
Uchafu ukeni upo wa aina nyingi sana, kuna uchafu mzuri na uchafu mwngine unaashiria kuna changamoto ya kiafya. Uhafu mwingi unaotoka unakuwa ukeni ili kukulinda dhidi ya maambukizi mengi. Topic ya leo tutajifunza zaidi kuhusu uchafu wa kunata ukeni na nini cha kufanya.
Ni kwaida kupata kiwango cha uchafu kiasi cha kujiko kimoja kila siku, na wingi wa uhafu utategemea upo siku ipi kwenye mzunguko wako.
Pamoja na kukulinda dhidi ya maambukii, uchafu wawea kuashiria endapo unaugua tatizo flani na kama inahitaji kwenda hospital haraka.
Je ni kawaida kutokwa uchafu wa kunata ukeni?
Uhafu wa ukeni unatofautiana mwonekano, wningi na uzito kulingana na mabadiliko ya homoni kwenye mzunguko wako. Uteute unaotoka ukiwa period siyo sawa na ule unaotoka siku za hatari.
Hebu tusome kwa undani nini kinatokea kwenye kila hatua/phase ya mzunguko.
Mzunguko wako unagawanyika katoka hatua/phase mbili; Tunaziita follicula phase na luteal phase. Katikati ya hivi vipindi viwili ndio kuna kipindi cha yai lililokomaa kutolewa yani ovulation.
Mabadiliko ya homoni na uchafu wa kunata ukeni
Vipindi hivi vyote vinaratibiwa na mabadiliko ya homoni ama vichocheo, homoni kama etrogen na progesterone. Estrogen inasaidia kujena ukuta na kuandaa kubeba mimba na pia inaathiri namna ya uchafu unaotoka.
Kama uchafu unatoka wa kunata basi kwa kiasi kikubwa yaweza isiwe tatizo. Lakini usiishie kwa kuangalia mwonekano tu wa uchafu, tazama na dalili zingine kama unahisi muwasho, haurufu mbaya, kutokwa damu na maumivu.
Kama uchafu unatoka ukeni ni wa kunata, ni mweupe na hauna rangi na hakuna haufu mbaya au dalili zingine mbaya mwilini. Basi hapo ujue uko salama kabisa
Je kwanini napata uchafu wa kunata ukeni
Uchafu wa kunata maa nwingi unaanza kutoka baada tu ya kumaliza hedhi na baada ya ovulation. Uchafu unavokuwa wa kunata zaidi ndvyo inakuwa ngumu kwa mbegu kuogelea na kurutubisha yai.
Uchafu huu wa kunata ni tofautia kabisa na uchafu uanovutika kama yai ambao unataoka kwenye ovulation. Uteute huu unakuwa laini na kuvutika ili kufanya mbegu kuogelea vizuri kwenda kurutubisha yai.
Vipi kuhusu uteute unaotoka ukiwa na hisia za mapenzi
Mwanamke ukiamshwa na hisia za mapenzi zikapanda, utahisi unyevunyevu ukeni na ute wa kuteleza. Huu ni ute alama ili usipate maumivu kwenye tendo wakati wa msuguano. Ute huu unaweza kunata kadiri unavoendelea na tendo.
Uteute karibia na siku ya hedhi
Unapokarbia kuanza hedhi utaanza kuona uteute wa jkunata ukeni, sawa na unapomalizia hedhi. Kipini hiki waweza kupata uchafu wa pink, brown au mwekundu ambao ni kawaida kabisa.
Uchafu unaoashiria maambukizi
Japo uchafu wa kunata ukeni siyo ishu kubwa sana, ni muhimu kutazama pia dalili zingine ili uone kama hauna maambukizi. Tazama kama uchafu unaambatana na dalili zingine kama
- maumivu ukeni na muwasho
- uchafu wa kijani
- uchafu mwingi sana katoka siku
- Uchafu wa kama maziwa mtindi au usaha
- maumivu wakati wa kukojoa au kwenye tendo
- maumivu chini ya kitovu
- harufu mbaya ukeni kama shombo la samaki
Lini unatakiwa kumwona daktari?
Mwone daktari mapema ukiona daklili mbaya hapo juu. Utapata vipimo na kuanza toba mapema, maana magonjwa kama ya zinaa siyo ya kuhelewa kupata tiba.
Hitimisho kuhusu uchafu wa kunata ukeni
Mhanganyiko wa uhafu ukeni, bakteria wazuri na uteute unasaidia kulinda uke wako na kufanya uwe mlaini
Uchafu mzuri ukeni unatofautiana kwa wingi na uzito kulingana na upo siku ya ngapi kwenye mzunguko wako
Hisia za mapenzi, Ujauzito , hedhi na pia maambukizi vyote hivi vinaathiri mwonekano na wingi wa ucchafu unaotoka
Kama una hofu juu ya uhafu wako unaooka ukeni, basi tizama kama una unatoa harufu, ni mwingi kupita kiasi, upo kama maziwa mtindi, wa kijani na una dalili zingine za muwasho na malengelenge. Hapo unatakiwa kumwona daktari mapema.