Categories
Afya ya mwanamke na uzazi

Kipimo cha Mimba na Jinsi ya Kusoma Majibu

kipimo cha mimba
UPT

Jinsi Gani Kipimo Cha Mimba Kinafanya Kazi?

Kipimo cha mimba kinafanywa kwa kuchukua sampuli ya mkojo au damu ili kupima uwepo wa homoni inayoitwa human chorionic gonatrophin(hCG).

Mwili wako huanza kuzalisha homoni hii baada tu ya yai lililorutubishwa kujishikiza kwenye ukuta wa kizazi. Kiwango cha kuzalishwa homoni hii huongezeka na kudabo kila baada ya siku 2 mpaka3.

Aina za Vipimo vya Mimba Zinazotumika Mara kwa Mara

Kipimo cha Damu

Kinafanyika hospitali pekee, hakitumiki sana kama kile cha mkojo, na majibu yake huchukua muda zaidi, yahitaji kusubiri. Kipimo hichi kinaweza kugundua uwepo wa mimba katika kipindi kifupi sana baada ya kushika ujauzito. Kabla hata hujaanza kuona dalili, ndani ya siku 6 mpaka nane.

Kipimo Cha Mkojo

UPT ama kipimo cha mkojo waweza kufanya ukiwa nyumbani ama hospitali. Unaweza kununua kifaa cha kupima famasi ya karibu ukapima na kujua majibu pasipo mtu mwingine yeyote kufahamu. Ni kipimo rahisi kutumia na kinatoa majibu haraka sana.

Maandalizi ya kufanya kipimo cha mimba cha mkojo

Kama unafanya kipimo ukiwa nyumbani, hakikisha unazingatia yafuatayo

  • unasoma kwa uangalifu maelekezo ya matumizi, kwenye pakiti lenye kifaa cha kupimia kabla hujaanda mkojo wa kupima
  • kipimo hakijaexpire
  • pima mkojo wa kwanza wa asubuhi baada ya kupitisha hedhi yako
  • usinywe maji au kinywaji chochote kwa wingi, kwasababu itafanya homoni ya HCG kuwa kidogo na kutoonekana kwenye kipimo.

Hatua za kupima

Namna ya kupima ni kwa kukusanya mkojo kiasi kidogo kwenye kikombe, kisha unazamisha kipimo kwa muda wa dakika 1. Hakikisha usivuke ule mstari wa maximum unapozamisha kifaa kwenye mkojo.

Majibu ya Kipimo Yanasomwaje?

Vipimo vingi kama mimba ipo huonesha mistari miwili ya rangi nyekundu na mstari mmoja kama hakuna mimba. Baadhi ya vipimo huonesha alama ya chanya(+) na vingine huandika neno pregnant au not pregnant.

Hata kama mstari mmoja umefifia na mwingine umekoleza, hapo tayari kuna mimba lakini bado changa. Ukirudia tena baada ya wiki moja au mbili basi mstari utakuwa umekolea zaidi.

Nina wasiwasi na majibu nifanyeje?

Endapo hujaridhika na majibu yako, subiri tena wikik moja kisha upime kwa usahihi kama ulivoelekezwa na mtoa huduma alieyekuuzia kifaa. Pia unaweza kwena hospitali na kufanya kipimo cha damu. Kipimo cha damu kinaweza kugundua mimba hata ndani ya wiki moja tu.

Kipimo cha Mimba ni sahihi Kwa asilimia Ngapi?

Maarufu kama UPT kipimo hiki waweza kufanya ukiwa nyumbani kinaweza kukupa usahihi wa matokeo kwa ailimia 99, kama utafuata maelekezo vizuri ya upimaji.

Kipimo cha damu ni sahihi zaidi ya asilimia 99. Kumbuka usahihi wa kipimo kama umejipima mwenyewe nyumbani unategemea jinsi gani umefuata maelekezo ya kupima na umri wa ujauzito

Lini Unatakiwa Kufanya Kipimo cha Mimba?

Baadhi ya vipimo vya homoni ya HCG vinaweza kutoa matokeo hata kabla ya kukosa hedhi yaani week moja baada ya kushika mimba, lakini fahamu kwamba matokeo yatakuwa sahihi zaidi endapo utasubiri wiki moja baada ya kukosa hedhi inayofuata.

Nawezaje Kupata Kipimo cha mimba nijipime Nikiwa Nyumbani?

Unaweza kununua famasi ya karibu na ukapata maelekezo kutoka kwa muhudumu wa famasi namna ya kutumia. Ni bei ndogo tu sh elfu moja.

Unahitaji maoni na Ushauri? Tuandikie kwa Whatsapp namba 0678626254. Usipige simu namba ni ya whatsapp tu

Bofya makala inayofuata: Dalili za mimba lakini kipimo kinasoma negative

Categories
Afya ya mwanamke na uzazi Siku za hatari

Je Unaweza Kushika Mimba Kwenye Hedhi?

kushika mimba kwenye hedhi
Upt

Endapo unatafuta mimba kwa muda mrefu bila mafanikio au unataka kushika mimba haraka, ni muhimu kufatilia kwa makini mzunguko wako wa hedhi kujua zipi siku za hatari. Moja ya imani potofu sana kwa wengi ni kuamini mwanamke hawezi kushika mimba kwenye hedhi.

Japo uwezekano ni mdogo wa kushika mimba wakati wa hedhi lakini inawezekana. Hapa chini ni maelezo ya kina unayotakiwa kufahamu kuhusu kufanya tendo na kushika mimba wakati wa hedhi.

Mimba inatungwaje?

Mchakato wa kushika mimba kwa mwanamke ni moja ya maajabu makubwa sana ya uumbaji wa binadamu. Yahitaji mbegu kutoka kwa mwanaume iungane na yai kutoka kwa mwanamke.

Yai likishapevuka na kutolewa kutoka kwenye mfumo wa mayai, linaweza kushi kwa masaa 12 mpaka 48 kabla ya kuharibika. Mbegu ya amwanaume ikishatolewa inaweza kuishi ndani ya kizazi cha mwanamke kwa siku mpaka tatu mpaka tano.

Siku za hatari

Wanawake wengi hupata hedhi kila baada ya siku 28 mpaka 33 za mzunguko. Na wengi wao mayai hukomaa siku ya 14 baada ya hedhi . Siku yai kutolewa inaweza pia kuwa ya 12, 13 14 au 15, siku hizi ndizo tunaziita siku za hatari.

Kitendo cha yai kupevuka na kutolewa kwa ajili ya urutubishaji huitwa ovulation. Na endapo kama yai na mbegu vitakutana basi uwe na uhakika mimba itatungwa.

Nini kinapelekea kushika mimba kwenye hedhi?

Siku ya yai kupevuka na kutolewa inatofautiana kulingana na mzunguko wako. Baadhi ya wanawake wenye mzunguko mrefu wa siku mpaka 35, ovulation yaweza kutokea siku ya 21 . Na wanawake wenye mzunguko mfupi zaidi wanaweza kushika mimba hata siku ya 7 ya hedhi.

Sasa kwa mantiki hii, chukulia hedhi yako inachukua siku 6 kuisha. Umefanya mapenzi na mtu katika siku ya tano ya hedhi, na yai ikapevuka siku ya 7, na tunajua mbegu zinaweza kukaa siku mpaka 6 ndani ya kizazi. Maana yake unaweza ukashika mimba ukikutana na mwanaume kwenye siku za hedhi yako.

Sababu ingine ni kuchanganya bleed ya ovulation na bleed ya hedhi.

Wakati wa ovulation mwanamke anaweza kupata matone kidogo ya damu kwa siku moja . Wanawake wengi wanaweza kuhisi ni damu ya hedhi. Kufanya tendo bila kinga katika muda huu utaweza kushika mimba.

Kama unahitaji kufatilia vizuri kujua siku zako za hatari, anza kwa kuweka rekodi ya mizunguko yako ya hedhi kwa miezi walau mi4. Andika lini unaanza hedhi, unamaliza baada ya muda gani, hedhi yako ikoje?.
Ukifatilia kwa miezi kadhaa ni rahisi kujua siku zako za hatari na ukaweza kucheza salama.

Uwezekano ukoje wa kushika mimba kwenye hedhi?

Chansi ya kushika mimba kwa mwanamke unaongezeka na kupungua kulingana na mwenendo wa siku zako za yai kupevuka. Uwezekano wa kushika mimba siku ya kwanza na ya pili ya hedhi ni mdogo sana chini ya asilimia 1.

Baada ya kuanza hedhi kwenye siku ya 13 uwezekano wa kushika mimba ni karibu asilimia 9 na chansi kuongezeka zaidi siku ya ovulation.

Tumia uzazi wa mpango kuepuka kushika mimba kwenye hedhi

Endapo bado hujajiandaa kabisa kushika mimba unaweza kuamua kutumia uzazi wa mpango. Nenda hospitali, onana na daktari atakupa maelekezo ya njia zote zinazopatikana ikiwemo faida na hasara za kila njia ya kupanga uzazi.

Baada ya maelezo ya daktari, utaweza kuchagua njia sahihi ya kutumia itakayokufaa ili kuzuia kushika mimba kwenye hedhi. Kumbuka tu kwamba njia nyingi za uzazi wa mpango haziwezi kukuzuia kupata magonjwa ya zinaa.

Zitakukinga tu dhidi ya miba isiyotarajiwa. Kama huna uhakika na mwenzi wako, hakikisha unatumia kinga kama kondomu, itakusaidia kukukukinga na magonjwa ya zinaa na mimba pia.

Hitimisho

Mzunguko wa hedhi unatofautiana kwa kila mwanamke, hivo inawezekana kabisa ukashika mimba siku za hedhi. Japo chansi ya kushika mimba ni ndogo mwanzoni mwa hedhi ila kadiiri unavokarbia siku ya ovulation chansi inaongezeka.

Kama umeshajaribu kutafuta mimba kwa zaidi ya mwaka mmoja bila mafanikio, muone daktari kupata vipimo na tiba. Daktari anaweza kukwelekeza vizuri namna ya kufatilia siku za hatari ili ushike mimba mapema.
Daktari pia anaweza kukufanyia vipimo kadhaa na kukupa dawa za kuchochea upevushaji wa mayai na kuongeza chansi ya kushika mimba.

Unahitaji maoni na Ushauri? Tuandikie kwa Whatsapp namba 0678626254. Usipige simu namba ni ya whatsapp tu

Bofya kusoma makala inayofuata: Jinsi ya kugundua siku za hatari kushika mimba