calender

Hii inawafaa zaidi wenye mzunguko mzuri. Ni topic ndefu inayohitaji kusoma taratibu na kuelewa. Ni zoezi ambalo laweza kuchukua miezi miwili mpaka mia4 kulifatilia na kulizoea, kwani yatakiwa kurekodi na kufatilia matukio na mabadiliko yote ya mwili wako.

Hatua kwa hatua za kufatilia kalenda

 1. Kwa miezi 8 mpaka 12, rekodi siku ambayo unaanza hedhi na uhesabu siku zote za kila mzunguko. Siku ya kwanza ni ile unayoanza hedhi katika mwezi husika na hesabu mpaka siku unayoanza hedhi katika mwezi mwingine hapo mzunguko mmoja utakuwa umekamilika
 2. Rekodi mzunguko mfupi na mzunguko mrefu zaidi katika ufuatiliaji wako. Kupata siku yako ya kwanza ya hatari, chukua namba ya mzunguko mfupi zaidi toa 18, mfano mzunguko wako mfupi ni siku 27-18 inabaki 9.
 3. Kupata siku yako ya mwisho ya hatari kwenye mzunguko, chukua siku za mznguko wako mrefu toa 11. Mfano mzunguko wako mrefu ilikuwa siku 30-11 inabaki 19.Katika mahesabu hapo juu ni kwamba siku kati ya mzunguko mfupi na mrefu ndizo siku zako za hatari, kwa maaana ya kuanzia siku ya 9 mpaka siku ya 19 ndizo siku zako za hatari.
 4. Kama unataka usishike mimba basi usifanye ngono siku ya 9 ya hedhi mpaka siku ya 19, au utumie condomu.

Kufatilia joto la mwili-Basalm metabolic rate.

Joto la mwanamke hushuka masaa 12 mpaka 24 kuelekea mda wa ovulation, baada ya hapo joto huongezeka tena baada ya ovulation. Tukisema ovulation maana yake muda wa yai kutolewa kwenye kikonyo chake na kuwa tayari kw aurutubishaji. Mabadiliko haya ya joto ni madogo sana chini ya nyuzi moja.

Kupima joto hili tumia kipimajoto maalumu kinachopatikana famasi, na upime kila siku asubuhi kabla ya kuamka. Kutumia joto la mwili kama njia ya kujua siku za hatari, mwanamke anatakiwa asifanye ngono kwenye siku ambazo joto linashuka. Utasubiri masaa 48 mpaka 72 baada ya joto kupanda ndipo ufanye tendo.

Kufatilia ute wa uzazi.

ute wa mimba

Njia hii ya ute inataka kufatilia mabadiliko ya uteute kwenye uke katika siku tofauti za mzunguko wako. Mwanamke atazalisha ute mwingi laini, unaovutika kama yai kwenye siku za hatari. Sasa wewe kama mwanamke unatakiwa ujifunze kufatilia na kutofautisha ute huo kwa kutumia vidole viwili. Ingiza ukeni taratibu kisha fanya kama unavuta kuona kama unavutika. Kama hutaki kushika mimba basi usifanye kabisa tendo kwa siku 3 mpaka 4 tangu uone huo ute ute wa kuvutika.

Ovulation Kits

kipimo cha kufatilia ovulation

Mwanamke anaweza kutumia vifaa malumu vya kufatilia yai kupevuka. Vifaa hivi vina mfanano na kipimo cha mimba cha mkojo ya UPT. Vipimo hivi vinaangalia kiwango cha homoni ya lutenizing(LH) kwenye mkojo. Homoni ya lutenizing inaongezeka masaa 20 mpaka 48 kabla ya ovulation. Vifaa vya kupima vinapatikana kwenye famasi, unaweza kununua package yako ukaweka ndani.

Utaanza kupima siku mbili mpaka tatu kabla ya siku ambazo unafikiri yai linakarbia kutolewa. Kipimo hichi kama ilivyo kwa kile cha UPT, kinapima mkojo na kunyesha rangi nyekundu. Kama yai limeshatolewa mistari mwili iliyokolea itatokea, na kama bado mstari utakuwa mmoja mwekundu. Kama ovulation imekaribia basi mstari utakuwa umepauka.

Vipimo hivi kwa kiasi kikubwa hutumika kufatilia yai kupevuka ili mwanamke aweze kushiriki apate mimba, lakini unaweza kuvitumia pia kupanga uzazi ili usishike mimba mapema wakati hujatarajia.

Withdraw method (kuchomoa uume kabla mbegu hazijatoka)

Withdraw inahitaji mwanaume kutoa uume haraka kabla mbegu hazijatoka wakati wa tendo. Changamoto ya njia hii ni kwamba wanawaume wachache wanaweza kujizuia na wakatoa uume nje kwasababu ya hisia kali na utamu wa kufika kileleni. Lakini pia mbegu kidogo zinaweza kutoka wakati mwanaume anakarbia kilele na zikasababisha mimba. Njia hii ina ufanisi wa asilimia 75 mpaka 80 katika kuzuia mimba.

Lactational infertility.

Njia hii inamaanisha kwamba unapokuwa unanyonyesha mayai yanakuwa hayapevuki kwahivo mimba haitaingia. Wanawake wanaonyonyesha, mayai huanza tena kupevuka week 10 mpaka 12 baada ya kujifungua. Katika miezi sita ya kwanza ambapo mtoto ananyonya pasipo kula chakula kingine, njia hii inakuwa na ufanisi zaidi.

Mtoto yatakiwa anyonye walau kila baada ya masaa ma4 na usipitishe zaidi ya masaa sita bila kumnyonyesha mtoto. Hakikisha unatumia njia hii miezi 6 tu ya mwanzo baada ya kujifungua. Faida zake ni kwamba huhitaji kutumia kinga yoyote wala njia yoyote ya kemikali ili kuzuia mimba,badala yake ni kunyonyesha tu ipasavyo.

Njia hii siyo ya uhakika kutumika pasipo kuzingatia njia zingine hasa baada ya miezi 6 kuisha na mtoto kuanza kula. Mwanamke anayenyonysha anaweza kushika mimba pale mtoto akipunguziwa ratiba ya kunyonya kwa siku.

Kuosha uke na kukojoa baada tu ya tendo

Njia hii inahitaji mwanamke kila anapomaliza tendo kwenda haraka washroom na kuchuchumaa kisha kunawa na kutoa mbegu na uchafu wote ukeni. Wanawake wengi pia husimama haraka na kukojoa ili mbegu zitoke nje kabla ya kulifikia yai. Njia hizi hazina uhakika hivo hakikisha unatumia na njia ingine kuzuia mimba.

Kutofanya kabisa tendo

Hapa mwanamke na mwanaume wanaweza kuamua kutokutana kabisa ili kuepuka mimba. Hii ndio njia pekee yenye uhakika wa asilimia mia kukukinga usishike mimba ambayo hujatarajia. Badala yake kila mmoja anaweza kufanya punyeto ili kujiridhisha.

Unahitaji maoni na Ushauri? Tuandikie kwa Whatsapp namba 0678626254. Usipige simu namba ni ya whatsapp tu

Categories
Uzazi wa Mpango

Je Kitanzi ni Njia Salama Kupanga Uzazi?

Jinsi ya kutumia Kitanzi
kitanzi

Kama wewe ni mwanamke unayetafuta njia gani salama ya kutumia upange uzazi wako, basi bilashaka umewaza kuhusu njia ya kitanzi. Kitanzi ni njia salama kwa wanawake wengi sana kwa sasa japo siyo wote.

Wengi inawakaubali na haina madhara makubwa ukilinganisha na njia zingine kama njiti, vidonge na sindano.

Kitanzi ni Nini

Kitanzi ama intrauterine device ni kifaa chenye umbo la T kinachoingizwa kwenye kizazi cha mwanamke ili kuzuia mimba isitunge. Kinfanya kazi kwa kuzuia mbegu ya kiume isilifikie yai lililokomaa na kulirutubisha. Kitanzi kikitumika ipasavyo uwezo wake wa kuzuia mimba ni zaidi ya asilimia 99.

Aina za Kitanzi

Kuna aina kuu mbili za kitanzi cha Copper na kile cha homoni

Kitanzi cha homoni (Hormonal IUD)

Kitanzi cha homoni kinaitwa hivo kwasababu kinatoa kichocheo kiitwacho progestin. Kazi ya kichocheo hiki ni kufanya ute wa ukeni kuwa mzito kiasi ya kuzuia mbegu kulifikia yai. Progestin pia inafanya ukuta wa kizazi uwe mwembemba sana na hivo kuzuia upandikizaji.

Kitanzi cha copper (Copper IUD)

Kitanzi cha copper kinafanya kazi kwa kuua mbegu zinazoingia kwennye kizazi kabla hazijafikia kulirutubisha yai.

Faida za kitanzi cha Copper ni kwamba

 • haivurugi mpangilio wa homoni
 • kinaanza kufanya kazi mapema tu ukiweka
 • Kinaweza kukaa mda mrefu mpaka miaka 10 na kikafanya kazi ya kuzuia mimba

Hasara zake ni pamoja na

Kupelekea upate hedhi nzito sana: Hii ni kwa baadhi ya wanawake na siyo wote. Aina hii ya kitanzi haifai kama unapataga hedhi nzito yenye maumivu makali.
Aleji ya copper: watu wenye aleji na madini ya copper njia hii haitawafaa

Ni zipi faida za Kutumia Kitanzi?

 • kinaweza kutumika kwa muda mrefu bila kubadilisha
 • huhitaji kukagua ama kufatilia mara kwa mara, ukishaweka mara moja tu kwa usahihi inatosha
 • gharama yake ni nafuu na unalipia mara moja tu
 • ni salama kutumia hata kama unanyonyesha

Ni watu gani wanapaswa kutumia kitanzi?

Wanawake wote wenye afya njema wanaweza kutumia kitanzi. Muhimu kumbuka kitanzi hakizuii kutoambukizwa magonjwa ya zinaa. Na usitumie kitanzi kama

 • unaugua ugonjwa wa zinaa ama umeugua PID hivi karibuni
 • ni mjamzito
 • una saratani ya kizazi au ya shingo ya kizazi
 • una tatizo la kutokwa damu kusiko kawaida

Je hedhi yangu itabadilika baada ya kuweka kitanzi?

Baadhi ya wanawake hupata maumivu kiasi kwenye hedhi baada ya kuweka kitanzi na hedhi kuwa nzito sana. Kwa miezi michache ya mwanzoni baadhi wanaweza kuona hedhi ikivurugika. Wanawake wengi hupata hedhi kidogo ama wengine hukosa kabisa hedhi.

Je Mwanaume Atakigusa Kitanzi Wakati wa Tendo la ndoa?

Kama kitanzi kimewekwa vizuri basi mwanaume ni ngumu kugusa kitanzi wakati wa tendo. Lakini hata kama ikitokea hivo basi haiwezi kupunguza ladha ya penzi kwasababu pia kamba fupi za kitanzi zinazobaki nje ya uke huendelea kuwa laini zaidi kadiri muda unavoenda.

Je kuna Madhara ya Kutumia kitanzi?

Kitanzi ni njia salama zaidi ya kisasa kupanga uzazi. Wanawake wengi hupata madhara madogo madogo ya kawaida kama kizunguzungu ambayo huisha ndani ya muda mfupi. Mwanzoni unapoweka kitanzi tegemea kupata maumivu kama vile yale ya hedhi.

Kama unapata maumivu makali sana ya tumbo ama kutokwa damu, tembelea hospitali mapema kupata ushauri wa dakari.

Mmoja kati ya wanawake kumi waliowekewa kitanzi anaweza kupata vimbe ndogo ndogo kwenye mayai(ovarian cyst). Kwa kisi kikubwa vimbe hizi hazina madhara na huisha zenyewe bia dawa.

PID

Kama utapata dalili za tumbo kujaa, kuvimba na maumivu makali chini ya kitovu muhimu uende hospitali haraka.
Kwa kiasi fuani matumizi ya kitanzi huongeza hatari ya kuugua PID, ambayo ni maambukizi kwenye kizazi, mirija na mifuko ya mayai.

Dalili za PID ikiwa ni pamoja na

 • maumivu wakati wa tendo
 • kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya ukeni
 • hedhi nzito kupita kiasi na homa.

Muone daktari mapema kama unaanza kupata dalili hizi ili utibiwe na kuepusha madhara zaidi ikiwemo kuziba kwa mirija.

Je kitanzi kinaweza kutoka chenyewe ?

Daktari atakuchunguza kama kitanzi hakipo sawa kila mara unapotembelea hospitali. Kitanzi kinatakiwa kishikiliwe na shingo ya kizazi. Kwa baadhi ya wanawake kitanzi kinaweza kutoka nje ya kizazi.

Hali hii hutokea hasa kama

 • hujawahi kuzaa
 • una umri chini ya miaka 20
 • umewekewa kitanzi mapema sana baada tu ya kuzaa au baada ya mimba kuharibika
 • una vimbe(fibroids) kwenye kizazi
 • kizazi chako kimeinama ama kina shape isiyo ya kawaida

Je vipi kama Nahitaji kuzaa kwa siku za baadae?

Kutumia kitanzi kwa watu wengi haitaathiri uwezo wako wa kushika mimba siku za baadae. Kama utafikia wakati unahitaji kubeba mimba ingine, tembelea hospitali onana na daktari muombe akutolee kitanzi. Baada ya hapo hedhi yako itarudi kuwa kawaida na utashika mimba mapema.

Je vipi kama sitashika mimba mapema?

Inatokea kwa wanawake wachache kupata madhara ya kitanzi, hasa kuvurugika kwa mazingira ya kizazi na hivo mimba kutoshika. Kwa grupu hili la wanawake tunawashauri kutumia hizi tiba asili ili kusafisha kizazi na kusaidia mayai kupevuka.

Asilimia 90 ya wanawake tuliowapa dawa hizi walishika mimba ndani ya miezi miwili. Kushoto ni dawa ya UCP kwa ajili ya kusafisha kizazi, ni dawa ya kuweka ukeni. Kulia Evecare ni dawa asili ya kurekebisha homoni, kuleta, ute na kusaidia mayai kupevuka.

Gharama ni Tsh 125,000/= kwa dozi hii ya wiki mbili.
Baada ya dozi utajipa miezi miwili ya kushika mimba

Makundi yasiyotakiwa kutumia Kitanzi

Japo kitanzi ni njia ya kisasa kupanga uzazi, haifai kwa kila mwanamke. Hutakiwi kutumia kitanzia endapo

 • una magonjwa ya zinaa ambayo hayajatibiwa
 • una saratani ya shingo ya kizazi na kizazi kwa ujumla
 • una matatizo kwenye kizazi chako kiasi inakuwa ngumu kwa daktari kukipachika
 • una magonjwa ini
 • una mimba

angalizo

Kuna wimbi kubwa la wajasiliamali mitandaoni wanauza vidonge fake vya evecare na ucp, tena wanauza kwa bei rahisi sana. Watu hao siyo madaktari wala siyo wataalamu wa afya na wanauza bidhaa feki ambazo ni hatari wa afya yako. Wengi wao hawana hata ofisi, ukipata madhara unakosa pa kuuliza. Kuwa makini na watu hao, wamejaa sana insta na fb

Unahitaji ushauri ama unataka tiba? Tuandikie kwa whatsapp namba 0678626254. Usipige simu namba ni ya whatsapp tu