Categories
Hedhi salama Menopause

Kukoma hedhi mapema

kukoma hedhi

Kukoma hedhi kitaalamu menopause ni kipindi katika ukuaji wa mawanamke ambapo damu ya kila mwezi inakata kutoka. Jambo hili hutokea hasa miaka ya 40 au wengine mpaka 50. Ni kipindi ambacho kinaambatana na mabadiliko mengine makubwa ya mwili ikiwemo kupungua hamu ya tendo, mashavu ya uke kusinyaa na mifupa kuwa dhaifu.

Kukoma hedhi mapema zaidi

Kwa wanawake wengi kukoma hedhi hata siyo jambo la kuliwazia mpaka pale utakapofikia miaka 40s au 50s. Japo mmoja kati ya wanawake 100 anaweza kukoma hedhi mapema zaidi akiwa na miaka 20s au 30s, kuliko ilivozoeleka.

Menopause inapoanza mapema zaidi kabla hujafikisha miaka 40, tunaita primary ovarian insufficiency au primary ovarian failure.

Kundi gani la wanawake wanaweza kukoma hedhi mapema zaidi?

Wakati unaanza kukoma hedhi, mifuko ya mayai yani ovary zinapunguza uzalishaji wa homoni za estrogen. Kukoma hedhi siyo kipindi kifupi, ni mlolongo wa miaka inaweza kuchukua hata miaka 5 au 10 kukoma kabisa hedhi. Utaanza kwa kukosa hedhi miezi mi3 mpaka 6 kisha baadae unakoma mwaka mzima.

Hichi kipindi cha kukosa hedhi ndicho chaweza kudumu mpaka miak 5 au 10 kabla hujakoma moja kwa moja.

Sababu nyingi zinaweza kupelekea mwanamke akome hedhi mapema kabla ya mda wake. Sababu hizi ni pamoja na

Dalili za kukoma hedhi mapema

Wanawake waliokoma hedhi mapema wanapata dalili za

Kumbuka siyo kawaida kwa mwanamke aliye kwenye umri wa kuzaa kupata dalili hizi, hivo hakikisha unamwona daktari mapema apate kupima homoni zako”

Daktari atahitaji kupima kiwango cha homoni ya estrogen na FSH kujiridhisha kama kweli umekoma hedhi.

Ushauri gani wa kuzingatia na Lishe ukiwa kwenye menopause?

Vyakula vya kutumia mara kwa mara ukishakoma hedhi

Unapojaribu kuekebiusha homoni zako zilizovurugika na kupunguza madhara ya menopause, lishe yako inatakiwa kujumuisha madini ya kutosha na mafuta mazuri. Unapokula lishe hii kwa wingi itakusaidia kuweka sawa homoni na pia kukupunguzia mafuta mabaya mwilini.

Weka akili kwamba kadri unavozeeka utahitaji kupunguza kiwango cha mlo wako kwasababu kasi ya shuguli za mwili inapungua na umri. Ni muhimu sana kujizuia vyakula vilivyosindikwa na kupendelea kula chakula safi. Vyakula vitakavyokusaidia ni pamoja na

1.Vyakula vyenye madini ya calcium kwa wingi

Mifupa kudhoofika ni moja na changamoto inayotokea baada ya kukoma hedhi. Japo mwanzoni huwezi kuona lakini madhara yake yanaweza kuonekana miaka ya baadae.

Mwili wako unajenga mifupa kuanzia ukiwa mdogo mpaka kufikia miaka 30. Baada ya hapo unaanza kupoteza mifupa. Kwa mwanamke kutokana na kupungua kwa homoni ya estrogen, kasi ya kumomonyoka mifupa inakuwa kubwa zaidi baada ya kukoma hedhi.

Ndiomaana tunashauri upendelee kula kwa wingi vyakula vyenye madini ya Calcium kama

  • maziwa
  • yogurt
  • mboga za majani za kijani kilichokolea na
  • dagaa
  • mboga zingine jamii ya kabeji kama broccoli, cauliflower na asparagus

2.Vyakula vyenye fiber/kambakamba kwa wingi

Vyakula vyenye kambakamba ni muhimu sana kwa afya ya moyo na mfumo wa chakula, pamoja na kuweka sawa uzito wako. Baadhi ya tafiti zinasema ulaji wa vyakula vya kamba kwa wingi unasaidia pia uzalishaji wa homoni ya estrogen. Homoni ambayo inapungua sana kwa walikoma hedhi.

Vyanzo vizuri vya kambakamba ni pamoja na karanga, parachichi, mbegu, maharage, nafaka, mbogamboga na matunda.

3.Mafuta yenye omega 3

Omega 3 ni kiambata kinachopatikana kwenye samaki na mbegu za maboga. Kiambata hiki kinasaidia kuimarisha moyo , kumarisha ngozi na kuzuia mwili kututumka . Mafuta haya yanapatikana zaidi kwenye samaki aina ya saladini na salmon. Tafiti zinasema kwamba kutumia omega 3 mara kwa mara kunasaidia uzalishaji wa homoni na kuzuia makali ya menopause.

4.Vyakula vya mafuta mazuri

Ni kweli kwamba vyakula vya mafuta havipandishi sukari kwenye damu ukilinganisha na vyakula vya sukari na wanga. Ndiomaana hata wenye uzito mkubwa na kitambi na wenye kisukari tunawashauri wale zaidi vyakula vya mafuta.

Pia vyakula hivi vinapunguza mpambano ndani ya mwili. Mafuta ndio yanayounda homoni zako mwilini. Hakikisha unapata mafuta mwali ambayo hayajachakachuliwa wala kuongezwa kemikali mbaya. Mafuta haya ni yale ya nazi, olive, vyakula kama nazi, parachichi, karanga ,ufuta na mbegu za maboga.

Categories
Magonjwa ya Kuambukiza

Tetekuwanga

tetekuwanga
tetekuwanga

Nini maana ya Tetekuwanga?

Tetekuwanga ni ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza. Ugonjwa unasababishwa na kirusi anayeitwa varicella-zoster. Watu wengi wanaugua tetekuwanga wakiwa wadogo, endapo hawakupata chanjo.

Mtoto anayeugua tetekuwanga anaweza kumwambukiza mtoto mwingine kwa urahisi sana. Kwa sasa tatizo siyo kubwa ukilinganisha na zamani kwani watoto sasa wanaweza kuachanjwa ili wasipate tetekuwanga.

Huwezi kuugua tetekuwanga mara mbili

Ukishaugua tetekuwanga huwezi tena kuugua maisha yako yote hata kama ukigusana na mgonjwa. Kama hujachanja unaweza kuugua tetekuwanga katika umri wowote ule.

Watu wazima wanaougua tetekuwanga wanakua wadhaifu sana na ugonjwa ukawapelekesha mno ukilinganisha na watoto. Ni bora kuugua tetekuwanga ukiwa mtoto kuliko kuugua ukubwani, au upate chanjo kabisa ili uisugue.

Tetekuwanga inaambukizwaje?

Unaweza kupata tetekuwanga kwa

  • kugusana na mgonwa mwenye tatizo
  • kuvuta hewa ya mgonjwa watetekuwanga au majimaji ya kooni na mafua
  • kugusa majimaji ya mgonjwa kwenye pua zako, mdomo na macho

Je kuna uhusiano gani kati ya tetekuwanga na mkanda wa jeshi?

Ukishaugua tetekuwanga, wale virusi wanabaki mwilini lakini hawasababishi tena tetekuwanga. Lakini siku virusi hawa wakiibuka wataleta ugonjwa mwingine unaoitwa mkanda wa jeshi ama shingles. Kwahivo mkanda wa jeshi hauambukizwi bali ni virusi wako wa tetekuwanga ulougua zamani ndo wanakuletea ugonjwa mpya.

Kumbuka watu wenye mkanda wa jeshi hawawezi kumuambukiza mtu mkdanda wa jeshi, basi wanaweza kumpa tetekuwanga, endapo huyo mtu hakuwahi kuugua tetekuwanga. Mkanda wa jeshi nao huisha wenyewe ndani ya week .

Dalili za tetekuwanga

Dalili za tetekuwanga hazijifichagi, ni rahisi sana kumtambua mgonjwa wa tetekuwanga. Dalili hizi ni kama

  • Homa
  • Kuhisi uchovu
  • kichwa kuuma
  • Maumivu ya tumbo
  • Malengelenge kwenye ngozi yanayowasha na kutoa maji
  • Makovu baada ya lengelenge kutoboka
  • Ngozi yenye madoadoa

Vipimo kugundua uwepo wa tetekuwanga

Kwa kutumia tu macho, muhudumu wa afya anaweza kugundua kwamba unaumwa tetekuwanga.

matibabu na huduma kwa mgonjwa wa tetekuwanga

Nawezaje kumsaidia mwanangu anayeumwa tetekuwanga?
Hakikisha mtoto anapata mda mwingi wa kupumzika na kunywa maji ya kutosha. tetekuwanga huwa inapona yenyewe ndani ya week 1 au mbili. Kumsaidia mtoto na muwasho unaweza kufanya haya

  • weka nguo yenye majimaji baridi kwenye lengelenge
  • hakikisha mwanao yupo eneo lenye ubaridi
  • ongea na mwanao asitoboea lengelenge kama mtoto mdogo sana mkate kucha ili ajijikune
  • unaweza kumpaka lotion maalumu au ukampa dawa zenye kiamabata cha antihistimine- nunua pharmacy
  • mwogeshe mwanao kwa maji baridi mara kwa mara. Mfute mtoto kwa taulo kama unakanda mwili, usifute kwa kusugua.

Usimpe mtoto dawa za asprin. Hizi zinaweza kumletea mtoto shida hasa mwenye homa. Kama huna uhakika dawa ipi ya kumpa mwanao, nenda pharmacy jieleze utapewa dawa sahihi.

Je kuna madhara zaidi yanaweza kutokea kwa mtoto mwenye tetekuwanga?

Changamoto kubwa zinazoweza kujitokeza kutokana na tetekuwanga ni pamoja na

  • bakteria kushambulia ngozi, damu na tishu laini
  • Nimonia- yani mapafu kujaa maji
  • mwili kupungukiwa maji kupita kiasi
  • ini kuathirika
  • damu kuganda

Nani anaweza kuugua zaidi na kulemewa na tetekuwanga?

Watu wenye afya njema, wanapougua tetekuwanga, huwa haiwapelekeshi sana. Japo wa watoto wadogo sana kuugua tetekuwanga inaweza kuwaletea shida zaidi, pia wenye mimba, wenye kinga dhaifu . Wagonjwa wa Ukimwi, saratani na wanapata tiba ya mionzi wanalemewa sana na tetekuwanga

Je tetekuwanga yaweza kuua mtu?

Ni mara chache sana tetekuwanga ikahatarisha maisha ya mtu. Watu wengi hupona mapema ndani ya wiki mbili baada ya kuugua. Japo wapo watu waliowahi kufa kwasababu ya tetekuwanga.

Je mwanangu anaweza kupata chanjo ya tetekuwanga?

Jibu ni ndio kuna chanjo ya tetekuwanga, ongea na mtoa huduma hospital atakupa maelekezo.

Je watu wazima wanaweza kuugua tetekuwanga?

Mtoto akishaugua tetekuwanga, mwili wake unapambana na virusi hao na kutengeneza kinga ya kudumu. Kinga hii inakaa mwilini miaka yote ya uhai wako, na itapambana na virusi wageni wataakaoingia siku zijazo.

Ni lini unatakiwa kumwona daktari?

Nenda hospital haraka endapo mtoto wako anapata dalili za

  • ana malengelenge kwe nye macho
  • kuumwa sana kichwa
    • ana malengelenge makubwa yanayotoa usaha
    • anashindwa kupumua vizuri

    Bofya kusoma kuhusu: kwanini unaugua kaswende sugu