Categories
Tendo la ndoa

Sababu Kwanini Uende Haja Ndogo Baada ya Tendo

haja ndogo baada ya tendo

Kwanini unatakiwa kwenda haja ndogo baada ya tendo?

Kwenye makala hii fupi tutaeleza kwanini unatakiwa kupata mkojo baada ya tendo. Na uhusiano wake na magonjwa kama UTI.

Je nini faida za kwenda haja ndogo baada ya tendo?

Ni muhimu sana mwanamke kjwenda haja ndogo baada ya tendo. Hizi ni sababu kwanini ufanye hivo

1.Kuepuka UTI

UTI ni maambukizi kwenye viungo vya njia ya mkojo kama kibofu, mirija ya mkojo na figo. Maambukizi haya yanatokea pale bakteria wanapokua kupita kiasi kwenye njia ya mkojo na kuwa wengi kwenye kibofu. Kama kinga yako ya kwenye njia ya mkojo ikifeli , bakteria hawa hukua na kuleta maambukizi.

Je kwanini wanawake wanapata zaidi UTI?

UTI inawapata zaidi wanawake kutokana na sababu hizi

Maumbile ya mwanamke: Mrija wa mkojo kutoka kwenye kibofu mpaka kwenye uke ni mfupi zaidi kwa mwanamke na hivo kufanya njia ya bakteria kusafiri mpaka kwenye kibofu kuwa haraka zaidi.

Uzazi wa mpango wa kisasa: Wanawake wanaotumia zaidi kitanzi kupanga uzazi wanaweza kupata maambukizi kirahisi

Ngono: hatari ya kuugua UTI ni kubwa zaidi kwa mwanamke anayefanya tendo kuliko yule aliepumzika kufanya tendo

Kukoma hedhi(menopause): Kupungua kwa uzalishaji wa homoni ya estrogen, inapelekea kupungua uteute ukeni na hivo uke kuwa kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi.

Sababu zingine zinazopelekea mtu augue UTI kirahisi ni pamoja na

Maumbile yasiyo ya kawaida kwenye njia ya mkojo: watoto waliozaliwa na hitilafu kwenye mfumo wa mkojo wanaweza kupata maambukizi kirahisi

Kuziba kwa njia ya mkojo: changamoto kama mawea ya figo yanaweza kuepelekea kuziba njiani na hivo kufanya mkojo kubakizwa, mkojo unapobakizwa mda mrefu inasababisha maambukizi.

Matumizi ya kifaa cha kusaidia kutoa mkojo yani catheter hasa kwa wagonjwa wa tezi dume na waliopata kiharusi

Dalili za UTI

Dalili kuu za UTI ni pamoja na

  • kukojoa mara kwa mara na kutoa mkojo kidogo
  • maumivu chini ya kitovu
  • mkojo wa njano wenye harufu
  • kuhisi uchovu sana
  • kuungua na maumivu wakati wa kukojoa
  • kupata hamu ya kwenda kokojoa mara kwa mara

Mrija wa mkojo kwa mwanamake

Mirija huu huitwa urethra, unasaidia kutoa mkojo kutoka kwenye kibofu kwenye njie ya uke. Kwa mwanamke mrija huuni mfupi(sm 2.5 mpaka 4) na kwa mwanaume ni (sm 15 mpaka 20). Hii inawafanya wanawake kuwa kwenye hatari zaidi ya kuugua UTI kuliko wanaume, kwasababu ili maambukizi yatokee ni lazima bakteria wapande mpaka kwenye kibofu. kama njia ni fupi maana yake ni rahisi zaidi kwa bakteria kufika kwenye kibofu na kwenda mpaka kwenye figo.

Kibofu cha mkojo

Kibofu cha mkojo n mfumo ulipo katikati ya mifupa na misuli ya nyonga, na kazi yake ikiwa ni kuhifadhi mkojo kutoka kwenye figo. Kibofu kinapojaa mkojo na kutanuka sana, kinatuma taarifa kwenye ubongo ili ukakojoe.

Wakati wa tendo la ndoa, bakteria wanaweza kuingia kwenye mrija wa mkojo na kupngeza chansi yako ya kuugua UTI. Ndiomaana ni muhimu sana baada ya tendo uende kukojoa ili kuflash vimelea kabla hawajaleta madhara.

Pia kufanya tendo wakati kibofu cha mkojo kimejaa kinapelekea kulegea kwa misuli ya kushikilia mkojo. Yani inafikia wakati unashindwa kuzuia mkojo kiasi kwamba ukocheka, ukipiga chanfya au hata kwenye tendo mkojo unakuponyoka.

Hakikisha unakojoa kabla na baada ya tendo siku zote.

Kwa ushauri na Tiba asili Tuandikie whatsapp namba 0678626254.

7 replies on “Sababu Kwanini Uende Haja Ndogo Baada ya Tendo”

Mimi wife yangu huwa anaugua kichwa.na tumbo chini ya kitovu pia na hedhi yake ni july ilikuwa tarehe 9.august ilikuwa 19 na septembe ilikuwa 12 je mwana mke huyu ana mzunguko sahihi wa hedhi?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *