Categories
Siku za hatari

Je kubana miguu baada ya tendo kunasaidia kushika mimba mapema?

kubana miguu baada ya tendo

Kwa mwanamke unapojaribu kushika mimba,unakuwa na shauku ya kujaribu mbinu mbalimbali ili jambo lako ilitimie mapema. Wengi wanasema kubana miguu baada ya tendo yaweza kusaidia, hili tutaona kwenye makala ya leo kama ni kweli ama siyo.

Wanawake wanaamini kwamba kubana miguu baada ya kutiwa mbegu ni mbinu ya kuanya ashike mimba mapema. Baada ya tendo mwanamke ananyoosha miguu juu na kuibana huku akiegemeza kwenye kitanda au ukuta kwa dakika kadhaa.

Kubana miguu baada ya tendo na nguvu ya uvutano(gavity)

Dhana hii inabebwa na imani kwamba nguvu ya uvutano ya dunia yani gravity inarahisisha mbeu kuogelea na kwenda kurutibisha yai mapema.

Ni ahisi sana kuamini jambo hili, lakini tumewauliza wataalamu wa afya na kupitia tafiti mmbalimbali, na hapa chini tutasoma ukweli kuhusu dhana hii tuone uhalisia wake.

Je urutubishaji unaanyikaje? na Je kubana miguu baada ya tendo kunasaidia?

Kabla ya kujua kama kubana miguu baada ya tendo inasaidia kuhika mimba, tuone kwanza urutubishaji unatokeaje.
Kuna njia mbili ambapo urutubishaji unaweza kufanyika, moja ni kwa kuingiliana mwanamke na mwanaume bila kina na mbili ni kwa mwanamke kupandikizwa mbegu hospitali kwa kutumia vifaa maalumu.

Kupandikizwa yani atifirtial insemination kunafanykika na mtaalamu wa afya aliyebobea. Mbegu za mwanaume zinakusanywa kwa uangaliffu na kutunzwa, kisha mwanamke ataandaliwa na kupandikiziwa mbegu kwenye siku zake za hatari

Kubana miguu baada ya tendo ni imani tu isiyo na ukweli

Kama wataalamu wanavosema hakuna ukweli wowote kwamba eti kubana miguu inasaidia mbeu kuogelea, pia hata kulala chali kwa mda siyo suluhisho la mbegu kufika kwenye yai. Kuna baadhi ya mambo mengine unaweza kuanya kuongeza hansi yako ya kushika mimba ikiwemo kuanya tendo kwenye siku za hatari.

Utajuaje siku za hatari?

Njia zifuatazo zitakusaidia kujua siku ya ovulation/siku za hatari

1.Kwa miezi 8 mpaka 12 rekodi siku ambayo unaanza hedhi na uhesabu siku zote za kila mzunguko. Siku ya kwanza ni ile unayoanza hedhi katika mwezi husika na hesabu mpaka siku unayoanza hedhi katika mwezi mwingine hapo mzunguko mmoja utakuwa umekamilika.

2.Rekodi mzunguko mfupi na mzunguko mrefu zaidi katika ufuatiliaji wako

3.Kupata siku yako ya kwanza ya hatari chukua namba ya mzunguko mfupi zaidi toa 18, mfano mzunguko wako mfupi ni siku 27-18 inabaki 9.

4.Kupata siku yako ya mwisho ya hatari kwenye mzunguko, chukua siku za mznguko wakko mrefu toa 11. Mfano mzunguko wako mrefu ilikuwa siku 30-11 inabaki 19.
5.Katika mahesabu hapo juu ni kwamba siku kati ya mzunguko mfupi na mrefu ndizo siku zako za hatari, kwa maaana ya kuanzia siku ya 9 na 19 ndizo siku zako za hatari. Kama unataka usishike mimba basi usifanye ngono siku ya 9 ya hedhi mpaka siku ya 19.

Kubana miguu baada ya tendo kunasaidia kushika mimba haraka? Lini unatakiwa kumwona daktari?

Kitu cha muhimu sana unatafuta mimba ni kutazama ushauri wa daktari na vipimo endapo unatafuta mimba kwa zaidi ya miezi 12 bila mafanikio.
Kama unajaribu mimba a una historia ya changamoto kama hedhi kuvurugika, magonjwa ya zinaa, kutoa mimba nyingi, kuugua vimbe kama fibroids nk unatakiwa kumwona specialist wa wanawake mapema.

Mwanaume pia inahitajika apime mbegu (semen analysis) maana yawezekana shida ikawa ipo kwake na siyo kwa mwanamke.

Kwa ushauri na tiba asili tuandikie kwa whatsapp namba 0678626254

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *