Categories
Afya ya mwanamke na uzazi Hedhi salama

Hedhi Mara Mbili Katika Mwezi

hedhi mara mbili katika mwezi
kalenda ya hedhi

Mzunguko wa hedhi

Hedhi ya kawaida inachukua mzunguko wa siku siku 21 maka 35. Nikisema mzunguko namaanisha jumla ya siku kuanzia ulipopata hedhi mwezi mmoja, mpaka utakapopata hedhi tena katika mwezi unaofata. Makala hii itaongelea tatizo la kupata hedhi mara mbili katika mwezi na nini cha kufanya.

Japo siyo kawaida kupata mizunguko tofauti kila mwezi. Baadhi ya mizunguko yaweza kuwa mifupi au mirefu kuliko mingine, na hivo kupelekea upate hedhi mara mbili katika mwezi.

Tazama na dalili zingine

Katika nyakati nyingi kupata hedhi mara mbili ndani ya mwezi mmoja yaweza isiwe tatizo. Lakini kama inatokea kwa kujirudia ni muhimu kutazama na dalili zingine zinazoambatana. Endelea kusoma zaidi ili kujifunza kuhusu changamoto ya hedhi mara mbili katika mwezi

Hedhi mara mbili katika mwezi kwa mara ya kwanza

Watu wenye mzunguko mfupi mara nyingi sana wanapata hedhi mwanzoni na mwishoni mwa mwezi. Kwa mtu mwenye mzunguko wa kawaida wa siku 28 au zaidi, akipata hedhi mara mbili lazima ashituke.

Kumbuka hedhi isipotoka kwa wakati inaashiria changamoto ya kiafya. Ni ni rahisi sana kuchanganya hedhi na bleed ingine. Waweza kudhani ni hedhi kumbe unatokwa na damu tu kutokana na changamoto fulani.

Changamoto zinazoweza kupelekea bleed isiyo ya hedhi ni pamoja na

Mimba- mimba inapojishikiza kwenye ukuta wa kizazi yaweza kupelekea bleed.Ugonjwa wa zinaa: magonjwa ya ngono yanaweza kupelekea upate bleed kidogo na kutokwa na uchafu usio wa kawaida ukeni.

Mimba kuharibika-Mimba inapoharbika inaambatana na maumivu makali na kutokwa na mabonge ya damu. Ni muhimu kwenda hospitali mapema ikiwa una mimba na umeanza kuona damu.

Mabadiliko ya uzito– Mazoezi kupita kiasi na mabadiliko makubwa ya uzito wa mwili yanaweza kupelekea hedhi mara mbili.

Uzazi wa mpango wa kisasa-Hedhi kuvurugika na kutoka mara mbili inatokea sana kwa wanaotumia njia za kisasa kuzuia mimba , mfano sindano, njiti na vidonge

Vimbe kwenye mlango wa kizazi na ukuta wa kizazi: Hizi ni vimbe ambazo siyo saratani kwenye kuta za mlango wa kizazi na kwenye ukuta wa kizazi, ambazo zaweza kupelekea upate hedhi zaidi ya mara moja.

Saratani ya mlango wa kizazi: kutokwa damu yaweza kuashiria uwepo wa saratani

Tofauti kati ya damu ya hedhi na bleed ya tatizo la via vya uzazi

Hizi dondoo zitakusaidia kujua kama damu unayopata ni hedhi ama siyo hedhi

Kama ni hedhi ya kawaida itakulazimu kubadili pedi au tampon kila baada ya masaa kadhaa. Na damu kawaida inakuwa nyekundu nzito au ya kungaa, brown au pink

Kama ni matone ya damu ambayo siyo hedhi, haitahitaji kubadili pedi au tamponi mara kwa mara, unaweza kutumia pedi moja tu kwa siku. Damu yake yaweza kuwa ya pick, brown na inakata mapema ndani ya siku moja au mbili

Chanzo kikubwa cha mzunguko mfupi na hedhi mara mbili katika mwezi

Nini kinapelekea hedhi mara mbili katika mwezi? inaweza kutokana na mzunguko mfupi ama changamoto ya kiafya inayopelekea bleed ukeni.

Baadhi ya mambo yanayopelekea hedhi mara mbili ni pamoja na

1.Kukaribia kukoma hedhi-Perimenopause

Perimenopause ni kipindi ambacho mwanamke anakarbia kukoma hedhi yake, wakati ambapo kunatokea mabadiliko makubwa ya homoni. Kipindi hichi waweza kupata hedhi mara mbili ndani ya mwezi mmoja. Perimenopasue inatofautiana kwa kila mwanamke.

Kuna wengine inachukua hata miaka 10 ndipo hedhi inakoma. Wakati wa kipindi hiki kuelekea kukoma, waweza kupata hedhi nzito sana, kuvusha miezi kadhaa bila hedhi, mzunguko kuwa mrefu , hedhi nyepesi sana. Menopause ndio kukoma hedhi kwenyewe. Mwanamke anakoma hedhi endapo atakosa hedhi kwa miezi 12 mfululizo.

2.Fibroids

Hizi ni vimbe zinazotokea kwenye kizazi. Ni vimbe zisizo saratani, na zaweza kuleta hedhi nzito, au ukavusha kabisa hedhi. Dalili zingine za fibroids ni pamoja na

 • kupata mkojo mara kwa mara
 • kuhisi uzito eneo la nyonga
 • maumivu chini ya mgongo
 • maumivu wakati wa tendo

Daktari atagundua kama una fibroids kwa kukufanyia kipimo cha utrasound.

3.Magonjwa ya tezi ya shingoni

Tezi huu huitwa thyroid, inakaa shingoni na ina umbo kama la kipepeo. Kazi ya tezi hii ni kuzalisha homoni ambazo zinaratibu mpangilio wa hedhi yako. Dalili za kwamba kuna tatizo kwenye tezi ya shingo ni pamoja na

 • kuhisi baridi mda wote
 • kuongezeka uzito
 • tumbo kujaa
 • kupungua mapigo ya moyo
 • kutoka na damu nyingi ya hedhi

Kwa upande mwingine ikiwa tezi yako inafanya kazi kupita kiasi utaanza kupata dalili hizi

 • kuhisi joto mda wote
 • macho kuvimba
 • moyo kwenda mbio sana
 • kukosa usingizi
 • kuharisha na
 • macho kuvimba

Hakikisha unaenda hospital, endapo utaanza kupata dalili hizi za tezi ya shingo.

Madhara zaidi ya kupata hedhi mara mbili

Watu wanaotoka kwenye familia zenye historia ya kuugua vimbe kwenye kizazi na kukoma hedhi mapema , wapo kwenye hatari zaidi ya kupata hili tatizo la hedhi mara mbili katika mwezi. Moja ya changamoto utakayopata kutokana na kupata hedhi mara mbili ni kupungukiwa damu. Dalili hizi zinaonesha kwamba umepungukiwa na damu.

 • mwili kuchoka sana
 • kizunguzungu
 • mapigo ya moyo kubadilika
 • kukosa pumzi
 • kuumwa sana kichwa

Je kuna umuhimu wa dawa kutibu hedhi mara mbili?

Hedhi mara mbili siyo tatizo ikiwa mzunguko wako ni mfupi. Japo ni muhimu sana kumuona daktari endapo kama utapata dalili hizi hapa chini

 • hedhi mara mbili kwa miezi mi2 au mi3 mfululizo
 • maumivu wakati wa tendo
 • hedhi nzito ya mabonge
 • damu ya kuganda
 • maumivu chini ya kitovu hasa kama maumivu hayaishi
 • maumivu makali kwenye hedhi
 • kupata matone ya damu katikati ya mzunguko ambayo yanajirudia mwezi unaofata

Kwa binti mdogo hakuna tatizo

Matibabu ya tatizo hili ya kupata hedhi mara mbili katika mwezi mmoja, yanategemea na chanzo cha tatizo. Watu wenye mzunguko mfupi au wanaopata hili tatizo kwenye miaka ya mwanzo ya kubalehe, hawahitaji tiba tatizo laweza kuisha lenyewe.

Tiba inalenga Chanzo cha Tatizo

Daktari anaweza kupendekeza akupe dawa za kurekebisha homoni zile za kupanga uzazi. Kama tayari unatumia dawa za kisasa za uzazi wa mpango, na unahisi ndio chanzo cha tatizo, mjulishe daktari ili akubadilishie njia ingine.

Kwa tatizo la tezi ya shingo: daktari anaweza kupendekeza vipimo zaidi na kukupa dawa kwa tatizo hili

Kama unakarbia kukoma hedhi: kuna dawa za hormone utapewa kupunguza ukali wa tatizo

Kwa vimbe yani fibroids: daktari anaweza kukupa dawa, ama akapendekeza upasuaji, kulingana na ukubwa wa tatizo.

Kubadili mtindo wako wa maisha pia utasaidia kurekebisha homoni zako, mfano kama una uzito mkubwa na kitambi, anza kufanya mazoezi na kupunguza vyakula vya sukari.

Bofya kusoma: Njia salama za kupunguza maumivu kipindi cha hedhi

Categories
Hedhi salama Siku za hatari

Kumeza P2, Maswali na Majibu

vidonge vya p2
vidonge vya p2 kuzuia mimba

Nini Kinatokea P2 isipofanya kazi?

P2 ni vidonge vya kumeza kwa dharula tu ili kuzuia mimba isiyotarajiwa endapo hukutumia kinga. Lakini unaweza kuwa unajiuliza je kuna uhakika gani kama p2 zinakusaidia kuzuia mimba? Uwezo wake ni asilimia ngapi? Na vipi kama haitafanya kazi nini kitatokea?

Hapa chini kuna majibu ya maswali yako yote kuhusu p2 kutoka kwa watalamu na wabobezi wa afya ya uzazi. Tusome zaidi.

Je unaweza kushika mimba hata baada ya kumeza p2?

P2 ama morning after pill au plan B, ni dawa zilizopo kwenye kundi la levonorgestrel. Ambazo kazi yake ni kuzuia usishike mimba baada ya tendo endapo umesahau kinga, au kondomu imepasuka au ulifanya tendo ukiwa umelewa.

Dawa zinafanya kazi kwa kuzuia yai kutolewa kwenye ovary wakati wa ovulation, na hivo kuzuia mbegu na yai zisikutane kufanye kiumbe.

Muda sahihi wa kumeza p2 ni upi?

Kumbuka mbegu inapoingia kwenye uke inachukua saa 12 mpaka 48 kwenda kurutubisha yai. Na dawa inafanya kazi vizuri endapo utameza ndani ya masaa 12 baada ya kufanya tendo. Ukimeza ndani ya masaa 24 chansi ya kuzuia mimba ni asilimia 95 na zaidi.

Ukimeza kuanzia masaa 48 mpaka 72, yani siku 2 mpaka 3 baada ya kufanya tendo, chansi ya kuzuia mimba inapunguza mpaka asilimia 61 pekee. Kumbe sasa uwezekano wa kushika mimba hata kama ulimeza p2 unaongezeka kadiri unavochelewa kumeza kidonge.

Dalili gani nitapata baada ya kumeza p2?

Baada ya kumeza p2 tegemea kupata dalili ama side effects kama

 • kichefuchefu
 • maumivu ya tumbo
 • kichwa kuuma
 • kizunguzungu na
 • kutapika

Kama utatapika ndani ya masaa mawili bada ya kumeza dawa, unatakiwa umeze tena kidonge kingine ama utumie njia ingine ya kuzuia mimba kama condom.

Je uzito mkubwa na kitambi ni kikwazo cha p2 kufanya kazi?

Jibu ni ndio, tafiti zinaonesha kwamba wanawake wenye uzito mkubwa na kitambi wapo kwenye hatari ya kushika mimba hata kama wametumia p2 vizuri. Inashauri kama wewe ni mnene tumia kitanzi cha copper kama njia ya kisasa kuzuia mimba.

Dawa Zinapelekea P2 isifanye Kazi

Ni muhimu pia kujua kwamba baadhi ya dawa zinaweza kuathiri utendaji wa P2. Dawa kama za fungus, HIV, dawa za kifafa na baadhi ya antibiotic,. Sasa unapoenda dukani kununua P2, hakikisha unamweleza muhudumu hali yako ya kiafya na dawa unazotumia kwa muda huo.

Je p2 zinafanya kazi kwenye ovulation?

Dawa za p2 zinafanya kazi vizuri kabla ya ovulation, yani kabla yai halijatolewa. Hii ni kwasababu inazuia kabisa yai kutolewa kwenye ovari na hivo kuzuia urutubishaji.

Lakini hata kama yai limeshatolewa, kidonge kinazuia mbegu kulifikia yai, kwa kufanya ute wa ukeni uwe mzito sana kiasi mbegu zinashindwa kuogelea.

Kama pengine umechelewa kumeza kidonge, na tayari yai limerutubishwa, basi kidonge kinazuia kiumbe kujishikiza kwenye ukuta wa kizazi na hivo mimba haitakuwepo.

Je kuna madhara kwa mjamzito kumeza P2?

Ni muhimu pia kujua kwamba, endapo umemeza kidonge bahati mbaya bila kujua kumbe kuna mimba, haitakuwa na madhara. Kiumbe kitaendelea kukua pasipo shida.

Maelezo ya Mwisho Kuhusu P2

Meza p2 kwa emergency tu na siyo kila siku. P2 ziapelekea hedhi kuvurugika na homoni kuvurugika. Tumia kwa tahadhari na usizoee kuzimeza kila siku.

Endapo unatafuta njia ya kupanga uzazi ya mda mrefu, tafadhali tembelea hospitali uonane na muhudumu akupe maelekezo.

Soma hapa ikiwa hedhi yako Imevurugika na unataka kuiweka sawa.

Categories
Afya ya mwanamke na uzazi Hedhi salama

Maumivu ya Tumbo la Chango

tumbo la chango

tumbo la chango

Chango ni kitu gani hasa?

Tumbo la chango au mchango, wengi husema wakimaanisha maumivu makali ya tumbo kipindi cha hedhi. Kitalamu maumivu haya huitwa dysmenorrhea, ikimaanisha maumivu kutokana na kujikaza kwa ukuta wa kizazi ili ubomoke na kutoa damu kipindi upo kwenye hedhi.

Aina za tumbo la chango

Kuna aina kuu mbili za maumivu haya ya hedhi ama mchango, ambayo ni primary dysmenorrhea na secondary dysmenorrhea.

Primary Dysmenorrhea (Tumbo la Chango la kawaida)

Chango hili la uzazi ni yale maumivu ya kawaida yanayokupata kila mwezi kwenye hedhi na hayatokani na ugonjwa wowote. Maumivu haya huanza siku moja ama mbili kabla hujapata hedhi yako. Waweza kuhisi maumivu kwenye nyonga, kiuno na tumbo pia.

Pia chango la namna hii huchukua masaa 12 mpaka 73 yani siku 3 kuisha, na inaambatana na dalili zingine kama kichefuchefu na kutapika na hata kuharisha. Chango la namna hii huwa linapungua kadiri unazozeeka ama pale utakapozaa.

Secondary Dysmenorrhea (Tumbo la Chango lisilo Kawaida)

Chango lako linaposababishwa la ugonjwa fulani kwenye via vya uzazi. Chango hili huanza mapema zaidi kwenye mzunguko hata wiki kabla na inachukua mda mrefu sana kuisha. Mara nyingi chango hili halina dlaili za kuchefuchefu, kutapika kukosa nguvu na kuharisha.

Nini kinapelekea upate maumivu makali sana kwenye hedhi?

Maumivu hutokea pale kemikali inayoitwa prostaglandin inapofanya ukuta wa kizazi kujikaza. Ukuta wa kizazi ambapo mtoto hujishikiza na kukua,umetengenezwa kwa misuli, na unajikaza kwenye hedhi ili kubomoka kutoa damu isiyohitajika.

Ukuta unapojikaza sana, unaleta mgandamizo kwenye mishipa ya karibu ya damu, na hivo kupunguza kiwango na hewa safi ya oksijen kwenda kwenye misuli. Na misuli inapokosa hewa ndipo unapata maumivu makali.

Chango la uzazi kutokana na ugonjwa

Chango hili laweza kutokea kwa kusababishwa na ugonjwa fulani, changamoto hizi ni pamoja na

 1. Endometriosis: Changamoto ambapo kuta za kizazi zinakua na kwenda nje ya kizazi. Tishu hizi nyakati za hedhi zitapelekea maumivu makali na kuvimba.
 2. Adenomysis: Hili ni tatizo ambapo kuta za kizazi zinakua kuelekea kwenue misuli ya kizazi. Tatizo hili kaweza kupelekea kizazi kutanuka na hivo kuletea bleed nyingi yenye maumvu
 3. PID: Haya ni maambukizi ya bakteria kwenye njia ya uzazi. PID yaweza kuleta maumivu makali chini ya kitovu, kwenye tendo na maumivu nyakati za hedhi yani chango.
 4. Fibroids: Hizi ni vimbe ambazo siyo za saratani ndani au nje ya kizazi, zinazopelekea chango kali sana
 5. Cervical stenosis: Hiki ni kitendo cha mlango wa kizazi kusinyaa na hivo kuzuia damu kutoka kwa kasi nzuri hivo kuleta maumivu ya chango kwenye hedhi.

Vipimo: Utajuaje kama Chango lako la kawaida au ni hatarishi?

Kama chango lako linachukua zaidi ya siku 3, hakikisha unaenda hospitali kufanyiwa vipimo. Kumbuka aina zote za chango zinaweza kutibiwa hospital na hata kwa tiba asili. Muhimu kwanza ni kujua nini kipo nyuma ya chango lako.

Kwanza kabisa daktari atakwambia ujieleze dalili zote unazopata kwenye hedhi pamoja na mzunguko wako ukoje. Pili daktari atakufanyia vipimo ndani ya via vya uzazi(pelvic exam) ambapo ataingiza kifaa ukeni kucheki kama kuna hali yoyote isiyo ya kawaida kwenye uke, mlango wa kizazi na kizazi chenyewe.

Daktari anaweza pia kuchukua kiwango cha majimaji kwenye uke na kupeleka maabara kwa ajili ya vipimo zaidi.

Nini kinatokea kama kuna ugonjwa?

Kama daktari atahisi pengine kutokana na dalili zako una chango la ugonjwa, hapo utafanyiwa utrasound. Na ikionekana kuna shida, daktari atajikita zaidi kukutibu tatizo husika.

Nini cha Kufanya ili Kupunguza Maumivu ya Chango kwa Muda

Kuna njia nyingi ambazo husaidia kupunguza maumivu ya hedhi ambazo unaweza kutumia ukiwa nyumbani kwako kabla ya kwenda hospitali. Kama maumivu ni makali sana unaweza:-

 • Kumeza dawa za kukata maumivu kama ibuprofen kwa ahueni ya haraka. Angalizo: dawa za maumivu isiwe ni nia ya kutumika kila mara kwani madhara yake ni makubwa kiafya, dawa hizi zitumike kwa uangalifu.
 • Tumia maji ya uvuguvugu kukandakanda mahali pa tumbo la chini
 • Epuka kuvuta sigara na kunywa pombe kipindi cha hedhi
 • Usitumie vinywaji na vyakula vyenye caffeine mfano majani ya chai na kahawa
 • Fanya masaji kwenye upande wa chini wa mgongo na sehemu ya tumbo la chini.
 • Pata muda mwingi wa kupumzika

Weka ratiba ya kufanya mazoezi mara kwa mara: Tafiti zinasema wanawake wanaofanya mazoezi hupunguza maumivu ya hedhi kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na wasiofanya mazoezi.

Lini natakiwa Kumwona Daktari?

Chango linapokuwa kali sana linapelekea baadhi ya wanawake washindwe kufanya kazi zao na kushindwa kwenda darasani. Huhitaji kabisa kuvumilia mateso ya namna hii, unahitaji kuishi vizuri na kufurahia maisha. Kama maumivu hayavumiliki hakikisha unaenda hospital haraka.

Jua mzunguko wako

Ni muhimu sana kujua mzunguko wako, pia ujue maumivu huwa yanaanza siku ngapi kabla ya hedhi. Kama chango linaambatana na dalili zingine mfano maumivu makali ya kichwa, bleed nzito sana na nyingi, nenda hospitali.

Je Tumbo la Chango Linapelekea Ugumba?

Kama tulivoona kwamba chango siyo ugonjwa bali ni dalili za maumivu makali ya tumbo la hedhi. Sasa kama unapata chango la kwanza (primary amenorrhea) hapo hakuna kikwazo cha kushika mimba. Lakini kama chango lako ni ile aina ya pili yani secondary amenorrhea, hapo lazima kuwe na kikwazo kushika mimba mapema.

nini ufanye kama umetafuta mimba mda mrefu bila mafanikio?

Endapo wewe na mme wako mmetafuta mimba kwa zaidi ya mwaka mmoja, nendeni hospitali wote wawili kupimwa kujua chanzo cha tatizo. Mwanamke utapima mirija, kizazi na homoni na mwanaume atapimwa mbegu kuona kama zina hitilafu.