Categories
Mifupa na Joints

Mifupa kusagika

mifupa kusagika

Mifupa kusagika kitaalamu tunaita osteoarthritis, ni ugonjwa uliopo kwenye kundi la degenerative disease. Haya ni magonjwa yanayosababishwa na kuchoka au kuharibika kwa muundo wa kiungo mpaka kupelekea kuzorota kwa ufanisi wake siku hadi siku.

Mifupa kusagika ama osteoarthritis inatokea zaidi mtu anavozeeka ama umri kwenda. Mabadiliko yanayopelekea mifupa kusagika yanatokea taratibu sana na yanaweza kuchukua miaka mingi mpaka kuleta athari. Japo katika mazingira flani hali yaweza kujitokeza katika umri mdogo.

Kuvimba na majeraha kwenye joint kunapelekea mabadiliko ya mifupa, kulegea na kuvunjika kwa maungio na hivo kupelekea maumivu na kuvimba kwa joint.

Kuna aina kuu mbili za mifupa kusagika (osteoarthritis)

primary osteoarthritis ambayo inaathiri zaidi vidole, uti wa mgongo,hips, magoti na kidole gumba.
Secondary: hii inatokea kutokana na tatizo lililokwepo awali mfano jeraha la kujirudia, baridi yabisi kama gout na rheumatoid arthritis na magonjwa ya kurithi ya joints.

Nani anaweza kupata shida ya kusagika mifupa?

Karibu asilimia 80 ya watu wazima wenye umri zaidi ya miaka 55 wanapata osteoarthritis. Kati ya hawa, asilimia 60 wana dalili za mifupa kusagika. Na inakadiriwa kwamba zaidi watu milioni 240 duniani kote wana dalili za mifupa kusagika. Wanawake waliokoma hedhi wapo kwenye hatari zaidi kutokana na kupungua kwa uzalishaji wa homoni ya estrogen.

Magonjwa au vitu gani hatarishi hupelekea mifupa kusagika?

Ukiacha swala la umri na magonjwa ya joints kama baridi yabisi, kuna mazingira na magonjwa yanayoongeza hatari ya kutokea kwa tatizo la mifupa kusagika. Fatilia maelezo yake kwa kina hapa chini.

1.Uzito mkubwa na kitambi: uzito mkubwa na kitambi unapelekea sana mifupa na jonits kusagika hasa eneo la magoti. Mwili unapokuwa mzito unaleta mgandamizo mkubwa eneo la joint na kupelekea tatizo. Ni muhimu kuweka sawa uzito wako ili upunguze hatari ya mifupa kusagika.

2.Kisukari na mafuta mengi. Kisukari na mafuta mengi kwenye mwili yanaongeza hatari ya kututumka ama kuvimba viungo vya ndani na kwenye joints na hivo kuongeza hatari ya mifupa kusagika. Kuongezeka kwa sukari kunapelekea sumu kuongezeka na kuleta hatari kwenye maungio.

3.Kupungua kwa homoni ya estrogen baada ya kukoma hedhi: Estrogen ni kichocheo ama homoni inayosaidia kulinda mifupa na maungio ya mifupa. Mwanamke anapofikia umri wa kukoma hedhi, kichocheo hiki kinapungua uzalishaji wake na hivo kuongeza hatari ya tatizo.

4.Magonjwa ya kurithi: Baadhi ya watu wanaweza kuugua magonjwa ya mifupa kwa kurithi kutoka kwa mababu. Hili ni ngumu kuepukika.

Je nitajuaje kama nina tatizo la mifupa kusagika?

Tofauti na magonjwa mengine ya joints, tatizo la osteoarthritis linaanza kukutafuna taratibu na kuchukua mika mingi mpaka kujionesha. Linaongezeka zaidi kutokana na kazi unazofanya na namna unavoshugulisha zaidi mwili kwako mfano kutembea na kukimbia. Hali ya maumivu na kuvimba kwenye maungio pia kunaongezeka siku hadi siku.

Kusagika kwa mifupa haisababishi wekundu kwenye kiungo kama ilivyo kwa baridi yabisi.

Unapoenda hospital daktari atachukua historia yako ya kuumwa na dalili unazopata. Anaweza kukufanyia kipimo cha X ray na MRI endapo ataona inafaa zaidi. Kama maungio yako yamejaa maji, daktari anaweza kuamua kufyonza maji yaliyopo .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *