Categories
Afya ya mwanamke na uzazi

Hedhi ya kuteleza kama mlenda

hedhi ya kuteleza

Kama hujawahi kupata hedhi ya kuteleza mithili ya mlenda, inaweza kukuchanganya sana akili siku ya kwanza.

Kwa mwanamke kuwa na mzunguko mzuri wa hedhi ni jambo la kujivunia na linaloleta heshima sana. Mzunguko wa hedhi unaweza kutoa picha kamili nini kinaendelea kwenye mwili wa mwanamke. Kama mfuko wa mimba unapata mzunguko mzuri wa damu, homoni zako zinbalansi, au kama mayai yanatolewa kwenye ovari

Makala hii itaongelea kwa kina juu ya hedhi ipi ni salama na ipi siyo salama. karibu tujifunze.

Hedhi ya kuteleza kama mlenda.

Kwa kiasi kikubwa kupata hedhi ya mlenda ni kutokana na damu iliyoganda kwenye ukuta wa kizazi inetolewa nje. Endapo unapata mabonge madogo madogo ya damu ujue ni jambo la kawaida kabisa.

Kumbuka kwamba unapoanza hedhi ndio mwanzo wa mzunguko wako. Ni kipindi ambacho ukuta wa kizazi unabomoka kwasababu yai halikurtubishwa. Hedhi ni mchanganyiko wa damu ya ukuta wa mji wa mimba, maji maji ya ukeni na yai lisilorutubishwa.

Kumbuka pia kwamba siku ya kwanza ya hedhi inaweza kutoka nyingi na nzito kuliko siku zingine.

Hedhi kidogo inayoambatana na maumivu makali ya tumbo

Kama unapata hedhi nyepesi, nyekundu inaweza kuashiria kwamba mzunguko wa damu kwenye mfuko wa mimba ni mdogo. Unaweza kupunguza hali hii kwa kufanya masaji kwenye eneo la tumbo ukitumia mafuta ya mnyonyo, ama kitambaa kilicholowekwa kwenye maji ya moto.

Hedhi ya vipande vipande vya damu

Kadiri hedhi inavoendelea, unaweza kuanza kupata hedhi kama ya damu iliyoganwanyika vipande. Hii ni kawaida na inatokana na kuganda kwa damu kwenye ukuta wa kizazi. Hii ni kawaida kabisa na isikupe hofu. Damu hizi za kuganda zinaweza kuwa nyekundu sana, nyekundu mpauko au brown.

Hedhi nzito yenye weusi ama brown

Hii inaonesha kwamba kuna masalia ya damu ya zamani kwa hedhi iliyopita. Kubaki kwa damu husababishwa na flow ya polepole sana na mzunguko mdogo wa damu ndani ya mfuko wa mimba. Unaweza kurekebisha tatizo hili kwa kuhakikisha unakunywa maji ya kutosha, kufanya masaji eneo la tumbo na pia unaweza kujaribu uterus cleansing package yetu.

Hedhi nyepesi ya majimaji

Pale unapoelekea kumaliza hedhi yako, unaweza kupata damu nyepesi sana na nyembamba. Damu hii inaweza kuwa nyeusi pia kutokana na mwingiliano wa hewa ya oksijen na damu.

Kama hedhi inatoka ni damu mbichi na nyekundu ya kung’aa. inaonesha inatoka moja kwa moja kwenye kizazi. Na inaweza kuashiria jeraha kwenye kizazi au pengine mimba kuharibika.

Nenda hospitali mapema endapo utaona damu mbichi na nyepesi ikitoka kwenye kizazi, hasa kama umepitisha hedhi kwa siku kadha,maana yake kuna uwezekano kulikuwa na mimba.Pia kama unatoa mabonge ya damu mfululizo na ni makubwa, hakikisha unaenda hospitali.

Je hedhi ya mabonge inaashiria nini??

Kutokwa na mapande ya damu kwenye hedhi mfululizo ni kitu hatari na inaashiria changamoto fulani ya kiafya. Hedhi nzito kisha inachukua zaidi ya siku 5 inaweza kuashiria dalili za

 • Vimbe kwenye kizazi (fibroids)
 • Kutanuka kwa kizazi (adenomysis)
 • Vimbe kwenye mayai (PCOS)
 • Saratani kwenye kizazi
 • Changamoto ya tezi ya shingoni (thyroid condition)
 • Majeraha kutokana na kitanzi
 • Upungufu wa vitamin K

Lini unatakiwa kumwona daktari?

Endapo unapata dalili ambazo hujazoea kweye hedhi yako, pamoja na dalili zinazokunyima uhuru, unatakuwa kumwona daktari dalili hizi ni pamoja na

 • Kukosa nguvu na kuishiwa pumzi kwenye hedhi-hii yaweza kuashiria upungufu wa damu
 • Maumivu na kutokwa damu kwenye sex
 • Mabonge ya damu makubwa
 • Kutumia zaidi ya pedi mja kwa lisaa
 • Hedhi ya maji maji ya kung’aa au kijivu
 • Kupata hedhi nyingi zaidi ya siku 7

  Kwa maoni na ushauri tuandikie kwa whatsapp namba 0678626254.