Tendo la ndoa ni moja na tukio tamu na la kufurahisha sana katika maisha ya mwandamu. Tendo linaimarisha ukaribu na upendo baina ya mke na mume. Pamoja na hayo ,watu wengi wanapata maumivu makali wakati wa tendo na hawafurahii kabisa. Kuna mambo mengi yanapelekea maumivu ukeni wakati wa tendo. Soma zaidi kujua nini cha kufanya kuondoa tatizo.
Maumivu kwenye tendo la ndoa ni kitu gani hasa?
Kitaalamu huitwa dyspareunia ni neno linalomaanisha maumivu ya via vya uzazi wakati wa tendo au baada ya tendo. Tatizo hili linawapata karibu asilimia 75 ya wanawake wote duniani.
Maumivu kwenye tendo yanaweza kuvuruga mahusiano, kukufanya ujihisi mpweke na huna thamani na kukosa kujiamini mbele ya mpenzi wako. Baadhi ya wanawake huamua kutojihusisha tena na tendo la ndoa baada ya kupata maumivu.
Pamoja na kwamba tatizo linatibika kwa kiasi kikubwa, watu wengi ni waoga sana kuelezea changamoto hii kwa kuogopa aibu ama kudharaulika.
Dalili za maumivu kwenye tendo
- maumivu ya haraka
- hali ya kuungua ukeni
- kukosa hamu ya tendo
- kushindwa kufika kileleni
- maumivu ya tumbo
Je haya maumivu yanatokea ukeni tu?
Maumivu kwenye tendo yanatofautiana kwa kila mtu. Baadhi ya wanawake wanahisi maumivu wakati uume unaingia, na wengine wanapata maumivu wakiguswa tu kwenye via vya uzazi. Baadhi wanapata maumivu ya tendo baada ya kukoma hedhi.
Maumivu yanaweza kutokea
- ndani ya ukeni
- kwenye mashavu ya ukeni
- chini ya mgongo
- ndani ya kizazi
- kwenye nyonga
- tumboni chini ya kitovu na
- kwenye ukuta unaotenganisha uke na mkundu
Baadhi ya wanawake wanapata maumivu baada tu ya kumaliza tendo, na wengine wakati wa kukojoa.
Nini kinapelekea maumivu kwenye tendo?
Baadhi ya sababu kubwa zinazopelekea mwanamke kupata maumivu ni pamoja na
1.Ukavu ukeni
Hii ni sababu kubwa zaidi ya maumivu kwenye tendo kutokana na kukosekana na ute ukeni na hivo msuguano kuwa mkubwa. Ukavu ukeni inatokea zaidi baada ya kukoma hedhi. Mabadiliko ya homoni yanapelekea kupungua kwa uzalishaji wa ute kwenye uke baada ya kukoma hedhi.
Sababu zingine zinazopelekea ukavu ukeni ni pamoja na kutumia njia za kisasa kupanga uzazi, kunyonyesha, stress na mwanamke kutoandaliwa vya kutosha.
2.Maambukizi
Maambukizi aina tofauti yanaweza kupelekea maumivu kwenye tendo. Maambukizi haya ni pamoja na
- maambukizi ya bakteria ya ni bacterial vaginosis
- fungus ukeni: dalili zake ikiwa ni pamoja na kutokwa uchafu unaoganda mzito, muwasho
- kisonono
- UTI kali
- PID na
- Chlaydia
Pia magonjwa mengine kwenye kizazi yanaweza kupelekea maumivu kwenye tendo. Magonjwa haya ni pamoja na
- Endometriosis- yani ukuta wa ndani wa kizazi kuvimba
- vaginismus: hii ni hali ya uke kugoma kuruhusu kitu chochote kuingia
- Fibroids: Vimbe kwenye ukuta wa kizazi
- Ovarian cyst: Vimbe kwenye mayai
- Bartholin abscess: hizi ni vimbe kweye tezi za uke
- Cervicitis: yani maambukizi kwenye mlango wa kizazi na kupelekea kuvimba kwake
Kumbuka magonjwa haya ni ngumu kwako kuyagundua ukiwa nyumbani. Ni mpaka kwenda hospitali, na kufanyiwa vipimo ndipo daktari atakwmabie endapo una uvimbe nk
Nini cha kufanya kuondoa maumivu?
Tiba ya tatizo inategemea na chanzo chake. Unapojiskia vibaya, hatua ya kwanza ni kwenda hospital na kuonana na daktari ili akusaidie kugundua chanzo cha tatizo.
Daktari atakuuliza baadhi ya maswali kujua historia ya tatizo, na aatapendekeza vipimo vya kufanyiwa.
Baada ya vipimo ndipo utapewa dawa sahihi ili uanze tena kufurahia tendo la ndoa.
Mawasiliano baina ya wapenzi
Mawasiliano ni nguzo muhimu sana kwenye mahusiano, itasaidia wapenzi kujuana kuhusu changamoto zao. Mpenzi wako ataweza kukuvumilia wakati unaendelea na tiba. Kumbuka kuendelea kufanya tendo wakati unapata maumivu ni mbaya, kwani itakuathiri kisaikolojia na kukfanya uchukue tendo la ndoa.
Kama chanzo cha tatizo ni ukavu ukeni, ni muhimu sana mtumie muda mwingi kwenye kuandaana.
Weka kwenye akili kwamba kutumia vilainishi vya kuganda kulainisha uke, yaweza kuleta madhara kwenye tishui laini za uke. Ni vizuri kutumia vilainishi vye maji maji pamoja na condom.
Kama maumivu unapata siku kadhaa tu, basi jaribu kubadili style ya kufanya mapenzi. Ongea na mwenzi wako akuingilie taratibu bila nguvu nyingi.
Lini unatakiwa kumwona daktari?
Muone daktari haraka endapo tatizo linajitokeza mara kwa mara, na maumivu yanazidi kila unapojaribu kufanya tendo. Pia kama unajihisi unaugua magonjwa kama fungus, unatokwa uchafu usio kawaida ana unapata maumivu ya tumbo muone daktari haraka.