Naamini umekuwa ukisikia hili neno kwa muda mrefu sana, pasipo kujua undani wa dawa hii ya viagra. Leo nitakweleza kwa undani kuhusu viagra, ikiwemo matumizi, upatikanaji, madhara yake ya mda mrefu na kitu gani waweza kutumia kama mbadala wa viagra.
Viagra ni kutu gani?
Endapo unawahi kufika kileleni ama unashindwa kusimamisha uume vizuri wakati wa tendo la ndoa. Ukienda hospitali, daktari anaweza kukuandikia utumie viagra. Hii ni dawa daktari anakwandikia kusaidia nguvu za kiume.
Viagra inakuja katika mfumo wa vidonge na hutakiwi kutumia mpaka uandikiwe na daktari, na utatumia kabla ya tendo siyo kila siku.
Viagra inafanyaje kazi?
Uume unasimama pale protini inayoitwa cyclic guanosine monophosphate(cGMP) inapotolewa kwenye damu, na kupelekea mzunguko mkubwa wa damu kuelekea kwenye uume. Mzunguko wa damu ukiwa mkubwa kuelekea kwenye uume hapo utaweza kudindisha vizuri na kupiga show mda mrefu bila kuchoka.
Je inachukua mda gani kwa Viagra kufanya kazi?
Viagra inaleta matokeo haraka sana baada tu ya kumeza dozi yako. Viagra inafanya kazi ndani ya lisaa. Kwa watu wachache inaweza kuanza kazi ndani ya nusu saa tu baada ya kumeza, na wengine mpaka baada ya masaa ma4.
Je vipi kama Viagra haitafanya kazi?
Endapo viagra haitafanya kazi, hakikisha unamjulisha daktari aliyekuhudumia. Daktari anaweza kupendekeza utumie dozi kubwa zaidi ya dawa, kisha ataendelea kukufatilia kama dozi hiyo kubwa imefanya kazi.
Je Nguvu a Viagra inaisha Ndani Ya Muda Gani?
Viagra inafanya kazi vizuri ndani ya masaa kadhaa baada ya kumeza. Kwa watu wengi dawa inafanya kazi ndani ya lisaa tu na kwa tu wachache dawa itaendelea kukupa nguvu mpaka masaa ma4. Kadiri mda unavosogea nguvu ya viagra inapungua na baadae kuisha. Hapo utahitaji kumeza tena ikiwa unataka kushiriki.
Kwahivo ieleweke hii siyo tiba ya tatizo lako. Ni booster tu ya mda mfupi ili ufurahie tendo, kisha utarudi kule kule.
Je Vigra inatumika Kwa Wanawake?
Pengine unajiuliza je mwanamke naye anatumia kuimarisha nguvu za kike? Dawa hii imethibitishwa kutumika kwa wanaume tu kwenye tatizo la uume kutosimama imara.
Je Kuna Matokeo/madhara Gani Kutumia Viagra?
Kama ilivo kwa dawa zingine zote, Viagra yaweza kuwa na madhara madogo na hata makubwa pia. Hapa chini ni list ya madhara yanayoweza kujitokeza. Kumbuka madhara haya yanatofautiana na umri wa mtu. Magonjwa mengine aliyonayo na pia dawa anazotumia kwa sasa.
Dalili/matokeo Ya Mda Mfupi
Dalili mbaya au matokeo yanaweza kujitokeza baada ya kumeza viagra ni pamoja na
- kichwa kuuma
- makamasi kwenye koo
- maumivu chini ya mgongo na misuli
- kizunguzungu
- kiungulia na
- mabadiliko kweneye kuona
Madhara Makubwa ya Viagra
Madhara makubwa yanaweza kujitokeza ukimeza viagra, ila usiogope, hayajitokezi mara kwa mara. ikiwa umepata matokeo haya, mweleze daktari mapema. Matokeo haya ni pamoja na
- kushindwa kuona
- kupata aleji
- presha kushuka sana
- kupata shambulizi la moyo
- kupungua uwezo wa kusikia na pia
- kuumia sana wakati wa kukojoa mbegu
- uume kukosa nguvu kabisa kwenye tendo hasa ukitumia viagra kwa mda mrefu
Jinsi ya Kutumia Viagra
Kwasababu dawa unaandikiwa hospitali, ni lazima daktari, ni lazima akwandikie matumizi ya dawa. Muhimu sana kufatilia maelekezo uliopewa na daktari wako. Viagra zinapatikana wa nguvu za ujazo tofauti, yani mg 25, mg 50 na mg 100.
Muda gani unatakiwa kumeza viagra
Viagra inatakiwa kumezwa pale tu inapohitajika, yani lisaa limoja kabla ya kwenda kufanya ngono. Haitakiwi kumezwa mara kwa mara. Hutakiwi kabisa kumeza viagra zaidi ya mara moja kwa siku.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu viagra
1.Je viagra inaongeza hamu ya tendo la ndoa?
Jibu ni hapana, viagra haiongezi hamu ya tendo. Unatakuwa uwe na msisimko tayari wa kuifanya tendo ili viagra ifanye kazi . Kazi ya viagra ni kuongeza msukumo wa damu kuelekea kwenye uume ili usimame vizuri kwenye tendo.
2.Je viagra inazuia kumwaga mbegu? au kukufanya umwage mbegu mara nyingi zaidi?
inawezekana kabisa viagra kubadili mfumo wa utoaji mbegu kama ilivokuwa mwanzo/ mabadiliko haya ni pamoja na
- kukuzuia kumwaga mbegu
- kufanya umwage mbegu mara nyingi zaidi
Kama unapata changamoto baada ya kutumia viagra, ongea na daktari aliyekuhudumia.
3.Je Viagra inafanya uume uendelee kusimama hata baada ya kumwaga mbegu?
Ndio, viagra yaweza kukufanya uendelee kusimamisha hata baada ya kumwaga mbegu. Lakini endapo uume utasimama zaidi ya masaa ma4 muone daktari haraka. Hii inaweza kuwa hali ya hatari inayohitaji usaidizi wa haraka, maana itaharibu uume wako.
4.Je Viagra inaongeza ukubwa wa uume wako?
Hapana, ni ngumu sana viagra kuongeza ukubwa wa uume wako kuliko kawaida. Uume utavimba tu wakati una hisia za tendo, ukimaliza tendo uume unarudi kawaida. Viagra itafanya tu uume usimame na uwe imara kuliko kawaida ila siyo kuongeza maumbile.
Makundi ya watu wasiotakiwa kutumia Viagra
Viagra yaweza isikufae endapo una matatizo baadhi ya kiafya. Ongea na daktari vizuri na mweleze historia yako yote kabla hujaanza kumeza viagra. Magonjwa ama changamoto hizo ni pamoja na
- magonjwaya moyo, stroke ama umefanyiwa upasuaji wa moyo ndani ya miezi 6
- uume wako una maumbile yasiyo kawaida , mfano umejikunja sana, ama unapata mjeraha mara kwa mara.
- Magonjwa ya damu kama sickle cell
- magonjwa ya moyo
- una presha ya kushuka
- una changamoto za kutokwa damu mfano puani na kwingine kwenye matundu
- vidonda vya tumbo: Hakikisha unamweleza daktari ikiwa unaumwa vidonda tumbo
- magonjwa ya figo na ini: kama figo na ini zina hitilafu, kumeza dawa yaweza kuongeza sumu mwilini na kuleta shida zaidi.
Viagra Na Pombe
Kunywa viagra na huku unaendelea na pombe yaweza kuleta shida ya kupungua zaidi kwa presha ya damu. Kama wewe ni mnywaji wa pombe hakikisha unamjulisha daktari kuhusu hilo mapema.