Jinsi Gani Kipimo Cha Mimba Kinafanya Kazi?
Kipimo cha mimba kinafanywa kwa kuchukua sampuli ya mkojo au damu ili kupima uwepo wa homoni inayoitwa human chorionic gonatrophin(hCG).
Mwili wako huanza kuzalisha homoni hii baada tu ya yai lililorutubishwa kujishikiza kwenye ukuta wa kizazi. Kiwango cha kuzalishwa homoni hii huongezeka na kudabo kila baada ya siku 2 mpaka3.
Aina za Vipimo vya Mimba Zinazotumika Mara kwa Mara
Kipimo cha Damu
Kinafanyika hospitali pekee, hakitumiki sana kama kile cha mkojo, na majibu yake huchukua muda zaidi, yahitaji kusubiri. Kipimo hichi kinaweza kugundua uwepo wa mimba katika kipindi kifupi sana baada ya kushika ujauzito. Kabla hata hujaanza kuona dalili, ndani ya siku 6 mpaka nane.
Kipimo Cha Mkojo
UPT ama kipimo cha mkojo waweza kufanya ukiwa nyumbani ama hospitali. Unaweza kununua kifaa cha kupima famasi ya karibu ukapima na kujua majibu pasipo mtu mwingine yeyote kufahamu. Ni kipimo rahisi kutumia na kinatoa majibu haraka sana.
Maandalizi ya kufanya kipimo cha mimba cha mkojo
Kama unafanya kipimo ukiwa nyumbani, hakikisha unazingatia yafuatayo
- unasoma kwa uangalifu maelekezo ya matumizi, kwenye pakiti lenye kifaa cha kupimia kabla hujaanda mkojo wa kupima
- kipimo hakijaexpire
- pima mkojo wa kwanza wa asubuhi baada ya kupitisha hedhi yako
- usinywe maji au kinywaji chochote kwa wingi, kwasababu itafanya homoni ya HCG kuwa kidogo na kutoonekana kwenye kipimo.
Hatua za kupima
Namna ya kupima ni kwa kukusanya mkojo kiasi kidogo kwenye kikombe, kisha unazamisha kipimo kwa muda wa dakika 1. Hakikisha usivuke ule mstari wa maximum unapozamisha kifaa kwenye mkojo.
Majibu ya Kipimo Yanasomwaje?
Vipimo vingi kama mimba ipo huonesha mistari miwili ya rangi nyekundu na mstari mmoja kama hakuna mimba. Baadhi ya vipimo huonesha alama ya chanya(+) na vingine huandika neno pregnant au not pregnant.
Hata kama mstari mmoja umefifia na mwingine umekoleza, hapo tayari kuna mimba lakini bado changa. Ukirudia tena baada ya wiki moja au mbili basi mstari utakuwa umekolea zaidi.
Nina wasiwasi na majibu nifanyeje?
Endapo hujaridhika na majibu yako, subiri tena wikik moja kisha upime kwa usahihi kama ulivoelekezwa na mtoa huduma alieyekuuzia kifaa. Pia unaweza kwena hospitali na kufanya kipimo cha damu. Kipimo cha damu kinaweza kugundua mimba hata ndani ya wiki moja tu.
Kipimo cha Mimba ni sahihi Kwa asilimia Ngapi?
Maarufu kama UPT kipimo hiki waweza kufanya ukiwa nyumbani kinaweza kukupa usahihi wa matokeo kwa ailimia 99, kama utafuata maelekezo vizuri ya upimaji.
Kipimo cha damu ni sahihi zaidi ya asilimia 99. Kumbuka usahihi wa kipimo kama umejipima mwenyewe nyumbani unategemea jinsi gani umefuata maelekezo ya kupima na umri wa ujauzito
Lini Unatakiwa Kufanya Kipimo cha Mimba?
Baadhi ya vipimo vya homoni ya HCG vinaweza kutoa matokeo hata kabla ya kukosa hedhi yaani week moja baada ya kushika mimba, lakini fahamu kwamba matokeo yatakuwa sahihi zaidi endapo utasubiri wiki moja baada ya kukosa hedhi inayofuata.
Nawezaje Kupata Kipimo cha mimba nijipime Nikiwa Nyumbani?
Unaweza kununua famasi ya karibu na ukapata maelekezo kutoka kwa muhudumu wa famasi namna ya kutumia. Ni bei ndogo tu sh elfu moja.
8 replies on “Kipimo cha Mimba na Jinsi ya Kusoma Majibu”
Mpenz wang anaxumbuliwa na kizunguzungu mara kwa mara tatizo ni nin
Tafadhali mpeleke hospitali mapema akapate vipimo, anaweza kuwa na upungufu wa damu
mke wangu toka ajiunge uzazi wa mpango ana mwaka wa tatu hajaona siku zake je hilo litakuwa na madhara!
Je kipimo chaminba kinawez kusoma minba ina mdagani?
Je, kama mke hana mimb na anatokwa na uchafu ni dalil gan?
Na je kama nimepima af imetokea mtar mmoja ambao haujakolea langi
Wengne hatutu mii whatsapp
Habr