Uchafu mweupe ukeni unatokea sana kwenye mzunguko wa mwanamke na yaweza kuashiria yai kupevuka. Japo katika mazingira flani yaweza kuashiria ugonjwa ama changamoto flani ya kiafya kama fungus.
Kwanini unatokwa na uchafu ukeni?
Kama ambayo mti huangusha matawi, ni kawaida kwa uke wako kujisafisha na kutoa bakteria waliokufa nje ya mwili.
Aina ya uchafu unaoona unabadilika kila siku kwenye mzunguko wako wa hedhi, lakini kwa kiasi kikubwa huwa inaashiria kwamba mwili wako unafanya kazi vizuri sana.
Ute wa ukeni unasaidia kufanya uke wako kuvutia na kuwa mlaini. Utokaji wa ute ni matokeo ya tezi zilizopo ndani ya uke na homoni zako, ndiomaana ute huu unabadilika katika vipindi tofauti vya mzunguko na hata ukiwa mjamzito.
kutoka ute unaashiria mwili kujisafisha
Kutokwa na uchafu ukeni pia ni namna ya mwili wako kubalansi kiwango cha tindikali. Uteute unaleta utelezi kwa ajili ya uchafu, bakteria na vimelea wabaya kutolewa nje ya uke.
Japo siyo kila unapopata uchafu ni kiashiria cha usalama, kuna kipindi waweza kuwa na shida kubwa sana ya kiafya. Endelea kusoma upate mwongozo ili ujue ni wakati gani ukamwone daktari.
Kwanini unapata uchafu mweupe ukeni?
Uchafu mzito mweupe ni kawaida, na unatokea sana kwenye mzunguko wako. Kitaalamu uchafu huu huitwa leukorrhea na ni wa kawaida. Uchafu unaweza kwa kuwa mzito siku chache kabla ya siku za hatari na baadae utakuwa na ute mlaini wa kuvutika kama yai.
Hii ni kiashiria kwamba upo kwenye muda mzuri wa kubeba mimba, maana yai linatolewa. Kama ulikuwa unatafuta mimba huu ndio muda wa kukutana kimapenzi.
Endapo ute unaotoka hauna harufu mbaya na wala hakuna dalili zingine mbaya kama maumivu kwneye tendo na maumivu chini ya kitovu, basi ni kawaida.
Nini kinasababisha Uchafu mweupe kama maziwa ukeni?
Kwenye siku za kwanza za mzunguko unaweza uona ute mwepesi , kama maziwa. Uchafu huu mweupe kama maziwa yaweza kuwa kiashiria kwamba una mimba. Kwenye hatua za mwanzo za mimba , baadhi ya wanawake wanazalisha uchafu mwembemba mweupe kama maziwa. Uchafu huu ni kutokana na mabadiliko ya vichocheo ama homoni na ni kawaida.
Uchafu mweupe kwa mjamzito
Kwa mjamzito uchafu huu unasaidia kutoa vimelea wabaya, bakteria na uchafu ukeni. Pia unasaidia kuweka kifuniko cha ute mzito kwenye mlango wa kizazi. Ute ambao utazuia kitu chochote kuingia kwenye kizazi wakati una mimba.
Kama tu uchafu wako hauna harufu wana kuleta muwasho na hakuna maumivu ya tumbo, basi ujue ni uchafu wa kawaida na huhitaji kupata mawazo.
Lakini kama rangi itabadilika na ya kijani au brown au njano, na inaambatana na harufu mbaya ya shombo la samaki, hapo ujue kuna maambukizi hasa ya bakteria.
Nini kinapelekea uchafu mweupe ukeni wa kunata?
Ukiwa kwenye siku zingine safe yani siku ambazo siyo za hatari, mwili wako unazalisha ute mzito wa kunata. Ute huu ni kama kizuizi cha mbegu kuingia kwenye kizazi.
Pia kazi ya uchafu huu wa kunata ni kuzuia usipate mamabukizi baada ya hedhi, pale ambapo uke unazalisha ute kidogo sana.
Uchafu mweupe mzito ulioganda kama mtindi
Kama unapata uchafu mwupe umekatika kama maziwa mtindi na ni mzito na unapata muwasho, basi hapo ujue una fungus.
Uke wako huwa unafanya kazi kubwa sana ya kubalansi mazingira ua utindikali ili bakteria wazuri wawepo kupabambana na vimelea wabaya. Endapo mazingira yakivurugika hapo ndipo fangasi watakuwa kupita kiasi.
Vimelea wa Fungus aina ya candida wanaweza kukua kupita kiasi na kuleta madhara kwenye uke, na hivo kupelekea utokwe na uchafu mzito wa kuganda. Uchafu huu ni matokeo ya kinga yako kupambana na vimelea hawa.
Watu wenye fungus ukeni wanapata dalili zingine kama
- muwasho kwenye mashavu ya uke
- kuvimba kwa mashavu ya uke
- maumivu wakati wa tendo
- maumivu na hali ya kuungua wakati wa kukojoa
- uke kuuma na kuvimba
Kama unaugua fungus ama umeanza kuona dalili, unaweza kwenda pharmacy ya karibu na kupata dawa.
Ni jambo zuri kusitisha kufanya tendo wakati unatibiwa maambukizi yako ya fungus. Mwanaume hana sababu ya kutibiwa kwasababu hawezi kuambukizwa kwa ngono.
Kama umeshaugua fungus zaidi ya mara 4 katika mwaka, ni vyema umuone daktari specialist wa wanawake. Unaweza kuwa na tatizo lililojificha ambalo linakufanya uugue fungus mara kwa mara.
Jinsi ya kuzuia uchafu mwingi ukeni
Kama unapata uchafu mwingi kupita kiasi na usio wa kawaida, unaweza kuwa na maambukizi, na unahitaji tiba kupona tatizo.
Uchafu mwingi kupita kiasi ni kiashiria cha
- magonjwa ya zinaa
- maambukizi ya bakteria na
- fungus
Lini yatakiwa kumwona daktari?
Ni muhimu kumwona daktari endapo uchafu unaotoka unanuka ama unaambatana na dalili hizi
- muwasho
- maumivu
- kutokwa damu
- kuvusha hedhi
- hali ya kuungua ukeni wakati wa tendo na kukojoa na
- vipele na malengelenge ukeni
Kumbuka kuepuka kuvuruga mazingira ya kwenye uke kama kutumia sabuni, marashi na kusafisha uke mpaka ndani. Tumia maji pekee kujisafisha na safisha eneo la mwanzo tu la uke. Uke umeumbwa kujisafisha wenyewe kila siku, hihitajio kutumia kemikali kujisafisha.