Kwanini unapata hedhi nyeusi?
Wanawake wengi wanaanza hedhi baada ya kuvunja ungo miaka 12 na 13, ikiwa hakuna tatizo lolote la kiafya. Hedhi ni damu inayotoka kila mwezi baada ya ukuta wa kizazi kubomoka, endapo mimba haikutungwa. Rangi na mwonekano wa hedhi yako ni kiashiria kikubwa kuhusu mwenendo wa afya yako ya uzazi.
Kwenye makala hii utajifunza
- chanzo cha hedhi kuwa nyeusi
- tiba ya tatizo na
- lini unatakiwa umwone daktari
Mabadiliko ya rangi ya hedhi
Rangi ya hedhi yako inaweza kubadilika kutoka kwenye nyekundu ya kungaa, chungwa, brown na pia nyeusi. Ni muhimu kutambua kwamba hedhi nyeusi, siyo kwamba inakuwa nyeusi hasa hapana. Ni ile hali ya weusi usiokoleakama vile damu ilopigwa na upepo ikaganda.
Sometime hedhi nyeusi yaweza kuashiria changamoto fulani ya kiafya na ndiomaana tumeandika makala hii ujifunze.
Chanzo cha hedhi nyeusi
Damu nyeusi ya period inachukua muda mrefu sana kutoka nje ya kizazi, na hivo kupitiwa na hewa. Kitendo huitwa oxidation, yani damu kuachanganyika na hewa na kuifanya iwe nyeusi au ya brown, sawa na rangi ya kahawa.
Hedhi nyeusi na na kutokwa uchafu ukeni mara nyingi siyo ishu kubwa ya kukuletea mawazo. Uke unajisafisha kila siku na hedhi yaweza kutokea ukapata nyeusi mara chache. Pamoja na hivo unatakiwa kufatilia afya yako na aina za uchafu unaotoka ukeni.
Sababu 8 zinazofanya upate hedhi nyeusi
1.Hedhi nyeusi kuashiria mwanzo au mwisho wa hedhi
Speed ya kutoka damu inakuwaga ndogo sana mwanzoni na mwishoni mwa hedhi. Hedhi inavochelewa zaidi kiutoka ndipo uwezekano ni mkubwa ikapitiwa na hewa ya oksijeni na kuwa nyeusi.
2.Kuna Kitu kimekwama ukeni
Hedhi nyeusi sometime inaweza kuashiria uwezo wa kitu ukeni kilichokwama, vitu hivi ni kama condom, kitanzi, sex toy, sponge na tampon. Damu hii isipotoka inafanya uke kuvimba kwa ndani na kupelekea maammbukizi.
Dalili hizi zinaashiria kwamba tayari umepata maambukizi ukeni na kwenye kizazi
- kutokwa uchafu unaonuka sana ukeni
- muwasho maeneo ya uke
- homa
- maumivu wakati wa kukojoa
- kuvimba na vipele ukeni
- maumivu ya tumbo chini ya kitovu na nyonga
Kama utagundua kwamba hedhi yako ni nyeusi na inaambatana na dalili mojawapo kati ya hizo juu, jua kuna kitu ndani, jichunguze.
3.Mabaki ya hedhi iliyopita
Hedhi inapokwama kutoka nje ya uke, inabaki na kugandana ndani na hivo kubadilika kuwa nyeusi.
Maumbile ya uke yanaweza kupelekea hali hii, mfano wanawake bikira wanakuwa na utando ukeni. Utando huu unaweza kuzuia flow nzuri ya hedhi na kupeleke damu nyeusi.
Mara chache tatizo laweza kuwa kubwa zaidi na kupelekea ukose hedhi. Muone daktari endapo utakosa hedhi zaidi ya siku 40 na hakuna mimba.
4.Uwezekano wa saratani ya mlango wa kizazi
Japo inatokea mara chache sana, lakini endapo unapata damu nyeusi ya hedhi, inayoambatana na kutokwa damu baada ya tendo au katikati ya mzunguko inaweza kuashiria saratani ya shingo ya kizazi.
Saratani ya shingo ya kizazi mwanzoni huwa haioneshi dalili. Pale ikifikia stage mbaya ndipo utaanza kuona dalili kama uchafu mwingi, wenye damu na unaonuka ukeni.
Dalili zingine ni pamoja na
- kuishiwa nguvu
- hedhi kutoka zaidi ya siku 7
- maumivu wakati wa tendo
- uzito kushuka kupita kiasi
- maumivu ya nyonga
- kuvimba miguu
- kushindwa kukojoa vizuri na
- kushindwa kunya vizuri
5.Hedhi nyeusi baada ya kujifungua
Baada ya kujifungua inachukua week 6 mpaka nane kwa mama kupata damu ya kwanza. Lakini kabla ya hapo mama hutokwa nna damu tangu siku ya kuzaa, na damu hii kitaalamu huitwa lochia.
Damu hii ya lochia huaanza kutoka nyingi siku za mwanzo, na badae kupungua sana. Mwanzoni damu yaweza kupitiwa na hewa ya oksijeni na kawa nyeusi.
Siku kadhaa mbele damu hii itaanza kuwa nyepesi na ykekundu au ya njano kabla ya kustope kabisa. Muone daktari endapo damu yako baada ya kujifungua inaambatana na harufu mbaya siku chache baada ya kuzaa.
6.Mimba kuharibika
Mimba nyingi zinaharbika ndani ya wiki 20 za mwanzo. Wataalamu wanasema asilimia 10 ya mimba zinazotungwa hutoka mapema kabla ya mda wa kujifungua.
Baadhi ya wanawake wanachanganya hedhi na mimba iliyoharika. Mimba inapoharbika na damu zikachelewa kutoka, yaweza kupelekea damu nyeusi ya mabonge. Unachotakuwa ni kufatilia kama utavusha hedhi kwa wiki moja na ulifanya sex, nunua UPT upime mkojo kujua kama mimba imo.
7.Ukuta wa kizazi unabomoka baada ya mimba kutunga
Sometime waweza kuchanganya damu ya mimba kutungwa na hedhi. Mimba inapojishikiza kwenye ukuta wa kizazi, inapelekea eneo husika kubomoka a damu kutoka. Japo ni mara chache sana inatokea lakini inawezekana.
Damu hii ya mimba kutungwa inatokea siku 10 mpaka 14 baada ya yai lililorutubishwa kujishikiza kwenye kizazi. Damu huisha dani ya siku chache na mara nyingi inakuwaga nyepesi, na yaweza kuwa nyeusi kwasababu inachelewa sana kutoka ukeni.
8.Hedhi nyeusi na magonjwa ya zinaa
Hedhi nyeusi ina uhusiano na maambukizi ya zinaa kama kisonono na chlamydia. Dalili zingine za magonjwa ya zinaa ni pamoja na
- uchafu ukeni unaonuka
- kuungua wakati wa kukojoa
- maumivu wakati wa tendo
- kuhisi mgandamizo eneo la nyonga
- muwasho ukeni
- kupata damu katikati ya mzunguko
Magonjwa ya zinaa kama yasipotibiwa mapema yanaweza kupelekea PID, ambapo ni maambukizi kwenye njia ya uzazi. PID inaweza kuathiri via vya uzazi ikiwemo mirija na kupelekea ushindwe kushika mimba ingine mapema.
Mwisho kabisa damu nyeusi yaweza kuashiria uwepo wa changamoto kwenye kizazi kama uvimbe yani fibroids na mimba kutunga nje ya kizazi.
Matibabu kwa changamoto ya hedhi nyeusi
Matibabu ya tatizo yanategemea na chanzo, hakikisha unaenda hospital endapo hujui nini kimepelekea utokwe na damu nyeusi. Tiba zitakuwa kwenye mgawanyo huu
- Kama kuna kifaa kimekwama ndani ya uke, daktari atakuchunguza na kukitoa haraka.
- Magonjwa ya zinaa mara nyingi yanatibika kwa antibiotics. Hakikisha unafatilia matibabu yote mpaka unamaliza kwani usipomaliza dawa mwili unakuwa sugu.
- Kama utavusha hedhi zaidi ya wiki mbili, muone daktari. Unaweza kuwa na mimba ama uchafu umeganda ukeni.
- Saratani ya shingo ya kizazi inatibiwa kwa muunganiko wa tiba ikiwemo chemotherapy, ,mionzi na upasuaji kulingana na ukubwa wa tatizo. Hakikisha unafanya vipimo vya mlango wa kizazi kila mwaka kujua kama kuna vihatarishi.
Lini unatakiwa kumwona daktari?
Hedhi ya kawaida inachukua 3 mpaka 7 kuisha na inajirudia baada ya siku 21 mmpaka 35. Ukipata hedhi nyeusi nje ya mzunguko wako na zaidi ya siku zako za hedhi ulozoea maana yake kuna shida.
Kama unapata damu nyeusi wakati wa ujauzito au baada ya kujifungua, au baada ya kukoma hedhi, ni muhimu kumwona daktari haraka. Yaweza kuashiria shida kubwa.
Tumia Evecare kuweka sawa hedhi yako
Evecare ni tiba asili kutoka india. imetengenezwa kwa muunganiko wa mimea tiba na kuwekwa kwenye mfumo wa vidonge 30 tu. Kama wewe unaamini kwenye tiba asili zenye ubora na una tatizo kwenye hedhi yako, basi usiache kutumia evecare. Lengo letu kukupa evecare ni kukusaidia
- kuweka sawa hedhi yako ianze kutoka nyekundu ya kawaida
- kurekebisha mzunguko wa hedhi na kuuweka sawa
- kupunguza maumivu makali ya hedhi kipindi cha hedhi
Gharama ni Tsh 75,000/= Dozi ya week mbili tu.
angalizo
Kuna wimbi kubwa la wajasiliamali mitandaoni wanauza vidonge fake vya evecare, tena wanauza kwa bei rahisi sana. Watu hao siyo madaktari wala siyo wataalamu wa afya na wanauza bidhaa feki ambazo ni hatari wa afya yako. Wengi wao hawana hata ofisi, ukipata madhara unakosa pa kuuliza. Kuwa makini na watu hao, wamejaa sana insta na fb.